Mama Salma Kikwete atesa na ndege ya Rais, JK aikwepa...

Mama Salma Kikwete atesa na ndege ya Rais, JK aikwepa...

Kulikoni said:
Mlalahoi,

My post was very clear, sikustate kuwa si kosa, I asked whether ni kosa or not. I still doubt kuwa eti ndege ya rais ni ya rais tuuu. Nasema hivi kwa sababu nnafahamu kuwa ni mwezi uliopita tu ilikuja delegation ya wataalamu wa Aviation wa UN, walipatiwa moja ya ndege za rais wakaenda nayo Zanzibar na Arusha (although nao pia hawawezi kukaimu urais JK akiwa na dharura).

My post was meant to highlight the exaggerations made by mwandishi... kuiita eti safari binafsi, kashfa nzitooo etc. My stand was also very clear: hata kama sheria inamruhusu, ingekuwa ni busara na more economical kutolitumia jidege hilo.

Delegation ya UN ilikuja kwa shughuli za kitaifa,sio kifamilia.Kuhusu kuakimu Urais,nilikuwa najaribu kukuonyesha kuwa kuwa mke wa Rais haimaanishi kuwa mshirika wa utawala.Kuna watu wenye mamlaka hiyo including VP,Spika and Chief Justice.

Kosa la mwandishi ni lipi kwa kuiita safari hiyo ni binafsi?
 
Mugishagwe said:
tafiti fafanua post yako maana ni ngumu kueleweka sasa .
Kashindwa kusema Mama Salma anaonewa.Ushamsikia huyo akiponda matumizi mabaya ya serikali?Hayo mambo ya kina Dr Gharib Bilal na ndege ya serikali sijui wapi na wapi!!!Na sijui kosa la Mbowe kumiliki Tanzania Daima ni lipi.Nadhani Tafiti Then Jadili angependa tubakiwe na magazeti manne tu:Uhuru na Daily News,na weekend kuwe na Mzalendo na Sunday News.

Ni mpuuzi pekee anaeweza kuafikiana na upumbavu wa Mkapa kwamba waliokuwa wanapinga ununuzi wa ndege walikuwa na wivu.May be Claire Short nae alikuwa na wivu alipokuwa anajaribu kuweka pingamizi kwenye ununuzi wa ndege hiyo, haiyumkiniki kwa masikini wa kutupwa kama sie ambao tuna priorities nyingine luluki kukimbilia kununua vitu vya kifahari huku wananchi wakiwa hohe hahe.Blair anatumia helikopta na ndege za Royal Marines na sometimes anatumia BA,sie watu wa matanuzi tunajifanya tunazo huku tunategemea wafadhili.

http://www.telegraph.co.uk/news/graphics/2006/08/03/nblair03.jpg
 
Kwanza tusahihishaneni.. ndege hiyo si ya Rais! Hiyo ni ndege ya Serikali inayotumiwa kusafirisha viongozi. Tatizo tulilonalo hadi sasa ni kuwa hatujui ni viongozi gani kwa mujibu wa sheria/taratibu wanatakiwa kusafiri na ndege hiyo kipaumbele kikiwa ni mfuatano wa viongozi wakuu (Rais, Makamu, Waziri Mkuu/Rais wa Zanzibar???, Spika..n.k) Sasa Mke wa Rais anakuwa wapi hapo?

Pili, kama hoja ni kuwa mtu yeyote mwenye fedha anawezak kukodi ndege hiyo kwa safari binafsi, tunaomba tuambiwe (It could come and pick me up...). Kama sivyo, ni nani alilipia safari hiyo kwa fedha zipi? Tatizo siyo mama Salma kutumia ndege hiyo.. tatizo.. ametumia kama nani, mwa fedha za nani, kwa utaratibu upi?
 
exactly Mwanakijiji......upo mwongozo wa huduma ambazo ni stahiki ya Raisi, Mkewe, na watoto wake. Naamini ni halali kwa Mama Kikwete kusafiri ni ndege ya serikali, ikiwa atakuwa anafanya shughuli za serikali.
 
Wazee hebu mtu mmoja aende utumishi, kuna kitabu cha sheria za serikali juuu ya mambo yote ya viongozi na hizi issue, ili tukate mzizi wa fitina,

Je sheria yetu ya serikali inamruhusu mke wa rais kusafiri na ndege iliyonunuliwa na serikali yetu ya jamhuri, kwa ajili ya matumizi ya rais, ambaye ni mumewe?

Je mke wa rais akiumwa na kuzidiwa, au watoto wake, hawataruhusiwa kupelekwa haraka nje hospitalini? Je vipi wakifa kwa sababu wananchi hatutaki watumie ndege tuliyomnunulia baba yao na mume wa first lady?

Kwenye hili nina wasi wasi, ingawa sina uhakika kuwa ni RUKHSA! Lakini mtu mmoja aweke sheria hapa inasema nini? Ipooooooo!
 
Mzee Mwanakijiji said:
Kwanza tusahihishaneni.. ndege hiyo si ya Rais! Hiyo ni ndege ya Serikali inayotumiwa kusafirisha viongozi. Tatizo tulilonalo hadi sasa ni kuwa hatujui ni viongozi gani kwa mujibu wa sheria/taratibu wanatakiwa kusafiri na ndege hiyo kipaumbele kikiwa ni mfuatano wa viongozi wakuu (Rais, Makamu, Waziri Mkuu/Rais wa Zanzibar???, Spika..n.k) Sasa Mke wa Rais anakuwa wapi hapo?

Pili, kama hoja ni kuwa mtu yeyote mwenye fedha anawezak kukodi ndege hiyo kwa safari binafsi, tunaomba tuambiwe (It could come and pick me up...). Kama sivyo, ni nani alilipia safari hiyo kwa fedha zipi? Tatizo siyo mama Salma kutumia ndege hiyo.. tatizo.. ametumia kama nani, mwa fedha za nani, kwa utaratibu upi?

Hivi Mwanakijiji,Air Force One ni US Presidential jet au US Government flight?Nadhani hapo ni suala la semantics tu.Kwa kuiiita "ndege ya Rais" haimaanishi imenunuliwa kwa hela yake bali primarily kwa matumizi yake.Nadhani hata JK anaposema "serikali yangu" hamaanishi kwamba ni mithili ya familia yake bali serikali anayoiongoza.Just like Jose Mourinho anaposema Chelsea ni "timu yake" ilhali owner wa timu hiyo ni Abramovich.

Maneno yafuatayo yalisemwa kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mheshimiwa Aloyce Kimaro (CCM-Vunjo).

"Mheshimiwa Spika, lingine nichangie kwenye usafiri. Hapa tulikua tunazungumzia suala la ndege ya Rais. Ndege ya Rais ilishanunuliwa kila leo ndege ya Rais hivi mnataka Rais wa Ari Mpya apande ndege gani? Naomba huu mjadala uishe tuende na Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya. Hii intake mpya ni ya mambo ya kisasa hata hili Bunge ni la kisasa, mwishowe mtasema hata hili Bunge tuliache turudi kuwe kwa zamani naomba wenye mawazo hayo yaishe twende mbele badala ya kurudi nyuma twende mbele kwa Kasi Mpya".

Kama unavyoona hapo,anataja "ndege ya Rais," lugha yetu ya Taifa ndani ya Bunge letu.
 
Mlalahoi, Ndege yoyote anayopanda Rais wa Marekani inakuwa "Air Force One"! Ila kuna ndege maalum yenye jina hilo ambayo ni kwa matumizi ya Rais na Makamu wake! Ndege hiyo haibebi mtu mwingine yoyote kama Rais hayumo, unless kama Rais mwenyewe ataidhinisha au itaamuliwa na mamlaka husika vinginevyo!
 
wewe mzee usituletee hapa. Airforce one ni kitengo maalum cha ndege za rais. sasa zipo mbili boengi 747 - 200B.
 
Peter, sijui nimekuletea nini hapo.. Rais Bush akipanda American Airlines hiyo ndege sekunde hiyo hiyo inaitwa "Air Force One"...!
 
Mzee Mwanakijiji said:
Peter, sijui nimekuletea nini hapo.. Rais Bush akipanda American Airlines hiyo ndege sekunde hiyo hiyo inaitwa "Air Force One"...!

YES, sawa kabisa

As soon as the president steps aboard an Air Force plane, that plane is referred to as Air Force One by the crew and all air traffic controllers.In order to avoid confusion with any other planes in the area. If the president rides on an Army aircraft, that aircraft is Army One, and whenever he boards his specialized helicopter, that craft is Marine One. Civilians generally refer to the physical plane itself as Air Force One
 
Wanasema nini kuhusu Air force one:-

Air Force One is a presidential airplane. Boeing 747-200B that has been modified to meet presidential requirements. The aircraft is known by the radio call sign used when the president is aboard: Air Force One.

Airforce one historically, several U.S. presidents have flown on Boeing aircraft.
In 1943, President Franklin D. Roosevelt flew to Casablanca aboard a Boeing model 314 Clipper.
In 1962, Boeing introduced U.S. presidents to modern jet transportation with the introduction of the Boeing model 707-320B. In all, seven presidents were served by the 707-320B.
Today, the chief executive flies aboard a specially configured 747-200B, the newest and largest presidential airplane.
Its capabilities include:-
Longer range for presidential travel Aerial refueling Self-sufficiency at airports around the world
The "flying Oval Office" has 4,000 square feet of interior floor space. Among its accommodations are:-
Conference/dining room
Quarters for the president and the first lady
An office area for senior staff members
Another office that converts into a medical facility when necessary
Work and rest areas for the presidential staff, media representatives and Air Force crews Two galleys that can provide 100 meals at one sitting
Multi-frequency radios for air-to-air, air-to-ground and satellite communications Principal differences between Air Force One and the standard Boeing 747 include state-of-the-art navigation, electronic and communications equipment; its interior configuration and furnishings; self-contained baggage loader; and front and aft air-stairs.

Sio ndege zote zenye uwezo huo bwana. Bush hapandi ndege yeyote ile! kuna kitengo cha airforce one White house na ukarabati hufanywa na kitengo hicho.
 
Airforce One or Hundred,pointi yangu kwa Mzee Mwanakijiji ni ufafanuzi wake kwamba Gulfstream Jet alopanda Mama Salma si "ndege ya rais" bali ndege ya serikali.Nadhani ni semantics tu...As to whether Bush anapopanda Precision Air inageuka kuwa Airforce One,hilo sina ujuzi wala interest nalo.Nakubaliana na Mzee Mwanakijiji kuwa ndege hiyo ni ya serikali lakini hakuna dhambi kuiita ndege ya rais hasa kwa vile imekuwa ikiitwa hivyo kwa mujibu wa lugha yetu ya Taifa,na pia Rais ndio kiongozi mkuu wa serikali na nchi inayomiliki ndege hiyo.JK akisema Tanzania ni nchi yake hawezi kumuudhi yeyote bcoz anamaanisha yeye ni kiongozi wa nchi hiyo and not the owner.

Air Force One
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jump to: navigation, search

For other uses, see Air Force One (disambiguation).

Air Force One
Air Force One flying over Mount Rushmore.
Air Force One flying over Mount Rushmore.
Name Air Force One
Primary function Presidential air transport
Contractor Boeing
Power plant Four General Electric CF6-80C2B1 Turbofans
Thrust 56,700 lbf (250 kN) per engine
Length 231 ft, 10 in (70.7 m)
Height 63 ft, 5 in (19.3 m)
Wingspan 195 ft, 8 in (59.6 m)
Speed (estimated) 630 mph (Mach 0.92)
Ceiling (estimated) 45,100 ft (13,700 m)
Maximum Takeoff Weight (estimated) 833,000 lb (375,000 kg)
Range 7,800 statute miles (6,800 nautical miles or 12 550 km) Note: it can be fueled in-flight so it has an essentially limitless range.
Crew 26
Total capacity 102
Introduction August 23, 1990 (No. 28000)
December 23, 1990 (No. 29000)
Deployment September 6, 1990 (No. 28000)
March 26, 1991 (No. 29000)
Inventory 2

Air Force One is the air traffic control call sign of any U.S. Air Force aircraft carrying the President of the United States. Since 1990, the presidential fleet has consisted of two specifically configured, highly customized Boeing 747-200B series aircraft—tail numbers 28000 and 29000—with Air Force designation VC-25A. While these planes are referred to as "Air Force One" only while the president is on board, the term is commonly used to describe either of the two aircraft normally used and maintained by the U.S. Air Force solely for the president. The reason they have two planes is that they take off together (the second one takes off about a half-hour after the first one) so people don't know which one the President is on. One is a decoy for possible attackers.

The VC-25A is capable of flying 12 600 km (7,800 miles)—roughly one-third the distance around the world—without refueling and can accommodate more than 70 passengers. Before these planes entered service, two Boeing 707-320B-type aircraft—tail numbers 26000 and 27000—had operated as Air Force One starting in 1962. The Air Force designation for these aircraft was VC-137. Since its inception, Air Force One has become a symbol of presidential power and prestige. Each Air Force One costs approximately 325 million dollars.
 
Mlalahoi said:
Delegation ya UN ilikuja kwa shughuli za kitaifa,sio kifamilia.Kuhusu kuakimu Urais,nilikuwa najaribu kukuonyesha kuwa kuwa mke wa Rais haimaanishi kuwa mshirika wa utawala.Kuna watu wenye mamlaka hiyo including VP,Spika and Chief Justice.

Kosa la mwandishi ni lipi kwa kuiita safari hiyo ni binafsi?

Ninavyoelewa mimi ni kuwa u-first lady nao pia ni wadhifa flani, ingawa si kama u-VP, u-spika n.k. If I am not mistaken, nae pia ana mabody guard hata akiwa hayuko na rais. Ikiwa hii safari ya Swazi alialikwa na kwenda in her capacity as first lady, sioni ni kwa vipi safari hiyo inakuwa ni safari binafsi.

Whether anaruhusiwa kutumia our 'air force one' au tunakubaliana na maudhui ya hiyo safari, that's another issue. Safari hii, to me, haikuwa binafsi. Na hapo ndipo nnapoona mwandishi katia chumvi.

My opinion.
 
Mlalahoi said:
....

Air Force One is the air traffic control call sign of any U.S. Air Force aircraft carrying the President of the United States. Since 1990, the presidential fleet has consisted of two specifically configured, highly customized Boeing 747-200B series aircraft—tail numbers 28000 and 29000—with Air Force designation VC-25A. While these planes are referred to as "Air Force One" only while the president is on board, the term is commonly used to describe either of the two aircraft normally used and maintained by the U.S. Air Force solely for the president. The reason they have two planes is that they take off together (the second one takes off about a half-hour after the first one) so people don't know which one the President is on. One is a decoy for possible attackers.

Peter, unachosema ni sawa na ninachosema hakina uongo!!! mine is the technical part of it..!
 
Kulikoni said:
Ninavyoelewa mimi ni kuwa u-first lady nao pia ni wadhifa flani, ingawa si kama u-VP, u-spika n.k. If I am not mistaken, nae pia ana mabody guard hata akiwa hayuko na rais. Ikiwa hii safari ya Swazi alialikwa na kwenda in her capacity as first lady, sioni ni kwa vipi safari hiyo inakuwa ni safari binafsi.

Whether anaruhusiwa kutumia our 'air force one' au tunakubaliana na maudhui ya hiyo safari, that's another issue. Safari hii, to me, haikuwa binafsi. Na hapo ndipo nnapoona mwandishi katia chumvi.

My opinion.

Nadhani u-"first lady" ungekuwa wadhifa basi Katiba ya Jamhuri ya Muungano ingetuambia kuhusu uteuzi,haki na wajibu wake kikatiba.Angalia kwenye wikipedia wameelezea kwa kirefu kuhusu "term" (not title) hiyo.Labda unataka kusema kuwa "mke" ni wadhifa.Kuhusu kuwa na bodyguards hata wewe ukiwa na nafasi ambayo unadhani inaweza kutishia usalama wako na una uwezo wa kifedha unaweza kukodi bodyguards.Mke wa rais anapatiwa bodyguards kama sehemu ya privileges wanazopatiwa baadhi ya members wa familia ya kiongozi wa nchi.Na ukibahatika kuongea na wajuvi wa mambo ya usalama watakwambia kuwa walinzi wa mke wa rais ni sehemu ya detail ya protection ya president.

Kuna tofauti kubwa kati ya hadhi/heshima anayopatiwa mtu na wadhifa wake.
 
Ahsante kwa maelezo na reference.

Nnachojiuliza tu ni kuwa, first lady anapoalikwa na mkuu wa nchi nyingine katika shughuli yao ya kitaifa, solely kutokana na 'hadhi/heshima' yake hii ya u-first lady, kiutaratibu gharama za safari (hata kama ni kwa commercial airline) anatakiwa alipe nani? zitoke kipochini mwake au serikalini?

In other words, as a general question, shughuli za ki-first lady zinagharamiwa na nani?

Naomba kufahamishwa na wanaofahamu.
 
Kuwa First lady vilevile kuendane na hali ya nchi. Kulikuwa hakuna umuhimu wa huyu mama kuchoma pesa za walala hoi eti sababu anakwenda kwenye sherehe hata kama alialikwa kwa kofia ya First lady. Hizo sherehe alizokuwa anapelekwa kwa gharama ya watanzania zimeisaidia nini Tanzania na watanzania?. Hii ndege kwanini tusiiuze na pesa yake tukashughulikia suala la umeme?. Kama USA First lady anaweza kupanda ndege ya kawaida, mama yetu Salma anashindwa nini?. Hata mwaka bado ina maana kisha sahau kwamba alikuwa anapanda Hiace (Vipanya) toka Dar kwenda Bagamoyo?
 
hivi kwanini tumuandame huyu mama? mama kikwete hawezi kuondoka nchini bila JK kuwa na taarifa, pamoja na usafiri atakaotumia. JK anapaswa kubeba lawama za matumizi mabaya ya fedha ya walipa kodi.

kuna tetesi kwamba wako wana mtandao wanaompiga vita huyu mama. mbinu za wana mtandao zinaeleweka, na mojawapo ni hiyo ya kuwabambikiza watu wengine lawama anazopaswa kubeba JK.
 
jokakuu kwa maneno mengine una maana kwamba sisi tunao debate hii issue dhidi ua huyu Mama sisi ndiyo wana mtandao ama mimi sijakuelewa ? Kwanza tunatafiti kujua kwa nini huyu mama atumie dege lote yeye mtu mmoja kwa gharama zetu . Majibu yakisha kuwa wazi then wenye akili watajua kwamba JK si mzalendo kwa Nchi ya kutumia mapesa mengi namna hiyo kwa ziara ambazo mimi nasema ni za krafiki huko aliko enda .Sijui kama ilitangazwa na sijui kuona mambo yale ya Mswati sisi wa TZ tumepata faida gani.Haya ni mambo ambayo yanonyesha jinsi JK anavyo tumia vibaya pesa yetu hata kama leo tunamsema mkewe lakini Nchi tumempa yeye na si mkewe .

Sisi si wana mtandao ila sisi ni wazawa na wazalendo bwana jokakuu .
 
Gharama za FIRST LADY niliwahi kusoma katika RAI wakati ule wa mama Mkapa kulaumiwa kwa kuspend over 65 milioni shilingi kwa kwenda katika mkutano wa wake wa marais wa afrika nchini Nigeria ni kuwa zinafall under category ya matumizi ya IKULU.

Nakumbuka bwana Kabourouh aliwahi sana kulipigia kelele hili alipokuwa bungeni kuwa matumizi kama haya yaa-ainishwe vizuri ili kuepuka matumizi mabaya kwani haifai kuweka matumizi makubwa namna hii kwa heading tu matumizi IKULU.

Ikulu haikutoa maelezo yeyote kuhusu hilo sasa hivi sina hakika matumizi hayo yanawekewa chini ya bajeti gani...
 
Back
Top Bottom