Mama Samia ubarikiwe sana kwa hii mikopo ya masharti nafuu kwa wakulima na wajasiriamali nchini pia naipongeza CRDB

Mama Samia ubarikiwe sana kwa hii mikopo ya masharti nafuu kwa wakulima na wajasiriamali nchini pia naipongeza CRDB

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Hii ilikuwa ndoto yangu ya siku nyingi sana na sasa Mama Samia kaitimiza. Binafsi nilikuwa nakerwa sana jinsi mikopo ya halmashauri na mingine ya serikali ilivyokuwa ikitolewa. Ilikuwa haina mfumo mzuri kwenye kutoa hali iliyokuwa inatoa mianya ya watu kujipigia na kutoirudisha. Mimi siamini kama kuna urahisi wa kupata utajiri wa kikundi kwa sababu wote kuwa na vision moja pia changamoto. Niliandika uzi kushauri.. Kulazimisha vijana wawe wajasiriamali/ wajiajiri ni kuzidi kuwapoteza zaidi. Sio wote wanaweza

Wiki kama 3 zilizopita kuna mwanangu mmoja kijijini akaniambia anko kuna hii mikopo ya serikali kwa riba nafuu kupitia CRDB tumeambiwa sisi wakulima tuombe. Sikuchukulia serious nikamjibu wewe timiza wajibu wako wa kuomba mambo mengine mwachie Mungu. Kweli kijana akajitosa.

Akawa ananipa updates ya kila hatua. Nikawa naona kama miujiza kwa sababu CRDB na wahusika wote hawakuwa na longolongo yoyote. Walifuata taratibu zote za mkopo bila kuangalia huyu mtoto wa nani na wa chama gani. Yaani hii mikopo haina CCM wala CHADEMA. Mwenye sifa za kupewa anapewa. Ninafahamu kuna watu toka CHADEMA, ACT na vyama vingine vya upinzani wamenufaika. Pongezi za dhati kwa CRDB kwa weledi uliotukuka.

Lakini kwenye mambo ya hela hawakosekanagi wahuni. Kwenye huu mchakato kuna watu ambao hudanganya watu watoe chochote kitu ili kupata mkopo. Hii ni mbaya sana. Kwa mfano kijijini kwetu kuna mheshimiwa diwani katajwa tajwa kutaka pesa za waombaji. TAKUKURU fuatilieni kwa karibu.
 
Hiyo mikopo labda masharti ni hadi uwe na kadi ya mbogamboga, wengine ni bora tufe njaa kuliko ku surrender kwa hilo lichama!.
Kwanini unasema LABDA badala ya kutafuta ukweli? Hii mikopo haina chama. Yeyote mwenye sifa anapewa.
 
Back
Top Bottom