Mama ni wakati wako AMUA!

Mama ni wakati wako AMUA!

1120ulimwengu

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2013
Posts
252
Reaction score
422
Jambo moja kubwa na hakika ambalo ukiwauliza raia wa nchi nyingi za Afrika magharibi au tuseme global south kuwa wanajua nn kuhusu Tanzania kwanza watakwambia wanaRais mwanamke!Wanaweza kukwambia pia juu ya mt.Kilimanjaro,Serengeti,baba wa Taifa JK Nyerere,beautiful flag,wasanii kama Diamond na Harmonize nk lakini first things first Rais Mwanamke mama SAMIA SULUHU HASSAN.Kwakweli ni jambo la kujivunia.
Na kwakuwa duniani tunapita nakuomba Mama Samia amua uache legacy nzuri,unaweza kuwa umwema,umsafi na unaipenda Tz sana lakini amini kabisa unaweza kuwa umezungukwa na walafi,criminals,mafisadi na corrupted people haswaa.Hawa hawawezi kuifanya legacy yako kuwa nzuri.Unapokuwa Rais unatakiwa uache alama wasije wajukuu wakasema alikuwepo Rais mwanamke mzuri,mwema,msafi na mzalendo lakini alizungukwa na walarushwa,wezi na mafisadi!Kama inakupendeza amrisha mawaziri wote na hata washauri wako wachunguzwe iwe kwa siri au wazi.Usizungukwe na watu wasiowaaminifu.Watu huangushwa na watu wanaowaamini sana sasa watu wanaokushauri na unaowaona kama wakweli waweza kuwa ndio wanaocheza michezo inayoleta hatari sana kwenye legacy yako.
Kwakua wew husoma JF nakuomba mama chunguza mawaziri wako hawa.Tunawasiwasi nao haiwezekan wew utafute hela kila siku lakini huku chini nafuu haipo!Mama amini usiamini ukickia milio ya maumivu ni mingi(ikiwa ni pamoja na hizo habar unazoona hazichujwi kushamiri) ujue kuna mahali mtu amefinywa,kilio ni matokeo ya maumivu.
Chondechonde mama wachunguze mawaziri(the executive pia) na washauri wako,mbona Bukele kaagiza hivyo.Hautakuwa wa kwanza na wala hautakuwa wa mwisho kufanya jambo zuri kama hili🙏🏿
 
Oya kashasema yeye ni chura unatakaje sasa mzee...Mwigulu pamoja na ujinga alio nao kwa kuua uchumi wa nchi ila ndo anamuona kichwa.
 
Kwanza, siamini kwenye kujulikana na mataifa mengine, hiyo Tanzania peke yake ni mpaka uitaje East Africa, hao kina Diamond ndo kabisaaa, labda useme wanajulikana kwa watu maarufu wachache walioshirikiana nao!

Kuhusu kuamua, mara ngapi sasa? Au hujui alichoamua kufanya?
- Basi ujue, kikubwa kuliko vyote ni kuuza pande la ardhi, hivyo vingine vingine kama kuimalizia Tanganyika, kuimarisha ustawi wa Abdul n.k ni vile vidogo dogo alivyoamua kuvifanya pia akiwa sanjari na cream yake ya akina Bashi, Madelu, Janu, Mbrawa, Hussein etc
 
Kuna nafasi mbili muhimu amezipata, halafu katika hali ya kushangaza; amezifanyia masihara.
1) Uundwaji wa Tume Huru ya Uchaguzi
2) Kuirejesha mezani ile Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba.

Angehakikisha tu hivi vitu viwili vinakamilika kwa usahihi, halafu angewaachia wababe wapambane wenyewe 2025. Na yeye angekaa zake pembeni.
Ilà sasa ndiyo hivyo tena. Tamaa ya madaraka imemshamvuruga akili.
 
Jambo moja kubwa na hakika ambalo ukiwauliza raia wa nchi nyingi za Afrika magharibi au tuseme global south kuwa wanajua nn kuhusu Tanzania kwanza watakwambia wanaRais mwanamke!Wanaweza kukwambia pia juu ya mt.Kilimanjaro,Serengeti,baba wa Taifa JK Nyerere,beautiful flag,wasanii kama Diamond na Harmonize nk lakini first things first Rais Mwanamke mama SAMIA SULUHU HASSAN.Kwakweli ni jambo la kujivunia.
Na kwakuwa duniani tunapita nakuomba Mama Samia amua uache legacy nzuri,unaweza kuwa umwema,umsafi na unaipenda Tz sana lakini amini kabisa unaweza kuwa umezungukwa na walafi,criminals,mafisadi na corrupted people haswaa.Hawa hawawezi kuifanya legacy yako kuwa nzuri.Unapokuwa Rais unatakiwa uache alama wasije wajukuu wakasema alikuwepo Rais mwanamke mzuri,mwema,msafi na mzalendo lakini alizungukwa na walarushwa,wezi na mafisadi!Kama inakupendeza amrisha mawaziri wote na hata washauri wako wachunguzwe iwe kwa siri au wazi.Usizungukwe na watu wasiowaaminifu.Watu huangushwa na watu wanaowaamini sana sasa watu wanaokushauri na unaowaona kama wakweli waweza kuwa ndio wanaocheza michezo inayoleta hatari sana kwenye legacy yako.
Kwakua wew husoma JF nakuomba mama chunguza mawaziri wako hawa.Tunawasiwasi nao haiwezekan wew utafute hela kila siku lakini huku chini nafuu haipo!Mama amini usiamini ukickia milio ya maumivu ni mingi(ikiwa ni pamoja na hizo habar unazoona hazichujwi kushamiri) ujue kuna mahali mtu amefinywa,kilio ni matokeo ya maumivu.
Chondechonde mama wachunguze mawaziri(the executive pia) na washauri wako,mbona Bukele kaagiza hivyo.Hautakuwa wa kwanza na wala hautakuwa wa mwisho kufanya jambo zuri kama hili🙏🏿
Mbwa akikaribia kufa hupoteza uwezo wa kunusa . Mwache aendelee kuwa kiziwi.
 
Back
Top Bottom