hahahahahah lol

Sis kweli leo umeniacha hoi

mie tangu jana nacheka tu daahh

umenikumbusha sabena jinsi watu tulivyokuwa tuna banana

Basi limesheena ile mabaya lakini utasikia kondactor anasema

"panda mama basi sio ndoo ya maji halijai hili " Dereva ndo kauchuna....

Zile ngozi za kimang'ati zinanuka, huyu anatapika mtoto kajinyea daaaahh

mmhhhh Sintokaa nisahau sabena ukitaka kutapika unapita watu kama kumi hivi

kufika dirishani kilicho kuwa kinaniudhi kuliko chote ni pale mtu anakula karanga na fanta

dahhh kilicho fuatia tuache tu ... halafu sasa hiyo barabara basi lina linaenda juu chini, juu , chini

ukifika uendako unahisi kama ulikuwa unapalilia heka 10 za mahindi , nguvu zimeisha ajili ya kutapika...