Elections 2010 Mama Sitta aeleza alivyokamatwa na TAKUKURU

Elections 2010 Mama Sitta aeleza alivyokamatwa na TAKUKURU

Tena Mama Sitta, yule DC aliyekamatwa Kilimanjaro wote wamepeta. Hii rushwa ndani ya CCM ni jadi na utamaduni wao.
 
Huko CCM kumejaa uoza, hakuna mtu yoyote ambaye ni safi anaweza kubaki huko, woooote ni wachafu,walafi,mafisadi, hatuwezi kuwaamini hata kidogo ,hawa wanajuana, wamedhulumiana ndio maana wanaumbuana.Kwa maovu yote yaliyofanywa na serikali ya CCM kwa miaka mitano iliyopita sitegemei mtu yoyote msafi abaki ndani ya genge hili la kimafia linalokwenda kwa jina CCM .
 
of course amebambikiwa.. hivi hamjiuliza pamoja na kelele zote za watu kukutwa wakitaka kutoa rushwa hakuna hata mmoja ambaye amefikishwa mahakamani? Na wote watashiriki Uchaguzi J'pili. Lengo ni kutengeneza majalada ambayo yatatumiwa na Kamati Kuu kuwaengua baadhi ya wagombea ambao wanaweza kushinda kabisa uchaguzi.

Kubambikiwa huwa kupo lakini katika hili mazingira ya saa 7.30 usiku halafu na maelezo ya mtuhumiwa kwa pamoja vinatia shaka. Hivi kwa mtu muelewa na mwenye uwezo kama Waziri umepigiwa simu kuna mgonjwa halafu unafunga safari kwenda kumtazama badala ya kuwaelekeza wampeleke mgonjwa hospitali halafu wewe utakwenda kumwonea huko. Vinginevyo mama Sita angekuwa na utaalamu wa utabibu.
 
Kikosi cha Spika Sitta kinapaswa kuwa angalifu sana kwenye mchakato huu. Wakiendelea kufanya kama wenzao mambo yatawawia magumu sana. Ukiangalia hata kwenye vyombo vya habari "shouting headlines" ni majina yao kwa wingi hata wanapozomewa!
 
Mazingira ya Mama sitta yanatia shaka kidogo hasa muda na mahali.Lakini pia ningependa kujua huyo mtoto ana uhusianano gani na Mama Sitta.Kwanini mtoto mgonjwa asiwe amelazwa hosipital kwaajili ya matibabu na badala yake awe gest house ?.

upo pia uwezekano mkubwa hasa kipindi hiki cha kampeni mgombea kujikuta anakwenda sehemu za ajabu ajabu pengine kujijengea mazingira mazuri kwa wapiga kura.Inawezekana Mama Sitta aliamua kweli kwenda kumwangalia mgonjwa lakini yakaandaliwa mazingira yakumchafua ili aenguliwe kwenye vikao vya mchujo kamati kuu.

Ifahamike wazi Mama Sitta ni miongoni mwa wabunge wa CCM wanaojipambanua kama wapiganaji dhidi ya lile kundi la waathirika wa kashfa za kifasadi ambao sasa wanafanya kila juhudi kuhakikisha wanakuwa na nguvu ndani ya Bunge.Ukifuatilia kwa makini harakati zote za ufisadi katika chaguzi za ndani za CCM utagundua kwamba wanaCCM wanaokumbana na mkono wa TAKUKURU ni wale wanaojiita wapiganaji !.
 
of course amebambikiwa.. hivi hamjiuliza pamoja na kelele zote za watu kukutwa wakitaka kutoa rushwa hakuna hata mmoja ambaye amefikishwa mahakamani? Na wote watashiriki Uchaguzi J'pili. Lengo ni kutengeneza majalada ambayo yatatumiwa na Kamati Kuu kuwaengua baadhi ya wagombea ambao wanaweza kushinda kabisa uchaguzi.

Say like you mean it

Katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alishakaririwa na gazeti hili akisema kuwa mgombea ambaye atabainika kujihusisha na vitendo vya rushwa, ataondolewa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge hata kama atashinda kwenye kura za maoni.

and now i would like to know why mama sitta?
 
Ahhh...mtazamo wako kwamba kabambikiwa...mbona wengine huwasemei wamebambikiwa...Mtu anapelekwa mahakamani bada ya kila kitu kuwa tayari na kujua mashahidi ni akina nani..kuhusu kupelekwa kamati kuu hilo nakubaliana na wewe
 
Hivi sheria ikoje jamani tuelimishane, unaweza kushitakiwa kwa kosa la kuwa njiani kwenda kutoa rushwa?ivi mtu kama mama sita akikutwa na shilingi milioni moja ni lazima awe amelenga kutoa rushwa?ivi ni idadi ngapi ya simu mtu mmoja anaruhusiwa kumiliki na ikizidi hapo basi zinakuwa ni kwa ajili ya rushwa, ivi rushwa lazima itolewe kwenye bahasha, inamaana hata ile ya rada pia ilitolewa kwenye bahasha?

Huyu mama, na wengine wengi kweli wanatoa rushwa, lakini kwanini hawa TAKUKURU wanapofikia hatua wanamkamata mtu wasiwe wanakuwa na ushahidi wa mojakwamoja ndio wafanye ivo...sitetei mtoa rushwa yeyote, ila TAKUKURU bado sana!
 
maelezo ya mama 6 ,yanatatiza kweli saa 7 usiku unapigiwa cimu waziri unaenda kumuona mgonjwa? kama cio uongo ni nini? i respect her sana lakini maelezo yake yanatia shaka,na huyo katibu wa ccm wa nini kama ni relative kwa nini asingemchukua mtu wa nyumbani kwake amsindikize?uko utata hata kwa ambaye hajui mazingira ya rushwa
 
huyu mama maelezo yake ya utetezi yanatia kichefuchefu ;
1. akamwangalie mtoto mgonjwa saa 7 ucku , je yeye ni daktari?
2. mtoto yupo GESTI . kwanini sio hospitali?
3. kwanini achukuane na katibu wa ccm wakati wanaenda kumwangalia mgonjwa au huyo katibu wa ccm ni daktari?

mamaa anatuzuga ,mpaka ifike octoba tutasikia mengi ya ccm
 
Sasa na hao takukuru mbona huo mtego wenye wameutega 'kijinga' hivyo? Kwa maelezo yao na haya ya mama 6, sioni ni vipi takukuru wanaweza kupeleka kesi hiyo mahakamani na kushinda. Wangemwacha mpaka akamwone huyo 'mgonjwa' aliyeitiwa na ndipo wamkamate pamoja na 'mgonjwa' wake! Mbali na hapo ni kuchafuana tu kusipokuwa na manufaa yoyote na kuharibu credibility ya takukuru.

Kama katika scandal zote hizi hakuna hata moja wanayoweza kuipeleka mahakamani na kushinda nadhani Dr Hosea itabidi awajibishwe. Hivi hawa takukuru wanashindwa hata kupose kama wajumbe ili washuhudie hizo rushwa zikitolewa moja kwa moja. Ukifuatilia chaguzi hizi kwa kiasi kikubwa rushwa haijajificha kiasi cha takukuru kushindwa kupata ushahidi usio acha shaka!

Au wametumwa kufanya kazi nyingine tofauti?
 
Kwa nini ofisa wa TAKUKURU wa K'njaro kahamishwa na kushushwa cheo baada ya kumkamata DC wa Kasulu, Betty Machangu? TAKUKURU wanatumika ovyo, aibu!
 
of course amebambikiwa.. hivi hamjiuliza pamoja na kelele zote za watu kukutwa wakitaka kutoa rushwa hakuna hata mmoja ambaye amefikishwa mahakamani? Na wote watashiriki Uchaguzi J'pili. Lengo ni kutengeneza majalada ambayo yatatumiwa na Kamati Kuu kuwaengua baadhi ya wagombea ambao wanaweza kushinda kabisa uchaguzi.

na si ajabu wote wanaobambikiziwa rushwa wako karibu na waliokinyume na kundi la mafisadi ndani ya chama na bungeni.
 
Kwa nini ofisa wa TAKUKURU wa K'njaro kahamishwa na kushushwa cheo baada ya kumkamata DC wa Kasulu, Betty Machangu? TAKUKURU wanatumika ovyo, aibu!

Kwani hii kampuni inayoitwa TAKUKURU mmiliki wake I mean ma share holders wake ni akina nani? napata shaka sana na ni kampuni/taasisi.

But ikiwa DC wa kasulu alibambikiziwa, basi msumeno huo huo utumike kwa mama sitta ikiwa naye amebambikiziwa.
 
Margaret Simwanza Sitta
aliyekamatwa ni Mr. Sitta au Mrs. Sitta? Kwanini mtoa mada asiandike jina kamili katika jina la topic?:fear:
 
Mapungufu yako pande zote mbili, kama ambavyo wengi mmeeleza. Kuhusu kuhujumiwa, nadhani mama Sitta lazima ajilaumu mwenyewe kwa kujitengenezea mazingira hayo. Kwenye baadhi ya magazeti, inaelezwa kwamba alipekuliwa sanduku lake na kukutwa vitu hivyo. Sijui kwa mtu aliyekuwa amekwisha lala anapoamshwa kwenda kumuona mgonjwa anafungasha kila kitu?

Kwa hadhi yake, siamini kama alikuwa kwenye guest za uchochoroni. Hotel zote za kueleweka zina taratibu za kukabidhi valuables mtu unapotoka, kama sio kuwa na safe vyumbani. Kuwa na sanduku kwenye gari ni dalili kwamba alikuwa bado anaendelea na mapambano. Hawajatupa details kuhusu kukamatwa kwake Nzega kabla ya tukio la juzi.

Suala la ufisadi na upambanaji linaweza kuwepo. La msingi, TAKUKURU na sisi wachambuzi tujiweke kwenye mazingira ya kuita spade a spade. Kama kila jambo tutaliangalia kwa mtazamo huo, ipo hatari ya kutoka nje ya mstari.
 
and now i would like to know why mama sitta?

i like this question

Mkuu, hapo ndio funny politics zinapoanza... tunao akina chenge, mramba nk ambao wana kesi za kujibu laini they are allowed to pick nomination forms na kupiga campaign... at the same time tunaye mama sitta aliyetuhumiwa [bado ahata kesi ya kujibu haipo], tunaongelea kumuengua

sijui tuna matatizo gani and these double standards are really killing Tz apart
 
Mgonjwa ........ guest house ........ usiku saa saba ........ simu ilipigwa kwa kulzimisha ........ naonewa ...... nawasiliana na wanasheria wangu.

Sijamuelewa vizuri huyu mama. asaidiwe kujua ana wajibu wa kutoa maelezo ya kutosha
 
Back
Top Bottom