KERO Mama Ntilie wanahatarisha afya zetu kwa kutumia vifungashio visivyo salama

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mmoja wa wadau wa JamiiForums, kuna kitu nataka nishauri au kukemea kabisa. Kuna vitu hawa Mama Lishe au Mama Ntilie wanafanya siyo kabisa kwa afya ya Wateja wao kupitia vitafunwa wanavyoouza.

Nimeona hali hiyo maeneo tofauti Nchini, ni kama vile ni watu ambao wote wana staili ileile.

Unakuta Mama Ntilie ana vifungashio vya magazeti yaliyotumika, ukiangalia hilo gazeti limepita kwa watu wengi sana, hatuwezi kujua huyo aliyelisoma mikono yake alikuwa amenawa au la hakuta mtu ana vimelea vya magojwa mkononi na anashika hilo gazeti halafu Mama Ntilie anakuja kuchukua kwa vifungashio vya vitafunwa.

Anayeathirika ni mlaji wa mwisho (mteja) ndio maana magojwa ya tumbo n.k hayaishi.

Inakera kweli kweli

Naomba kuwasilisha
 
Hiyo TISA kumi kwenye kuhifadhi vyakula ambapo wanatumia makaratasi ya NAILONI kuhifadhi wanasema ni kichocheo cha KANSA kwa kwenda mbele. Hawa maofisa Afya inabidi wawaelimishe jamani
 
Hii nchi hakuna serikali.

Mama Ntilie wanapika kisha wanafunikia Manailoni ila serikali haifanyi operesheni ya kutembelea mama Ntilie na kuwazuia outright. Ndiyo maana KANSA imekuwa nyingi sana nchini
 
Biashara ya magazeti ya kufungashia vitu ni magazeti yasiyosomwa yaliyokosa wateja.

Yakishapitwa na wakati bila kununuliwa ndiyo huuzwa kwa kupimwa.

Siyo magazeti galiyokusanywa toka majumbani mwa watu, hapana.

Hata hivyo siungi mkono vitafunwa ama vyakula vingine vilovyotayarishwa kwa kuliwa kufungashiwa kwenye magazeti.
 
Hawajali Kwa kuwa Wana elimu ndogo sana waliyopatiwa na majizi ya ccm, wengine hata kusoma hawajui unamwambia habari za afya na vimelea? Ccm ni janga Kuu!
 
Muhimu ni kutembea na kifungashio chako ili kuepuka hiyo kadhia
 
Usisahau yale maandishi kwenye magazeti ni kemikali. Halafu unajua mchakato wa kutengeneza hayo makaratasi ya magazeti? Kemikali inahusika kotekote.

NB: Katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu mwakani, hawa mamantilie tumekubaliana waitwe maafisa lishe!
 
Unakula kwa mama ntilie hadi karne hii?
 
Hapo umeangalia kigezo kimoja tu cha kifungashio lakini kuna mengi ya kutisha zaidi
Mafuta yaliyotumika
Mazingira yaliyotumika kuandaa Hicho kitafunwa
Vyombo vilivyotumika
Mikono inayokuhudumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…