kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,846
- 20,319
Hii nchi inazidi kuoza tu hii imenisikitisha sana
MJAMZITO AFARIKI KATIKA MAZINGIRA YA UTATA KITUO CHA AFYA MBEZI YA KIMARA, DAR ES SALAAM!
Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!
Ndugu yetu Elizabeth Jonas Muyugi wa Kimara Temboni alikuwa ni mjamzito. Jana, 9 Agosti 2024 alifika Kituo cha Afya Mbezi tangu saa 2 asubuhi akiwa mzima wa afya. Alikuwa na dalili za uchungu wa kujifungua ndipo alifika Kituo cha Afya ambapo alikuwa akihudhuria Clinic. Picha hii alipigwa jana mchana akiwa Kituo cha Afya Mbezi.
Hadi saa 6 usiku, alikuwa mzima, lakini ilipofika saa 6.30 usiku, ndugu waliomba kuwa kama imeshindikana wamhamishe hospitali kwenda hospitali kubwa. Ilipofika saa 9 usiku mama wa Elizabeth aliiona Ambulance (gari la wagonjwa) na ilikaa muda mrefu wakiwa na mjadala wa wauguzi na baadaye ikaondoka bila ya kubeba mtu. Saa 12 asubuhi, ilifika tena ambulance na ikaondoka bila mgonjwa. Lakini baada ya hapo, mume wa Elizabeth alitaka kujua juu ya hali ya mgonjwa. Muuguzi alijibu kuwa yupo safi hana changamoto yeyote. Saa 12 asubuhi, mama alitaka kupeleka chai wamkazuia. Lakini muda mchache baadaye tukapewa taarifa ya kuwa Elizabeth amefariki dunia.
Aliitwa daktari bingwa kufanya utenganishaji wa mama na mtoto. Wamefanya hapa na ndipo daktari akaita ndugu kutueleza kwamba report (taarifa ya kitabu) yake inaonesha kuwa hakuna shida yoyote. Sisi tunahisi mgonjwa alifariki mapema na ndiyo maana Ambulance iliondoka bila kubeba mgonjwa.
Wauguzi wa Kituo hiki walipoulizwa walifanya jitihada gani kuokoa mtoto au kutenganisha na mama, walisema kuwa hawana experience (ujuzi) ya kumukoa mtoto. Sisi tunaona kuna uzembe. Hawa hawana chumba cha upasuaji, hawana wataalamu, Kituo ni kidogo. Wanakiri kuwa kuna uzembe umefanyika lakini hawatoi majibu ya kueleweka kwani ni Kituo cha Afya ambacho hakina wataalamu. Lakini ni kwa nini waliendelea kukaa na mgonjwa wakati walijua kuwa hawana wataalam wanakuwa kimya.
Daktari Mkuu kafika muda huu ametenganisha mtoto na mama ambao wote ni marehemu. Na wanasema kuwa kesi hii hawajawahi kukutana nayo. Mgonjwa hakuishiwa damu, hakuwa na pressure, protine kwa mkojo ilikuwa safi, nk. Tunajiuliza ni wangapi wanakufa kwa staili hii? Mtoto pia amekufa kwa kuondolewa tumboni muda huu.
Ni dhahiri kuwa hatuwezi kuurudisha uhai wa Elizabeth wetu sasa hivi, lakini tunataka serikali iweke vitendea kazi na madaktari bingwa huku ili Watanzania wengi wasipoteze uhai kesho, na siku zijazo. Kinatuumiza ni kuwa, Elizabeth pia aliomba kama haiwezekani hapa basi apelekwe hospitali yeyote akafanyiwe upasuaji lakini pia hawakumsikiliza. Ombi lake lilitolewa mapema sana. Huo ni uzembe wa hali ya juu.
Muda huu tunaelekea Mlonganzila kupeleka mwili wa Elizabeth na mwili wa mtoto wake.
Ni mimi nduguye Elizabeth!
Mbezi, Dar es Salaam; 10 Agosti 2024
Ndugu Watanzania!
Taarifa hii inasikitisha sana kwa upande wetu, sisi Askofu Mwamakula tunaomba mamlaka husika kufanya uchunguzi wa tukio hili kubaini ukweli wa hisia zilizotolewa na ndugu juu ya kifo hicho ili kuchukua hatua zaidi kwa ajili ya kuboresha utendaji wa Kituo hicho na kuokoa maisha ya watu wengine siku zijazo. Lakini pia tunasisitiza ndugu wa marehemu, wasikilizwe kuhusu kilichotokea sambamba na kuwahoji pia wauguzi au waganga wa Kituo hicho.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 10 Agosti 2024; saa 8:40 alasiri