Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yule aliyesema maisha ya bongo ni less stressful akifananisha na ya Ulaya alikuwa anamaanisha nini ?Nimesoma hii habari nikapanda juu kuangalia tarehe, unajua kwanini? Kwasababu nilihisi nishaisoma. Maanake nini? Ni kwamba haya matukio yanajirudia kila siku na hakuna mabadiliko yoyote. Hii nchi imeoza.
Yule ni wale ameajiriwa,mshahara 1.5m,anaendesha tako la nyani basi anasahau kuwa 90% ya watu nchi hii ni masikini wa kutupwa.Yule aliyesema maisha ya bongo ni less stressful akifananisha na ya Ulaya alikuwa anamaanisha nini ?
Tupe mpango mkakati mkuu.Kwa hiyo tunaongea tu ili kupooza hasira, au kuna mpango mkakati wa kuwawajibisha wazembe hao?
Hebu semeni kitu haraka aseee!
Watumishi wa hospitali za serikali, polisi, ni watu wanaoishi kwa msongo wa, mawazo kutokana na maisha magumu,wapo tayari kufanya chochote wapate pesa ya kupunguza maumivu, sasa ukikutana nao, na, hauna kitu, lazima, uumie,Hii nchi inazidi kuoza tu hii imenisikitisha sana
MJAMZITO AFARIKI KATIKA MAZINGIRA YA UTATA KITUO CHA AFYA MBEZI YA KIMARA, DAR ES SALAAM!
Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!
Ndugu yetu Elizabeth Jonas Muyugi wa Kimara Temboni alikuwa ni mjamzito. Jana, 9 Agosti 2024 alifika Kituo cha Afya Mbezi tangu saa 2 asubuhi akiwa mzima wa afya. Alikuwa na dalili za uchungu wa kujifungua ndipo alifika Kituo cha Afya ambapo alikuwa akihudhuria Clinic. Picha hii alipigwa jana mchana akiwa Kituo cha Afya Mbezi.
Hadi saa 6 usiku, alikuwa mzima, lakini ilipofika saa 6.30 usiku, ndugu waliomba kuwa kama imeshindikana wamhamishe hospitali kwenda hospitali kubwa. Ilipofika saa 9 usiku mama wa Elizabeth aliiona Ambulance (gari la wagonjwa) na ilikaa muda mrefu wakiwa na mjadala wa wauguzi na baadaye ikaondoka bila ya kubeba mtu. Saa 12 asubuhi, ilifika tena ambulance na ikaondoka bila mgonjwa. Lakini baada ya hapo, mume wa Elizabeth alitaka kujua juu ya hali ya mgonjwa. Muuguzi alijibu kuwa yupo safi hana changamoto yeyote. Saa 12 asubuhi, mama alitaka kupeleka chai wamkazuia. Lakini muda mchache baadaye tukapewa taarifa ya kuwa Elizabeth amefariki dunia.
Aliitwa daktari bingwa kufanya utenganishaji wa mama na mtoto. Wamefanya hapa na ndipo daktari akaita ndugu kutueleza kwamba report (taarifa ya kitabu) yake inaonesha kuwa hakuna shida yoyote. Sisi tunahisi mgonjwa alifariki mapema na ndiyo maana Ambulance iliondoka bila kubeba mgonjwa.
Wauguzi wa Kituo hiki walipoulizwa walifanya jitihada gani kuokoa mtoto au kutenganisha na mama, walisema kuwa hawana experience (ujuzi) ya kumukoa mtoto. Sisi tunaona kuna uzembe. Hawa hawana chumba cha upasuaji, hawana wataalamu, Kituo ni kidogo. Wanakiri kuwa kuna uzembe umefanyika lakini hawatoi majibu ya kueleweka kwani ni Kituo cha Afya ambacho hakina wataalamu. Lakini ni kwa nini waliendelea kukaa na mgonjwa wakati walijua kuwa hawana wataalam wanakuwa kimya.
Daktari Mkuu kafika muda huu ametenganisha mtoto na mama ambao wote ni marehemu. Na wanasema kuwa kesi hii hawajawahi kukutana nayo. Mgonjwa hakuishiwa damu, hakuwa na pressure, protine kwa mkojo ilikuwa safi, nk. Tunajiuliza ni wangapi wanakufa kwa staili hii? Mtoto pia amekufa kwa kuondolewa tumboni muda huu.
Ni dhahiri kuwa hatuwezi kuurudisha uhai wa Elizabeth wetu sasa hivi, lakini tunataka serikali iweke vitendea kazi na madaktari bingwa huku ili Watanzania wengi wasipoteze uhai kesho, na siku zijazo. Kinatuumiza ni kuwa, Elizabeth pia aliomba kama haiwezekani hapa basi apelekwe hospitali yeyote akafanyiwe upasuaji lakini pia hawakumsikiliza. Ombi lake lilitolewa mapema sana. Huo ni uzembe wa hali ya juu.
Muda huu tunaelekea Mlonganzila kupeleka mwili wa Elizabeth na mwili wa mtoto wake.
Ni mimi nduguye Elizabeth!
Mbezi, Dar es Salaam; 10 Agosti 2024
Ndugu Watanzania!
Taarifa hii inasikitisha sana kwa upande wetu, sisi Askofu Mwamakula tunaomba mamlaka husika kufanya uchunguzi wa tukio hili kubaini ukweli wa hisia zilizotolewa na ndugu juu ya kifo hicho ili kuchukua hatua zaidi kwa ajili ya kuboresha utendaji wa Kituo hicho na kuokoa maisha ya watu wengine siku zijazo. Lakini pia tunasisitiza ndugu wa marehemu, wasikilizwe kuhusu kilichotokea sambamba na kuwahoji pia wauguzi au waganga wa Kituo hicho.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 10 Agosti 2024; saa 8:40 alasiri
Ifike hatua JF iwe jukwaa la kuchukua hatua, hasa katika masuala ya misingi kama haya.Tupe mpango mkakati mkuu.
Ujiandae pia kwenye safu madhubuti ya ulinzi, maana kushinda kesi ni hatua moja tu ya awali kuelekea ushindi kamili.Sababu kuu hapo ni umasikini na ujinga(kukosa Elimu).
Ndio mimi natamani nikasome medical legals ili nije niwatetee watu kama hawa.
Kuna watumishi wengi watafungwa kama hii kitu ikifika bongo.
Watanzania tunakufa kikondoo sana. Vitu vingine bila kukiwasha havitabadilika.Hicho kituo cha Mbezi kina mapungufu Mengi sana ya kutoa huduma,kuna mama alifika hapo mida ya saa 6 usiku kupata huduma maana alikuwa na mtoto mchanga alishikwa na ugonjwa ghafla.....lakini hawakupata huduma yeyote waliamua kurudi nyumbani na hapo walikuwa wametoka maeneo ya Kontena....sasa kama kituo kipo na hakitoi huduma stahiki kuna umuhimu gani wa kuwepo!!!!!
Sasa kwa andiko lako utasemaje ameuwawa, je wajua masaa yote yale ,watoa Huduma wamepigana kiasi gani?, je unajua kwenye uzazi zipo changamoto nyingi ambazo zinaweza mpelekea mzazi mda wowote hali ya kiafya kwake kubadilika ? Na ndo maana mama akijifungua lazima kaa chini ya uangalizi kwa masaa 24 ,unafikiri kwa nini?Hii nchi inazidi kuoza tu hii imenisikitisha sana
MJAMZITO AFARIKI KATIKA MAZINGIRA YA UTATA KITUO CHA AFYA MBEZI YA KIMARA, DAR ES SALAAM!
Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!
Ndugu yetu Elizabeth Jonas Muyugi wa Kimara Temboni alikuwa ni mjamzito. Jana, 9 Agosti 2024 alifika Kituo cha Afya Mbezi tangu saa 2 asubuhi akiwa mzima wa afya. Alikuwa na dalili za uchungu wa kujifungua ndipo alifika Kituo cha Afya ambapo alikuwa akihudhuria Clinic. Picha hii alipigwa jana mchana akiwa Kituo cha Afya Mbezi.
Hadi saa 6 usiku, alikuwa mzima, lakini ilipofika saa 6.30 usiku, ndugu waliomba kuwa kama imeshindikana wamhamishe hospitali kwenda hospitali kubwa. Ilipofika saa 9 usiku mama wa Elizabeth aliiona Ambulance (gari la wagonjwa) na ilikaa muda mrefu wakiwa na mjadala wa wauguzi na baadaye ikaondoka bila ya kubeba mtu. Saa 12 asubuhi, ilifika tena ambulance na ikaondoka bila mgonjwa. Lakini baada ya hapo, mume wa Elizabeth alitaka kujua juu ya hali ya mgonjwa. Muuguzi alijibu kuwa yupo safi hana changamoto yeyote. Saa 12 asubuhi, mama alitaka kupeleka chai wamkazuia. Lakini muda mchache baadaye tukapewa taarifa ya kuwa Elizabeth amefariki dunia.
Aliitwa daktari bingwa kufanya utenganishaji wa mama na mtoto. Wamefanya hapa na ndipo daktari akaita ndugu kutueleza kwamba report (taarifa ya kitabu) yake inaonesha kuwa hakuna shida yoyote. Sisi tunahisi mgonjwa alifariki mapema na ndiyo maana Ambulance iliondoka bila kubeba mgonjwa.
Wauguzi wa Kituo hiki walipoulizwa walifanya jitihada gani kuokoa mtoto au kutenganisha na mama, walisema kuwa hawana experience (ujuzi) ya kumukoa mtoto. Sisi tunaona kuna uzembe. Hawa hawana chumba cha upasuaji, hawana wataalamu, Kituo ni kidogo. Wanakiri kuwa kuna uzembe umefanyika lakini hawatoi majibu ya kueleweka kwani ni Kituo cha Afya ambacho hakina wataalamu. Lakini ni kwa nini waliendelea kukaa na mgonjwa wakati walijua kuwa hawana wataalam wanakuwa kimya.
Daktari Mkuu kafika muda huu ametenganisha mtoto na mama ambao wote ni marehemu. Na wanasema kuwa kesi hii hawajawahi kukutana nayo. Mgonjwa hakuishiwa damu, hakuwa na pressure, protine kwa mkojo ilikuwa safi, nk. Tunajiuliza ni wangapi wanakufa kwa staili hii? Mtoto pia amekufa kwa kuondolewa tumboni muda huu.
Ni dhahiri kuwa hatuwezi kuurudisha uhai wa Elizabeth wetu sasa hivi, lakini tunataka serikali iweke vitendea kazi na madaktari bingwa huku ili Watanzania wengi wasipoteze uhai kesho, na siku zijazo. Kinatuumiza ni kuwa, Elizabeth pia aliomba kama haiwezekani hapa basi apelekwe hospitali yeyote akafanyiwe upasuaji lakini pia hawakumsikiliza. Ombi lake lilitolewa mapema sana. Huo ni uzembe wa hali ya juu.
Muda huu tunaelekea Mlonganzila kupeleka mwili wa Elizabeth na mwili wa mtoto wake.
Ni mimi nduguye Elizabeth!
Mbezi, Dar es Salaam; 10 Agosti 2024
Ndugu Watanzania!
Taarifa hii inasikitisha sana kwa upande wetu, sisi Askofu Mwamakula tunaomba mamlaka husika kufanya uchunguzi wa tukio hili kubaini ukweli wa hisia zilizotolewa na ndugu juu ya kifo hicho ili kuchukua hatua zaidi kwa ajili ya kuboresha utendaji wa Kituo hicho na kuokoa maisha ya watu wengine siku zijazo. Lakini pia tunasisitiza ndugu wa marehemu, wasikilizwe kuhusu kilichotokea sambamba na kuwahoji pia wauguzi au waganga wa Kituo hicho.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 10 Agosti 2024; saa 8:40 alasiri
Sasa kwa andiko lako utasemaje ameuwawa, je wajua masaa yote yale ,watoa Huduma wamepigana kiasi gani?, je unajua kwenye uzazi zipo changamoto nyingi ambazo zinaweza mpelekea mzazi mda wowote hali ya kiafya kwake kubadilika ? Na ndo maana mama akijifungua lazima kaa chini ya uangalizi kwa masaa 24 ,unafikiri kwa nini?
Sikiliza msipende kuja na maanndiko ya kuzua taharuki bila sababu, hivi kwa akili yako timamu watoa huduma wa afya wapo pale kuua wagonjwa ?
Ni kwa sababu ni msiba na toa pole vinginevyo watoa huduma wa kituo hisika wanatakiwa kukufungulia kesi kwa kuwachafua kwamba Uyo mama kauwawa , Tuache jua jua kwenye fani za watu,
Hivi unajua mtumishi wa afya mteja au Mgonjwa wake akifariki baada ya kuangaika naye kwa mda mrefu anavyoumia sema ,huwa wanajikaza tokana na kazi nyenyewe .