DOKEZO Mama na mtoto wadaiwa kufa hosptalini Kimara kwa uzembe wa watoa huduma

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
R.I.P Lizzy, hospital zetu zina uzembe mwingi ukilegeza Tu umekwenda na maji!
 
Nimesoma hii habari nikapanda juu kuangalia tarehe, unajua kwanini? Kwasababu nilihisi nishaisoma. Maanake nini? Ni kwamba haya matukio yanajirudia kila siku na hakuna mabadiliko yoyote. Hii nchi imeoza.
Yule aliyesema maisha ya bongo ni less stressful akifananisha na ya Ulaya alikuwa anamaanisha nini ?
 
Watumishi wa hospitali za serikali, polisi, ni watu wanaoishi kwa msongo wa, mawazo kutokana na maisha magumu,wapo tayari kufanya chochote wapate pesa ya kupunguza maumivu, sasa ukikutana nao, na, hauna kitu, lazima, uumie,
 
Tupe mpango mkakati mkuu.
Ifike hatua JF iwe jukwaa la kuchukua hatua, hasa katika masuala ya misingi kama haya.

Kadiri tunavyozidi kuongea, akina sie vichwa vinapata moto, huzuni, ghadhabu na wahaka kwa pamoja.

Nasemaje! Emu tufanyeni jambo la maana kuhusu hili!

Sisi ndio sauti za maamuzi za wale wanaoonewa!
 
Kifupi inauma sana pale unapompoteza mpendwa/wapendwa wako, kwa sababu tu ya uzembe wa hao watoa huduma za afya.
 
Sababu kuu hapo ni umasikini na ujinga(kukosa Elimu).

Ndio mimi natamani nikasome medical legals ili nije niwatetee watu kama hawa.

Kuna watumishi wengi watafungwa kama hii kitu ikifika bongo.
 
Kuna mijitu kutwa kusifia,anaupiga nwingi
 
Sababu kuu hapo ni umasikini na ujinga(kukosa Elimu).

Ndio mimi natamani nikasome medical legals ili nije niwatetee watu kama hawa.

Kuna watumishi wengi watafungwa kama hii kitu ikifika bongo.
Ujiandae pia kwenye safu madhubuti ya ulinzi, maana kushinda kesi ni hatua moja tu ya awali kuelekea ushindi kamili.
 
Poleni sana wafiwa kwa pigo hilo ila msinge pokea miwili hiyo kirahisi hivyo. Mngeisusa mpaka viongozi wa ngazi za juu wapate habari. Inavyo onesha imeisha hiyo wamewaachia mkazike Marehemu wenu. Poleni sana
 
Nkionaga mtu yeyote anajiita influencer sijui staaa sijui ana follower wengi anasema Ccm hoyeee naweza mkata kofi
 
Kuna uzi mlikuwa mlikuwa mnasifia mama mama yupi wanani?? Nyie mnakrem maisha ila hali halisi mazwazwa ni watu wanashida hadi wanazima halafu mama mitano tena wapi where hajatatua kitu hata hizo shule nothing bana
 
Watanzania tunakufa kikondoo sana. Vitu vingine bila kukiwasha havitabadilika.
 
Sasa kwa andiko lako utasemaje ameuwawa, je wajua masaa yote yale ,watoa Huduma wamepigana kiasi gani?, je unajua kwenye uzazi zipo changamoto nyingi ambazo zinaweza mpelekea mzazi mda wowote hali ya kiafya kwake kubadilika ? Na ndo maana mama akijifungua lazima kaa chini ya uangalizi kwa masaa 24 ,unafikiri kwa nini?

Sikiliza msipende kuja na maanndiko ya kuzua taharuki bila sababu, hivi kwa akili yako timamu watoa huduma wa afya wapo pale kuua wagonjwa ?

Ni kwa sababu ni msiba na toa pole vinginevyo watoa huduma wa kituo hisika wanatakiwa kukufungulia kesi kwa kuwachafua kwamba Uyo mama kauwawa , Tuache jua jua kwenye fani za watu,

Hivi unajua mtumishi wa afya mteja au Mgonjwa wake akifariki baada ya kuangaika naye kwa mda mrefu anavyoumia sema ,huwa wanajikaza tokana na kazi nyenyewe .
 

Siku yakikukuta usije kulia lia hapa jukwaani. Kama kuna uzembe umefanyika wacha usemwe na ukemewe. Habari za kutishia watu kuwafungulia kesi hazitusaidii kama Taifa. Mgonjwa kaomba rufaa wamemnyima, wanaulizwa walichukua hatua gani kumtenganisha mama na mtoto wanasema hawana ujuzi. Acha kutetea uzembe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…