Mama Salma Kikwete anusurika kupata ajali mkoani Mara

Mama Salma Kikwete anusurika kupata ajali mkoani Mara

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Posts
5,551
Reaction score
2,153
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete leo amenusurika kupata ajali baada ya Lori linalodaiwa kuwa na magendo kukaidi amri ya polisi kusimama kupisha msafara huo... Gari la usalama lililazimika kulikinga gari la Mama Salma Kikwete... Hali iliyolazimisha Gari la alilipanda Mama Salma kutoka nje ya Barabara... Ajali hiyo ilisababisha baadhi ya magari yaliyokuwa katika msafara huo kutoka nje ya barabara kuepuka ajali... SOURCE: Radio One (Taarifa ya habari ya saa 7)
 
Hiyo biashara ya kupisha misafara ya viongozi au wake zao inatupotezea muda jamani!!! Inaudhi!
 
Pole FL1 sorry ai mii FL.
Nashauri akachekiwe presha...
 
Pole Mama Salma, mungu atakulinda na majanga yote.

"Ila cha kujifunza hapa ni kwamba maisha ya binadamu yoyote yule ni muhimu kuyalinda bila kujali nafasi yake kwani hilo ni Jukumu mama la serikali yoyote kuhakikisha usalama wa Raia wake, Matukio kama haya yapo mengi sana kila siku nchi nzima, daladala kuchomekeana wao kwa wao pamoja kuchomekea magari mengine, barabara mbovu, madereva wanapata leseni kwa rushwa badala ya qualifications" - Umefika wakati sasa kuwalinda Raia wote na ajali zinazoweza kuzuilika, Nina hakika kama vyombo vya habari vingekuwa vinatangaza matukio yote ya aina hii ya msafara wa FL basi 24hour hazitoshi. Law enforcement agents waache longolongo na Rushwa wafanye Kazi yao"
 
namuonea huruma huyo dereva na wote walioko kwenye lorry lililobeba magendo. Yaani anataka kugonga FL
 
Nadhani, hii ni hatari sana. Dereva anayehusika akamatwe na awekwe ndani na sheria ichukuwe mkondo wake na umma tujulishwe kitu gani kimetokea!!! That is not fair at all!!
 
Hivi na nchi zilizoendelea wake wa viongozi wanasafiri kwa utitiri wa msururu kama hapa kwetu?
Pole mama ridhiwani kwa maswahibu yaliyokupata.
 
Pole mama rais alikuwa taarime?Taarime kwa magendo mpaka wanataka kumgonga mke wa mkulu.Na Jukwaaa lililo tengenezwa kwa ajiri ya kuhutubia hawa wababe wa taarime wamelivunja...habari ambazo sio rasmi walikuwa wanataka ahutubie...wamzomee...lakini hao askari walivyo wengi naona na ubabe wao wameogopa..Kipigo.
 
Hiyo biashara ya kupisha misafara ya viongozi au wake zao inatupotezea muda jamani!!! Inaudhi!

Ndugu umezungumza jambo jema. Hivi utaratibu wa kupishana ili mke wa Raisi apite una mantiki gani? Maana kwa Raisi au WAziri mkuu angalau tunaweza sema wanawahi katika shughuli za kitaifa (though its not always the fact). Sasa huyu mke wa Raisi nae anapishwa, tena huko MAra ambapo hata foleni sidhani kama ipo. I think hili jambo tuliangalie kwa umakini. maana waka mama zetu wanajifungulia njia kutokana na foleni ndeefu, na barabara mbovu, ati mke wa Raisi anapishwa kwa shughuli za Taasisi yake binafsi. Kesho mtasema watoto wa raisi wakiwa wanatoka shule, mke wa Ridhi, na mchumba wake naniii wote wapishwe.
 
inaweza ikasaidia kupunguza misafara ya hawa watu, ila pole yake
 
Pole Mama Salma Kikwete.

Ninamshukuru Mungu katika Jina la Yesu kwa kukunusuru.

Mungu aendelee kukulina na akuongezee Umri mtimilifu wa kuishi hapa Duniani. Amen
 
Hiyo biashara ya kupisha misafara ya viongozi au wake zao inatupotezea muda jamani!!! Inaudhi!

Imagine kwa Zuma...five of them...inabidi siku nzima ukae kwenye foleni...luckily ni south africa miundombinu si haba
 
Back
Top Bottom