sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
“Wawekezaji wanalalamika sana kumekuwa na urasimu mkubwa Tanzania, kodi kwa Wawekezaji hazieleweki, napokea taarifa kutoka kwa Wasaidizi wangu, Wafanyabiashara wanataka kuniona niwahakikishie kama watafanya kazi kwa utulivu ili warudi Tanzania”——-Rais Samia Suluhu baada ya kuwaapisha Viongozi wapya Ikulu Dar es salaam leo
“Wawekezaji wanataka kuja Tanzania lakini kwa mambo yetu wanakimbia, tuvute tena uwekezaji, tupate ajira,fedha izunguke,uchumi ukue, nikiwa Makamu wa Rais kuna Mwekezaji alikuja, sijui alitishwa nini!, nadhani kaambiwa tutakupiga kosa la uhujumi uchumi, akaondoka”———Rais Samia
“Vibali vya kazi vimekuwa janga, wanaosimamia vibali vya kazi wamejigeuza Miungu Watu , wamegeuza mradi, Mtu anawekeza mnalazimisha aweke Mtanzania, kila Mwekezaji ana haki ya kuweka Mtu anayemuamini yeye kwanini umlazimishe?, mtende haki”———Rais Samia
“Tunataka Wawekezaji wa-enjoy Tanzania, Makampuni yanafungwa Ndugu zangu sio uongo, tukiweka vikwazo tunawarudisha nyuma, wakiondoka uchumi wetu unashuka, ajira zinapungua na mzunguko wa pesa unapungua na hiki ndio kilio kikubwa cha Watanzania kuwa mifuko mitupu”———Rais Samia
#MillardAyoIkuluUPDATES