Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Maria alifanya utaratibu wa kupandikiza mbegu ili apate watoto (IVF) akiwa na umri wa miaka 67. Aliingia kwenye kitabu cha Guineas Book of Records kwa kuwa mama aliyepata watoto akiwa na umri mkubwa zaidi.
Maria alipunguza umri wake kwa miaka 12 wakati akipata matibabu yake. Madaktari walimuuliza kama yuko kwenye ndoa na aliwajibu kuwa kuolewa na kuoa ni hiari ya mtu.
Maria alijifungua watoto mapacha wakiume Christian na Paul na aliwalea mpaka alipogundulika na saratani. Watoto wamerithiwa na mdogo wake ambae hana mtoto. Mdogo wake amemuahidi Maria atawalea watoto na kuwaeleza ukweli kuwa mama yao alifariki na alihatarisha maisha yake ili awape uhai.
Mama yake Maria alifariki akiwa na miaka 100 na Maria alikua na matumaini ya kuishi na kufika umri huu.