Mtaka Haki
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 492
- 149
HAWA WANAWAKE WA MBEYA WAMEVUNJA REKODI KWA KUWA MNO WAWAZI. HUKO MOSHI HUWA WANAMSHANGILIA LAKINI AKISHAONDOKA WANAMSENGENYA NA KUMCHARURA KISHA WANAAAPA KUTOKIPIGIA KURA CHAMA CHAKE.
HAPA WANAMUONYESHA WAZI KUWA WAO NI CHADEMA? NAOMBA WANAWAKE MSIENDELEE KUMTESA MAMA YETU. ACHENI APITE KWA AMANI KUOMBA KURA.
JAPO MNALALAMIKA ANAOMBA ZA FAMILIA. SITAKI MUMTESE MKE WA RAIS HATA KAMA ANAMALIZA MUDA WAKE MPUNGIENI TAFADHALI.
NA THOBIAS MWANAKATWE
21st October 2010
B-pepe
Chapa
Maoni
Mke wa Rais , Salma Kikwete
Mke wa Rais , Salma Kikwete, ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya baadhi ya wanawake wa vijiji vya wilaya ya mpya ya Momba mkoani hapa ukiwemo Mji wa Tunduma kumuonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati akiwa njiani akitokea kwenye ziara mkoani Rukwa.
Akizungumza jana na wanawake wa Jiji la Mbeya wakati akiwa njiani akitokea Sumbawanga, alisema aliona kundi la wanawake ambapo alipojaribu kuwasalimia kwa kuwaonyeshea mkono juu, lakini nao walijibu kwa kumnyooshea alama ya vidole viwili ambayo inatumiwa na Chadema katika salamu zao.
Nimeshangaa kuona katika mkoa wa Mbeya, sijawahi kuona katika mkoa mwingine nilivyofika karibu na Tunduma wanawake wananionyeshea vidole viwili, wakati maeneo mengine kila ninapopita wananishangilia sana, alisema.
Hata hivyo, baadhi ya wanawake walimfariji na kumhakikishia kuwa watake wasitake lazima CCM itashinda kwa kishindo.
Mama Kikwete alisema wanawake waonyeshe msimamo kwa kukipigania Chama cha Mapinduzi (CCM).
Wanawake wanafahamika ni watu wenye msimamo, huwezi kukuta mwanamke anahama CCM na kuhamia vyama vya upinzani na hata kama wapo ni wachache sana, lakini wanaume wao ni kawaida yao kila kukicha ni kubadilisha vyama,alisema Mama Salma Kikwete.
Alisema wanawake ambao kura hazikutosha wakati wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM hawana sababu ya kuendelea kukaa na kinyongo na badala yake wawape ushirikiano walioshinda kuhakikisha CCM inapata ushindi.
Aliongeza kuwa wanawake wana kila sababu ya kujivunia na kutembea kifua mbele kutokana na mafanikio yaliyopatikana chini ya serikali ya CCM ikiwa ni pamoja na wanawake wenyewe kuinuliwa katika ngazi za maamuzi.
Alisema wanawake wana kila sababu ya kujivunia maendeleo ya wanawake kama ilivyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro ambaye ni mfano mzuri wa kuigwa na wanawake wa Tanzania.
CHANZO: NIPASHE