Mama Salma Kikwete afunguka maisha yake ya uraiani

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506


Mke wa rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete amevitaja vitu anavyovipenda kufanya akiwa nyumbani.

Akifanya mahojiano na waandishi wa habari wa Clouds Media waliomtembelea nyumbani kwake kuelekea siku ya mama duniani, siku ya Jumapili, Mei 8, amesema, “Mimi ni mama wa watoto tisa, kulea watoto tisa haikuwa shughuli ndogo lakini nashukuru Mungu kwa baraka ya kuwapata watoto wangu. Watoto wangu wamekuwa wakisaidiana sana wakati wa kuleana na kushirikiana katika kila jambo. Ukiacha hao tisa nina watoto wengine ninaowasomesha nina watoto wengi sana, nawapenda sana wanangu naamini hata wao wananipenda pia.”

Aidha Mama Salma aliongeza, “ninapoona wanangu wanaandikwa vibaya kwenye magazeti, nachukizwa na jambo hilo kama mzazi, lakini natambua haya yanatokana na maisha tuliyoyachagua – maisha ya siasa, na hivyo ndio siasa ilivyo na la kufanya kama mzazi ni kumpa ushauri mzuri mwanangu katika kudili na jambo hilo.”

Mama Salma aliendelea kwa kusema kuwa anapenda kupika hata akienda jikoni hakuna atakayemuuliza kwanini ameenda huko kwa sababu anaenda kuwapikia watoto na mumewe.

Akijibu swali alilouliza Feza Kessy kuhusu anatumia jina gani wakati anamuita rais mstaafu Jakaya Kikwete, Mama Salma alijibu, “Huwa namuita mume wangu.”

Hata hivyo Mama Salma amezitaja kazi nyingine ambazo anazipenda kuzifanya akiwa nyumbani kuwa ni pamoja na kuandika kila kila kitu kinachotokea na kukaa na watoto na kuwafundisha na kuwaelezea vitu muhimu.


Chanzo: Bongo 5
 
Hii familia ina amani sana kwa kweli baada ya Lowasa kukosa Urais
Ni kweli kabisa kwasababu angekuwa Rais angetumbua majipu yaliyoiva huko na mpaka sasahivi hayatumbuliwi.
 
Sijasoma post yako but let me make a comment! Kufunguka nini ameishi miaka over 50 uraian leo miaka kumi amesahau uraiani. Waafrika shidaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Mkuu kwani Lowassa alikuwa na nini na hiyo familia??

Vipi ule msemo wa bora nusu shari(Magufuli) kuliko shari kamili(Lowassa) uko applicable hapa??
Baba wa hiyo familia alimchinjia baharini Lowasa alafu ukizingatia 2005 alitumia ela zake nyingi sana kwa ajili yake awe Rais.
 
Kumbe huyu mama kazaa watoto tisa??

Mbona bado anaonekana "mbichi"......??
Wamama wa zamani achana nao ila sie wa chips kuku baga pizza mmoja tu chaliii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…