Elections 2010 Mama Salma ataka makundi yavunjwe

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
11,662
Reaction score
6,888
Hivi huyu Salma au Salima anahusika vipi kwenye kupiga kampeni? Je, ni kiongozi wa UWT? Je, gharama anazotumia zinatakiwa kujumuishwa kwenye zile za mgombea urais wa CCM? Hivi ni kwa nini anaonekana kukamia mumewe ashinde tena urais hata kuwataka UWT wapige kampeni za shuka kwa shuka? Hivi ana uchungu kweli na watanzania wote au yeye na wanawe tu?

Source: Habarileo (1/9/10)
 
Anataka kuwa kama Lucy Kibaki.
Ndo anapoelekea huko.
 

Hivi angekuwa mumeo au mkeo anagombea usingempa ushirikiano? Kwani yeye afurahi kuwa Ikulu au kutambuliwa kama FIRST LADY? Tusiwe tunauliza maswali yenye majibu tayari!!!
 
aghaaaaaaaa huu ndio uongozi wa CCM chini ya uongozi wa JK bwana, Salima ana power kuliko unavyoweza fikiri, msafara wake huko kwenye kampeni ni noma, kweli hela zetu ( walala hoi) zinateketea.Pipooooooooooos Pawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Si vibaya kwa mke wa Rais kumsaidia mumewe kupiga kampeni. Hii inafanywa kila mahali. Hata wabunge huwa wanashirikiana na wake/waume zao katika kampeni.

Sababu za kushiriki kwao zinatokana na utashi wao binafsi. Vile vile kampeni hutumia rasilimali nyingi za familia ikiwemo muda spouse anaotumia kufanikisha azma yake ya kisiasa na pesa ambazo zingeweza kutumika kwa familia endapo mgombea asingeamua kugombea nafasi anayoomba.

Hivyo, sioni ubaya wa Mama Kikwete kushirikiana na mumewe katika kampeni, kama ambavyo haikuwa vibaya kwa kijana wa Kikwete (Ridhwani) kusaidia kutafuta wadhamini.

Kama angekuwa anamsaidia katika majukumu yake kama Rais, ningemshangaa sana, kwani hahusiki kikatiba wala kisheria kufanya hivyo. Vile vile, ushiriki wake ungekuwa na madhara (+/-) kwa uongozi wa nchi.
 
familia ya kikwete naonna wanafungu lao ndani ya ccm mama salma endelea kunenepa na kuwanyonya wan awake wenzio ila kiyama kitafika
 
Umemsahau kaka "riziwani" mbona naye yuko kwenye mizunguko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…