Mama na mwanaye wakutwa wamefariki dunia chumbani kwa kukosa hewa

Mama na mwanaye wakutwa wamefariki dunia chumbani kwa kukosa hewa

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,402
Reaction score
4,532
Nimeona nitoe taaluma hapa kusaidia jamii
Ukilala usiku hasa hasa kama nyumba haina madirisha ya kuingiza hewa ya kutosha kisha ukaingiza jiko la mkaa kinachotokea ni kwamba hewa ya oxygen iliyopo chumbani ina react na mkaa na kutokea hewa ya carbon dioxide

C + O2 = CO2
hii carbon dioxide inajaa chumbani inazidi nguvu oxygen sasa hii carbon dioxide ina react tena na mkaa na kutengeneza hewa ya sumu isiyo na harufu ya carbon monoxide
C + CO2 = 2CO
hii carbon monoxide kwa vile ina bond moja tu au tuseme C-O inaingia kwenye mapafu na kupambana na chembe nyekundu za damu zinaitwa oxyhaemoglobin na kufanya binding hivyo damu inashindwa kufanya kazi yake iliyokusudiwa hivyo matokeo yake ni kifo.

Uzuri au ubaya wa kifo chake ni kwamba unakufa huku unajiona kabisa unajisikia mchovu na unajiwa na wazo unyanyuke ufungue mlango lakini unakuwa huwezi unajisikia raha sana kuendelea kulala na hapo ndio kifo kinapokupata sasa

Tukio hili limetokea Kagera usiku wa kuamkia 30th Jan 2025
Chanzo Mwananchi 30th Jan 2025
 
Mkuu naona umechambua mambo lakini si kweli kwamba kinachowaua ni carbon dioxide bali ni carbon monoxide. Ingekuwa ni carbon dioxide huenda wangekuwa wanashtuka na kuamka. Carbon monoxide haina ladha, haina harufu, haina rangi ndiyo maana watu huwa wanauawa na carbon monoxide bila hata kutambua. Wewe ukikaa kwenye chumba kilichojaa carbon dioxide utashtuka.
Japo mkaa unatoa carbon dioxide, pia kama kuna limited supply of oxygen unazalisha carbon monoxide kwa kiasi kikubwa na ndiyo huwa inaua watu haraka sana na pasipo wao hata kuwa na utambuzi.
Mbona kaandika ni kaboni monoksaidi ndio inayoua. Huenda hukumsoma hadi mwisho.
 
Je ukiingiza kuni ndani ukawasha
Moto wa kuni sio mbaya ila sasa zile kuni kumbuka zitaungua mwisho zitatengeneza mkaa
sema nini bahati ya kuni zinawaka na ule mkaa unaungua haraka na kuwa majivu na ndio maana mababu zetu walikuwa hawapati hii shida ya vifo nyumba zao zile za zamani mkaa wenyewe kama mkaa ndio hatari zaidi sababu unawaka taratibu.
 
Mkuu naona umechambua mambo lakini si kweli kwamba kinachowaua ni carbon dioxide bali ni carbon monoxide. Ingekuwa ni carbon dioxide huenda wangekuwa wanashtuka na kuamka. Carbon monoxide haina ladha, haina harufu, haina rangi ndiyo maana watu huwa wanauawa na carbon monoxide bila hata kutambua. Wewe ukikaa kwenye chumba kilichojaa carbon dioxide utashtuka.
Japo mkaa unatoa carbon dioxide, pia kama kuna limited supply of oxygen unazalisha carbon monoxide kwa kiasi kikubwa na ndiyo huwa inaua watu haraka sana na pasipo wao hata kuwa na utambuzi.
Nisome vizuri mkuu
hakuna mahali nimeandika carbon dioxide ndio inayoua nahisi umesoma haraka
ahsante kwa kunikosoa
 
Daaaa kama kifo hiki kinaleta na raha yakujisikia kulala naoana ni kizuri zaidi.
 
Hii habari ya majiko kila wakati inatokea na watu hawajifunzi.

Pengine huwaza nikitaka kulala nitalitoa nje au nitalizima halafu wanapitiwa jumla.
 
Wamekufa kifo cha kusikitisha maskini...daaah
Mtu akiweka jiko la mkaa linalowaka kwenye chumba kisichoingiza hewa anaweza kufa kwa sababu ya sumu ya gesi ya monoksidi ya kaboni (carbon monoxide - CO). Hii ni gesi hatari inayozalishwa wakati mkaa au mafuta yanapoungua bila hewa ya kutosha (uchomaji usiokamilika).

Mchakato wa Hatari Unavyotokea:

1. Ukosefu wa Oksijeni:

Mkaa unapowaka, hutumia oksijeni (O₂) kutoka kwenye hewa na kutoa gesi ya kaboni dioksidi (CO₂) na joto.

Katika chumba kisicho na mzunguko wa hewa, oksijeni hupungua haraka, na uchomaji wa mkaa hauwezi kukamilika vizuri.



2. Uzalishaji wa Monoksidi ya Kaboni (CO):

Kwa sababu hakuna oksijeni ya kutosha, badala ya kuzalisha CO₂ pekee, mkaa huanza kutoa monoksidi ya kaboni (CO).

CO ni gesi isiyo na harufu, rangi, wala ladha, hivyo ni vigumu kuitambua bila vifaa maalum.



3. Sumu ya Monoksidi ya Kaboni Katika Mwili:

Mtu anapovuta hewa yenye CO, molekuli za CO huingia kwenye damu kupitia mapafu.

CO huungana na hemoglobini kwenye damu, ikichukua nafasi ya oksijeni. Hemoglobini inapaswa kubeba oksijeni kwenda kwenye seli, lakini ikiwa na CO, haziwezi kufanya kazi hiyo.

Matokeo yake ni kwamba mwili haupati oksijeni ya kutosha, hali inayosababisha upungufu wa oksijeni kwenye viungo muhimu kama ubongo na moyo (hypoxia).



4. Dalili za Sumu ya CO:

Kizunguzungu

Kichefuchefu

Uchovu usio wa kawaida

Maumivu ya kichwa

Kupoteza fahamu

Kupumua kwa shida, ambayo inaweza kupelekea kifo ikiwa mtu hatapata hewa safi kwa haraka.




Kwanini Mtu Anaweza Kufa?

Ikiwa CO itaendelea kujaa kwenye damu, ubongo na moyo hukosa oksijeni kabisa, na kusababisha mtu kupoteza fahamu na hatimaye moyo kusimama (cardiac arrest).

Ikiwa mtu hatapewa msaada kwa haraka (kama kuhamishwa kwenye eneo lenye hewa safi na kupatiwa oksijeni), anaweza kufariki.


Jinsi ya Kuepuka Hatari:

Kamwe usitumie jiko la mkaa ndani ya chumba kisicho na uingizaji wa hewa.

Hakikisha kuna madirisha au njia za kupitisha hewa ili kuongeza mzunguko wa oksijeni.

Ikiwezekana, tumia vifaa vya kupima viwango vya CO ndani ya nyumba.

Ukianza kuhisi dalili za kizunguzungu au kichefuchefu ukiwa karibu na mkaa unaowaka, toka nje mara moja na upate hewa safi.


Kwa ufupi, maji ukiyazidi hutapika—vivyo hivyo, ikiwa CO itazidi mwilini, huwezi kupumua, na unaweza kufa bila hata kujua kinachoendelea!
 
macho yatakuwasha, kamasi jesepi litakutoka kisha utatoka nje mbio kwenda kutafuta nafuu
Duh, mambo ya kemia haya!Ule mchakato wa mchanganyiko wa hizo hewa ndiyo huleta hivyo vitu??
 
Nimekurupuka kama watanzania tunavyokurupuka sikusoma mpaka mwisho. Nisamehe bure.
usijali ndugu yangu mambo mengi sana maisha magumu,january nayo hii bado makovu yake hayaishi,huku tena Trump ameweka ngumu tusiende Marekani,ndgu zetu waliokule wanarudishwa sasa watakuwa mzigo kwetu tutabanana nao mtaani,Trump tena kaweka kauzibe dawa za kufubaza ukimwi yaani lazima akili itangulie kidogo kwa muda
 
Back
Top Bottom