Mama Sinyali Boss la Kariakoo

Mama Sinyali Boss la Kariakoo

We unaangalia mkorogo, hayo ni mafuta tu, nakupenda urembo, kujiamini, upambanaji wa kutafuta pesa, na kuongea vile mbele ya waziri, mbele ya umati si wote wanaujasiri ule, na kutokuogopa tra kusema mabaya yao, na ndio mana kafatwa na waandishi wengi na wamempongeza ujasiri ule.
 
Mimi ni Mjasiriamali wa vipodozi na niko Kariakoo kwa muda wa miaka 20 na zaidi, kero tunazokutana nazo hapa Kariakoo ni nyingi sana na zinavunja moyo, kero ya kwanza hatufanyi biashara kwasababu ya (TRA), Wateja sasa hivi wananunua mizigo nje ya Kariakoo wanaogopa TRA, kwa mana hiyo sisi tunashinda tu vibarazani maana hakuna biashara wala wateja"

"Watu wa TRA na watu wa Taka wanatuumiza sana, mimi mpaka nilishapiganaga na vitoto vya TRA ndiyo maana nilivyosikia Waziri Mkuu anakuja nikasema leo lazima niende nikatoe nyongo iliyonikaa kwa muda mrefu, nilivyoenda pale mkutanoni bahati nzuri Waziri Mkuu akaniita nikaenda kutoa baadhi ya kero zangu, nasema baadhi kwasababu bado sijamaliza nina mengi ya kumwambia Waziri Mkuu, bado naitafuta namba yake"

"Tumefirisika hatuna kitu, mimi nilikuwa na pesa yani hapa sina kitu, ili kujisukuma inatubidi tujiingize kwenye mikopo ya "kausha damu" ambayo kwa mimi binafsi mkopo wa "kausha damu" umevunja ndoa yangu, nimeachana na mume wangu kwasababu ya "kausha damu", "kausha damu" imeniharibu sura, sikuwa hivi, mimi ni natural sijajichubua hata kidogo hii ni ngozi ya Kichaga Og, ila kulia kila saa na mikopo ya kausha ndiyo imeniunguza sura"

"Hapa nimepungua sana watu wanaonijua wanashangaa sana, nina kg 198 ila nilikuwa na kg 210, natamani sana kupungua, natamani niwekewe puto hata sasa hivi, Peter Msechu siyo wa kuwekewa puto, mimi ndio natakiwa niwekewe hilo puto.

"Hakuna biashara Kariakoo, TRA wameua biashara yaani tumekaa tu lakini biashara hakuna, wateja wanaokuja wananunua kopo la mafunzo elfu 10, kwa siku unatoka na elfu 20 ya mauzo, hapo unalipa kodi, TRA na Taka, kuna biashara hapo?, zamani nilikuwa nauza milioni moja, moja na nusu mpaka milioni mbili kwa siku, nyumbani kwetu mimi ndio kama Bhakresa, ndugu wote wananitazama mimi lakini awamu hii nimeshindwa hata kuwapeleka watoto shule".

Aidha Bi Sinya amesema anavutiwa sana na Mbosso, kila anaposikiliza wimbo wa Mbosso moyo wake unakwatuka anajisikia raha burudani, hadi kufikia sasa hivi mama huyo anaendelea kujizoea maelfu ya followers huko Instagram, ambapo jana alikuwa na followers elfu mbili pekee na hadi kufikia leo sasa hivi ana followers elfu 15 na zaidi.

Credit: FB

View attachment 2628823
Alieleta hizi makeup auliwe.
 
Sinyali kama Sinyali, basi apewe maua yake.
 
Back
Top Bottom