Mama N'tilie kuweni wasafi, mnawaharibia wenzenu

Mama N'tilie kuweni wasafi, mnawaharibia wenzenu

Eewaaaa!
Kama hilo futo! Ndo maana nikasubiri usiku uingie ili nipeleke gheto! Assume ningepita nalo mchana kweupe, paparazi wangeninasa, hiyo picha ikaanza kutumiwa kutengenezea funny memes!
[emoji3][emoji3]
 
Eewaaaa!
Kama hilo futo! Ndo maana nikasubiri usiku uingie ili nipeleke gheto! Assume ningepita nalo mchana kweupe, paparazi wangeninasa, hiyo picha ikaanza kutumiwa kutengenezea funny memes!
[emoji3][emoji3]
Usikute huenda ni wewe na futo lako limekukalia baada ya kushindwa kulipa bill
 
Mimi niliacha kula migahawani baada ya kumkuta Mama wa mhagahawa anaoga bila sabuni nyuma ya mgahawa wake huku ikiwa ndani ya sufuria lile kubwa la wali alfajiri na mapema.

Kumbe yale maji ndio atapikia wali, mengine anachanganya kwenye mboga mboga,chai,n.k.
 
Mimi niliacha kula migahawani baada ya kumkuta Mama wa mhagahawa anaoga bila sabuni nyuma ya mgahawa wake huku ikiwa ndani ya sufuria lile kubwa la wali alfajiri na mapema.

Kumbe yale maji ndio atapikia wali, mengine anachanganya kwenye mboga mboga,chai,n.k.
Duh! Na hapo si ajabu ana imani za kishirikina na hicho anachofanya ni maelekezo kutoka kwa mtu, sababu katika hali ya kawaida hiyo haiji hata kidogo.
 
Nitangulize angalizo, sio wote wasiozingatia usafi, naamini ni 6% ndo wanawaharibia wenzao!

Ngoja niwape story. Nyakati za alfajiri nimemsindikiza bonge wangu kuelekea ubungo kwa wifi yake akae huko ili kesho kutwa aelekee Kibaha!

Wakati narejea nyumbani, muda ule nimeshuka kwenye daladala (wakuu mimi sina gari [emoji16]) nikaona bora nipate kifungua kinywa, maake kwangu gesi imekata! Nikaangaza chocho kwa chocho nikakutana na migahawa miwili imeungana, moja lina sister pic qal ndani na la pili lina mama mtu mzima, halafu juu ya kimeza chake kuna deli la maandazi [emoji39][emoji39]

Sijui ilikuwaje nikajikuta kwenye kimgahawa cha mwana mama kuyafuata yale maandazi pasi na kufikiria kuhusu utelezi kule kwa yule mwanadada [emoji848]

Nimeagiza zangu mindazi minne ya 150 150 na chai ya 200 pale, nikaanza kuibugia (wakuu, mi sina hela nyingi [emoji23][emoji23] mi mtanzania halisi na chembe chembe za uswazi, siku mkiskia eti nikapaki Range langu pale darajani, naomba replies za chai ziwe nyingi sana hadi nikimbie ID [emoji23])

Andazi la kwanza lilikuwa swadakta, yaliyofuata sasa ni matatizo, kama vile yananukia mafua! Moja kwa moja nikajisemea kimoyo moyo kuwa lazima tumbo liniume tu iwe isiwe, kwa hiyo nikaendelea kula huku nikiwaza box langu la frajil nimeliweka wapi?

Ghafla kitoto kinachotambaa kikatoka huko nje na mafua mengi yametapakaa uso mzima halafu michirizi (source) iliyokolea kutokea puani! Yule mwanamama alikuwa akisukuma nchapati [emoji16][emoji16] akamwita mwanae, akamsuuza lile fua na maji tiririka, halafu akasuuza mikono pasipo sabuni, akanitizama kama namwangalia, akajua simuoni, akaitupa mikono ndani ya kando la ngano ili kuchanganya mchanganyiko ule maridadi! Lilikuwa limebaki andazi moja nikaamua kuliacha pale, nikapita sokoni kununua ndimu 2 kwa ajili ya kukata kichefuchefu! Nimetembea barabara nzima kama mjamzito! Duh!

Wachache wenu jitahidini kuwa wasafi bhana!

Wengine hatuna uwezo wa ku attend hotel za wahudumu model wanaovaa sare na vi note books mkononi!

Kule chapati ya 400 ni Tsh 1300

Chai ya maziwa ya 500, kule 1500

Tuhurumiane wapishi!
Hapo shukuru tu hujadrive.
 
Duh! Na hapo si ajabu ana imani za kishirikina na hicho anachofanya ni maelekezo kutoka kwa mtu, sababu katika hali ya kawaida hiyo haiji hata kidogo.
[emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna mtoto wa mama vitumbua mmoja aliwahi nambia kuwa mama yake huwa anashikia chupi vitumbua wakati wa kuweka vitumbua kwenye deri!

Hapo mtu unajikuta unaonja ute ute wa mbususu bila kupenda!
 
Halafu wananiudhi wanaoweka chakula kwenye kontena za plastiki sivipendi.Isitoshe ukipita mgahawani muda wa mchana maji ya kuoshea vyombo machafu hata bata hanywi wala wao hawawezi kuoshea kwao tena wanatia sahani au kijiko wamekuletea chakula.Wito kwa watumishi wa afya wapite migahawani mchana.
Mwingine aliwahi nisuuzia kijiko alichotoka kulia mtu mwenye kikohozi kwa maji bila sabuni! tena bila kukipikicha kwa vidole!
 
Kama wauza chips tu
Asilimia kubwa ya mama lishe maji wanayooshea vyombo tangu asubuhi hadi usiku ni hayohayo na muda mwingine huongezeka wingi bila kujua yanatoka wapi, anaweza kuanza na lita 15 asubuhi ifikapo usiku ni lita 18
 
Mwingine hapa kainamia jungu la supu jikoni wakati anasumbuliwa na mafua tiririka!

Ngoja niagize chai na chapati tatu tu!
 
Back
Top Bottom