John...
Hotuba ile ya
Sophia Kawawa ni moja katika misiba mikubwa iliyowafika
Waislam wa Tanzania.
Baada ya
Sophia Kawawa kusema maneno yale katika ile hotuba yalifanyika
Maandamano makubwa Zanzibar ya kumpinga na mtu mmoja aliuawa na askari
walioamrishwa kuyazuia na wengine kadhaa katika waandamanaji kubakia vilema.
Baadhi ya washtakiwa 15 walisindikizwa na askari kwenda Chuo Cha Mafunzo
kutumikia kifungo chao.
Waandamanaji hawa walifikishwa mahamani na ilifanyika kesi iliyogusa
hisia za Waislam wengi Tanzania.
Mshtakiwa aliyetia fora kwa majibu yake mahakamani alikuwa
Sheikh
Said Gwiji ambae alikuwa katika wakati ule ni mwanafunzi wa
Sheikh
Nassoro Bachu kati ya masheikh vijana maarufu Zanzibar wakati ule.
Sheikh Gwiji na wenzake walihukumiwa kifungo sikumbuki miaka mingapi
lakini ni zaidi ya mwaka na walitumikia kifungo kile.
Nilifanya mahojiano na
Sheikh Gwiji nyumbani kwake Zanzibar mwaka wa
2012 kwa ajili ya kipindi cha TV Imaan Zanzibar na kisa hiki cha
Sofia
Kawawa alikieleza kwa kirefu.
Kushoto Sheikh Said Gwiji akifanya mahijiano na Mwandishi