Mama Salma Kikwete awataka wakazi wa Mkoa wa Lindi kuipigia kura ya ndiyo katiba pendekezwa

Ta Muganyizi

R I P
Joined
Oct 19, 2010
Posts
5,355
Reaction score
2,736
MAMA KIKWETE AWATAKA WAKAZI WA MKOA WA LINDI KUIPIGIA KURA YA NDIYO KATIBA PENDEKEZWA
salma-pps%2B(1).jpg
Mama Salma Kikwete
Na Anna Nkinda – aliyekuwa Lindi

Wananchi wa mkoa wa Lindi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuipigia kura ya ndiyo katiba inayopendekezwa kwani ni bora na imegusa maeneo yote kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.

Rai hiyo imetolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wananchi waliohudhuria sherehe ya kushangilia ushindi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa katika mtaa wa Ruaha kata ya Mingoyo wilayani humo.

Katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana wananchi wa mtaa wa Ruaha waliwachagua Mwenyekiti na wajumbe wote watano kutoka Chama Cha Mapinduzi.

Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema katiba inayopendekezwa imeangalia maeneo yote yanayomgusa binadamu ikiwa ni pamoja na haki za wanawake na watoto, watu wenye mahitaji maalum wakiwemo walemavu na wazee.

"Katiba iliyopo sasa ilitungwa na baadhi ya watu waliokuwa madarakani kwa wakati ule na haikuwahusisha wananchi, lakini hii inayopendekezwa wananchi wameshiriki kuitunga kwa kutoa maoni yao", alisema Mama Kikwete.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mwantumu Mahiza aliwahimiza wananchi hao kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili wasipoteze haki yao ya msingi ya kupiga kura.

Mahiza alisema kama kuna watu waliojiandikisha katika miaka ya nyuma wabebe vitambulisho vyao ili viweze kunukuliwa na kwa wale wenye umri wa kuanzia miaka 18 wakajiandikishe na walio na umri wa chini ya hapo wasijiandikishe.

Aliwaasa wananchi hao kutokubali wageni waliokaa katika maeneo yao kwa kipindi cha chini ya miezi sita kujiandikisha.

Akisoma taarifa ya CCM tawi la Ruaha Mohamedi Ngashona ambaye ni mjumbe alisema viongozi hao wamejipanga kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa mtaa huo ambazo ni uharakishaji wa ujenzi wa zahanati, ukarabati wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa nyumba za walimu.

Kuwatambua kaya maskini na wazee kwa kuwapatia huduma muhimu, uimarishaji wa barabara ya kutoka Mnazimmoja hadi Ruaha na utekelezaji wa sera ya umeme vijijini hasa vilivyopitiwa na mradi wa bomba la gesi.

Katika mkutano huo jumla ya wanachama 43 walijiunga na chama hiyo kati yao wanne walitoka Chama cha Wananchi CUF .
 
Alafu Serikali inasema Viongozi wadini wanaosema wananchi wapige kura ya HAPANA ni wachochezi...............ila Mama namba moja wa nchi..........nikiwa na uhakika aliongea na mkuu wa kay anasema wapige kura ya ndiyo.
 
Huyu mama anafanya mambo mengi ambayo hakupaswa ayafanye.. Hivi kwanini hawa ma-first ladies wa siku hizi wasiwe kama mama Maria Nyerere..? Kazi yao iwe kuhakikisha waume zao wanakuwa katika right minds muda wote na kuhakikisha familia inaendelea vizuri.. Matokeo yake ndo hata muda wa kuangalia maendeleo ya mtoto huna mwishowe mtoto anafeli pamoja na kusoma shule kubwa..
 
Nijulisheni Ki-KATIBA huyu ni NANI,
 
wanaposema katiba ni bora basi wafafanue itawasaidiaje wananchi kuondokana na umasikini kiuharisia na je ni je kwa jinsi gani katiba inatoa suluhisho kwa kero za wananchi hasa ukosefu wa miundombinu na huduma muhimu kwa wananchi wa tz
 
Alafu Serikali inasema Viongozi wadini wanaosema wananchi wapige kura ya HAPANA ni wachochezi...............ila Mama namba moja wa nchi..........nikiwa na uhakika aliongea na mkuu wa kay anasema wapige kura ya ndiyo.

Watu wahamasishwe tu kujitiokeza kwa wingi kupiga kura na viongozi watendaji wa serikali na dini.

Lakini viongozi wa vyama vya siasa akiwemo huyu mama ruksa kueleza wanataka watu wapige upande gani.Huyu mama si kiongozi mtendaji wa serikali au dini ni mwana CCM na kiongozi katika chama cha mapinduzi ana haki kuongea hivyo.

Ila nadhani kuna tatizo la viongozi hasa wa dini kuchanganya mambo kisa eti wamemsikia raisi kasema watu wapige kura ya ndiyo.Raisi ni mwenyekiti wa CCM taifa.Akiongea mambo ya kutaka watu wapige kura ya ndiyo anaongea msimamo wa chama chake yeye akiwa kiongozi wa chama.

Lakini inapofika askofu ambaye anaongoza kanisa lenye wanachama wa UKAWA ,CCM na wasio na vyama naye akajitosa eti kupigia debe eti kura ya ndiyo au hapana hapo anakuwa hajui vizuri kazi yake kama kiongozi wa dini kwa waumini wake wenye vyama tofauti na misimamo tofauti ya kisiasa.Maaskofu ni vizuri wabakie kwenye majoho yao siasa wawaachie waumini.Askofu awaambie tu waende kupiga kura kwa kadri ya dhamiri zao kisha aendelee kuwaswalisha wakishatoka kupiga hiyo kura sawasawa na dhamiri zao.
 
Nijulisheni Ki-KATIBA huyu ni NANI,

Hatambuliki na katiba ya zamani wala hii rasimu ya ccm wanayoipigia debe.. Ndo maana hakuna kipengele kinacholazimisha rais lazima awe na mke.. Sema kwa kuwa ufisadi umetamalaki sasa na uvunjaji wa katiba umeshamiri ndo sasa imewafanya hawa wake kufungua NGO zenye anuani ya ikulu na kupiga madili ya nguvu..
 
Watu wahamasishwe tu kujitiokeza kwa wingi kupiga kura na viongozi watendaji wa serikali na dini.

Lakini viongozi wa vyama vya siasa akiwemo huyu mama ruksa kueleza wanataka watu wapige upande gani.Huyu mama si kiongozi mtendaji wa serikali au dini ni mwana CCM na kiongozi katika chama cha mapinduzi ana haki kuongea hivyo.

Ila nadhani kuna tatizo la viongozi hasa wa dini kuchanganya mambo kisa eti wamemsikia raisi kasema watu wapige kura ya ndiyo.Raisi ni mwenyekiti wa CCM taifa.Akiongea mambo ya kutaka watu wapige kura ya ndiyo anaongea msimamo wa chama chake yeye akiwa kiongozi wa chama.

Lakini inapofika askofu ambaye anaongoza kanisa lenye wanachama wa UKAWA ,CCM na wasio na vyama naye akajitosa eti kupigia debe eti kura ya ndiyo au hapana hapo anakuwa hajui vizuri kazi yake kama kiongozi wa dini kwa waumini wake wenye vyama tofauti na misimamo tofauti ya kisiasa.Maaskofu ni vizuri wabakie kwenye majoho yao siasa wawaachie waumini.Askofu awaambie tu waende kupiga kura kwa kadri ya dhamiri zao kisha aendelee kuwaswalisha wakishatoka kupiga hiyo kura sawasawa na dhamiri zao.

Kama mama Salma angewaambia wana-ccm kupiga kura ya ndiyo angekuwa sahihi. Lakini anapowaambia wananchi wa Lindi (wakiwemo ukawa na wale wasiokuwa na chama) anakosea. Anaingilia uhuru na dhamiri za watu.

Yatosha maovu yake kwa siku!
 
Ongeeni mambo ya maana acheni mbwembwe!!
 
Sijakuelewa. Kwa hiyo katiba hiyo inayohamasishwa na wana CCM ipigiwe kura ya Ndiyo....ambayo kwa akili yako unasema ni ruksa....itawafaaa wana CCM peke yao au hata wana UKAWA itawaongoza? Maana ingekuwa katiba ya Chama kwa maoni yangu isingekuwa shida. Anayesema ipigiwe kura ya Hapana maana yake kaona kuna kitu kapunjwa au haikumtendea haki. Usiangalie upande mmoja eti kanisani kuna wana UKAWA.

Kitu cha pili.....kwa kutumia hoja yako.......ina maana hayo maneno CCM huyasemea chooni? Maana jukwaani au kijijini au mjini wanapohutubia kuwa ipigwe kura ya NDIYO kuna UKAWA , ccm etc.......Ni PM nikusaidie materials ya Philosophy.........ili ujue tofauti kati ya Argument, Explanation and Description....ili uweze kujenga hoja.
 
Kama mama Salma angewaambia wana-ccm kupiga kura ya ndiyo angekuwa sahihi. Lakini anapowaambia wananchi wa Lindi (wakiwemo ukawa na wale wasiokuwa na chama) anakosea. Anaingilia uhuru na dhamiri za watu.

Yatosha maovu yake kwa siku!

Good reasoning.................na mie nimemuuliza....hayo maneno ya kura
ya NDIYO CCM huyasemea chooni? Maana sio kweli kuwa unaweza kwenda sehemu mtaa mzima ukawa CCM au CDM tu
 
Huyu mama anafanya mambo mengi ambayo hakupaswa ayafanye.. Hivi kwanini hawa ma-first ladies wa siku hizi wasiwe kama mama Maria Nyerere..? Kazi yao iwe kuhakikisha waume zao wanakuwa katika right minds muda wote na kuhakikisha familia inaendelea vizuri.. Matokeo yake ndo hata muda wa kuangalia maendeleo ya mtoto huna mwishowe mtoto anafeli pamoja na kusoma shule kubwa..
Kila unayemuona anang'ang'ania katiba ya Chenge na Sitta na kupinga rasimu yenye maoni halisi ya wananchi ya Jaji Warioba ujue alipo au alicho nacho kinapungukiwa na uhalali. Hivyo wanajitahidi kutofikishwa mbele ya sheria muda usio mrefu ujao, wakisema na huyu ni miongoni mwao utapinga!?

kuanzia sasa maaskofu ruksa kupiga kampeini makanisani,ila ikitoke waumini wanataka wapige kura ysa ndiyo wasiwafukuze uumini wao
 
Back
Top Bottom