Mama na binti yake wahukumiwa kwa kuuza viungo vya miili ya wafu

mama D

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
19,981
Reaction score
35,581
Mmiliki wa zamani wa Chumba cha kuhifadhu maiti na mama yake wamehukumiwa kifungo cha jela huko Colorado baada ya kupasua mamia ya miili na kuuza sehemu za mwili.

Waendesha mashtaka walisema Megan Hess, 46, na Shirly Koch, 69, walikata maiti 560 na kuuza viungo vya miili bila idhini kati ya 2010 na 2018.

Wanawake wote wawili walikiri makosa ya ulaghai mapema mwaka huu.

Hess atafungwa jela 20, huku Koch akihukumiwa miaka 15 jela.

Kulingana na waendesha mashtaka huko Colorado, wawili hao mama na binti walivuna sehemu za miili, na wakati mwingine miili mizima katika na kuviuza .

Hess - ambaye aliendesha biashara ya Jumba la Mazishi la Sunset Mesa katika mji wa Montrose - alitoza familia hadi $1,000 (£834) kwa uchomaji maiti ambao haukufanyika na badala yake kuikabidhi miili hiyo kama michango bila malipo , waendesha mashtaka walisema.

"Wanawake hawa wawili waliwadhulumu wahasiriwa ambao waliwageukia wakati wa huzuni," Leonard Carollo, ajenti maalum wa FBI anayesimamia Denver, alisema katika taarifa.

"Lakini badala ya kutoa mwongozo, wanawake hawa wenye pupa walisaliti imani ya mamia ya wahasiriwa na kukata viungo vya wapendwa wao’

Kesi hiyo ilichochewa na uchunguzi wa Reuters, ambao ulisababisha FBI kuvamia nyumba hiyo mwaka wa 2018. Ni kinyume cha sheria nchini Marekani kuuza viungo, lakini uuzaji wa viungo vya mwili kwa sasa haudhibitiwi na sheria ya shirikisho ya Marekani.

Taarifa za waathiriwa waliojawa hisia zilitawala kikao cha hukumu cha Jumanne.

"Wakati Megan alipoiba moyo wa mama yangu, alivunja moyo wangu," alisema Nancy Overhoff, kulingana na Denver Post. Erin Smith alisema: "Tumekuja leo kusikia pingu zikikazwa."

Akiielezea kama "kesi ya kuhuzunisha zaidi ambayo nimewahi kukumbana nayo kwenye benchi", Jaji Christine Arguello aliamuru wanawake hao wawili wafungwe gerezani mara moja.

Kuna watu walikua wanasema watu wanaofa yia kazi mochwari akili hua zinahama sa sijajua huyu mama na bintie ni Nani aliyewahi fanya kazi hii kabla ya kumiliki hio mochwari binafsi na uhakika mmoja wao anauzoefu 99.9% kwa mama zinaangukia kwake.
 
Nilijua tu ni wanawake mana akili zao wanazijua wenyewe[emoji16][emoji16]

Btw, iyo mili inatofauti gani na mili iliyoliwa na wanyama au iliyopotelea uko baharini.[emoji124]
 
Lakini ukiiangalia kwa jicho jingine ukiacha la wizi. Wamesaidia watu kujua kuwa wanaweza kuendelea kuwa mchango mzuri kwa walio hai.

Mtu akifa tunachukua spea tunampatia alopungukiwa, show love even when dead✌.

Jamii ielimishwe kuhusu kudonate vya walofariki, badala ya kuwachomolea walio hai ambao nao bado wanavihitaji. Mfano figo hizi

Wizi sio mzuri, wafungwe.
 
Ni aina gani ya viungo vya miili hiyo walivyokuwa wanachukua? Je viungo hivyo vya miili iliyokufa vilikuwa vinatumiwa kwa kazi gani? (kama ni afrika tungesema ni kwa ajili ya ushirikina)
 
MIKA 3:2-3
Ninyi mnaoyachukia mema, na kuyapenda mabaya; ninyi mnaowachuna watu ngozi yao, na nyama mifupani mwao.
Naam, mnakula nyama ya watu wangu, na kuwachuna ngozi zao, na kuivunja mifupa yao; naam, kuwakata vipande vipande kama kwa kutiwa chunguni, na kama nyama sufuriani.

ZABURI 53:4
Je! Wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawakumwita MUNGU.

ZABURI 14:4
Je! Wote wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawamwiti BWANA.
 
Niemeparamia uzi nikijua ni habari za bongo kumbe ni za majuu, huko majuu hamnazo
 
MIKA 3:2-3
Ninyi mnaoyachukia mema, na kuyapenda mabaya; ninyi mnaowachuna watu ngozi yao, na nyama mifupani mwao.
Naam, mnakula nyama ya watu wangu, na kuwachuna ngozi zao, na kuivunja mifupa yao; naam, kuwakata vipande vipande kama kwa kutiwa chunguni, na kama nyama sufuriani.

ZABURI 53:4
Je! Wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawakumwita MUNGU.

ZABURI 14:4
Je! Wote wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawamwiti BWANA.
Hizo ni lugha za picha tu. Zilimaanisha matajiri, watawala au wenye nguvu walivyowadhulumu masikini na wanyonge.
 
Nani kukuambia au wapi paliandikwa kwamba "Hizo ni lugha za picha tu. Zilimaanisha matajiri"????

Kuyaelewa maandiko ni ufunuo ambao haupatikani kwa kufundishwa darasani

Fuata sheria za Mungu na utulia miguuni kwa waliochaguliwa na kupewa mafunuo kama mwanafunzi utafaidika
 
Mmiliki wa zamani wa Chumba cha kuhifadhu maiti na mama yake wamehukumiwa kifungo cha jela huko Colorado baada ya kupasua mamia ya miili na kuuza sehemu za mwili.

Waendesha mashtaka walisema Megan Hess, 46, na Shirly Koch, 69, walikata maiti 560 na kuuza viungo vya miili bila idhini kati ya 2010 na 2018.

Wanawake wote wawili walikiri makosa ya ulaghai mapema mwaka huu.

Hess atafungwa jela 20, huku Koch akihukumiwa miaka 15 jela.

Kulingana na waendesha mashtaka huko Colorado, wawili hao mama na binti walivuna sehemu za miili, na wakati mwingine miili mizima katika na kuviuza .

Hess - ambaye aliendesha biashara ya Jumba la Mazishi la Sunset Mesa katika mji wa Montrose - alitoza familia hadi $1,000 (£834) kwa uchomaji maiti ambao haukufanyika na badala yake kuikabidhi miili hiyo kama michango bila malipo , waendesha mashtaka walisema.

"Wanawake hawa wawili waliwadhulumu wahasiriwa ambao waliwageukia wakati wa huzuni," Leonard Carollo, ajenti maalum wa FBI anayesimamia Denver, alisema katika taarifa.

"Lakini badala ya kutoa mwongozo, wanawake hawa wenye pupa walisaliti imani ya mamia ya wahasiriwa na kukata viungo vya wapendwa wao’

Kesi hiyo ilichochewa na uchunguzi wa Reuters, ambao ulisababisha FBI kuvamia nyumba hiyo mwaka wa 2018. Ni kinyume cha sheria nchini Marekani kuuza viungo, lakini uuzaji wa viungo vya mwili kwa sasa haudhibitiwi na sheria ya shirikisho ya Marekani.

Taarifa za waathiriwa waliojawa hisia zilitawala kikao cha hukumu cha Jumanne.

"Wakati Megan alipoiba moyo wa mama yangu, alivunja moyo wangu," alisema Nancy Overhoff, kulingana na Denver Post. Erin Smith alisema: "Tumekuja leo kusikia pingu zikikazwa."

Akiielezea kama "kesi ya kuhuzunisha zaidi ambayo nimewahi kukumbana nayo kwenye benchi", Jaji Christine Arguello aliamuru wanawake hao wawili wafungwe gerezani mara moja.

Sura nzuri, roho mbaya!

Sijui kwanini shetwani anapenda kujificha nyuma ya wanawake wenye mishepu!
 
Back
Top Bottom