tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,327
- 4,624
Mtafiti yupo kule NIMR Center. Anakesha kuandika tafiti mbalimbali ili apate ufadhili, pasipo msaada wowote toka NIMR HQ. Kwa jasho na damu anapata ufadhili na kupeleka pesa kituoni kwake ambazo zinasaidia hata kuendesha kituo. Halafu from nowhere anakuja mteule mmoja wa Rais anataka hizo pesa zipelekwe makao makuu, na kukatwa asilimia 15. Anataka ku control kila kitu, katika ulimwengu huu wa decentralization. Pesa yako kuipata toka NIMR HQ unapaswa uifanyie kazi ya ziada, utadhani unaomba ufadhili wa pili huko NIMR HQ.
Sasa itabidi wale ndugu zetu wa vituoni wasiandike andiko hata moja, tuwaachie nyie wa makao makuu tuone kama mtaletewa pesa huko mliko. Si mnaona wanafaidi sana.
Prof. Aboud ukifika sehemu, tumia muda kujifunza kwanza. Usikurupuke kama vile watangaulizi wako hawakufanya kazi yoyote. Hizo pesa za vituoni ambazo wenzenu wanahaingaika usiku na mchana kuzitafuta, hutoziona.
NIMR ni zaidi ya Mloganzila, usije iua NIMR kama yule mwenzako wa Ifakara.