Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Nitangulize angalizo, sio wote wasiozingatia usafi, naamini ni 6% ndo wanawaharibia wenzao!
Ngoja niwape story. Nyakati za alfajiri nimemsindikiza bonge wangu kuelekea ubungo kwa wifi yake akae huko ili kesho kutwa aelekee Kibaha!
Wakati narejea nyumbani, muda ule nimeshuka kwenye daladala (wakuu mimi sina gari [emoji16]) nikaona bora nipate kifungua kinywa, maake kwangu gesi imekata! Nikaangaza chocho kwa chocho nikakutana na migahawa miwili imeungana, moja lina sister pic qal ndani na la pili lina mama mtu mzima, halafu juu ya kimeza chake kuna deli la maandazi [emoji39][emoji39]
Sijui ilikuwaje nikajikuta kwenye kimgahawa cha mwana mama kuyafuata yale maandazi pasi na kufikiria kuhusu utelezi kule kwa yule mwanadada [emoji848]
Nimeagiza zangu mindazi minne ya 150 150 na chai ya 200 pale, nikaanza kuibugia (wakuu, mi sina hela nyingi [emoji23][emoji23] mi mtanzania halisi na chembe chembe za uswazi, siku mkiskia eti nikapaki Range langu pale darajani, naomba replies za chai ziwe nyingi sana hadi nikimbie ID [emoji23])
Andazi la kwanza lilikuwa swadakta, yaliyofuata sasa ni matatizo, kama vile yananukia mafua! Moja kwa moja nikajisemea kimoyo moyo kuwa lazima tumbo liniume tu iwe isiwe, kwa hiyo nikaendelea kula huku nikiwaza box langu la frajil nimeliweka wapi?
Ghafla kitoto kinachotambaa kikatoka huko nje na mafua mengi yametapakaa uso mzima halafu michirizi (source) iliyokolea kutokea puani! Yule mwanamama alikuwa akisukuma nchapati [emoji16][emoji16] akamwita mwanae, akamsuuza lile fua na maji tiririka, halafu akasuuza mikono pasipo sabuni, akanitizama kama namwangalia, akajua simuoni, akaitupa mikono ndani ya kando la ngano ili kuchanganya mchanganyiko ule maridadi! Lilikuwa limebaki andazi moja nikaamua kuliacha pale, nikapita sokoni kununua ndimu 2 kwa ajili ya kukata kichefuchefu! Nimetembea barabara nzima kama mjamzito! Duh!
Wachache wenu jitahidini kuwa wasafi bhana!
Wengine hatuna uwezo wa ku attend hotel za wahudumu model wanaovaa sare na vi note books mkononi!
Kule chapati ya 400 ni Tsh 1300
Chai ya maziwa ya 500, kule 1500
Tuhurumiane wapishi!