Mama Sofia Kawawa

Mwaka 1977 unapelekwa UDSM...! Shikamoo. Sikutanii tena. Nashika adabu yangu. Na kama utapendezwa utakuwa unanituma dukani kibiriti au hata jagi la Maji ya Kunywa ndani, nitaleta!
 
Duh 1977?

Dada shkamoo
 
John...
Hotuba ile ya Sophia Kawawa ni moja katika misiba mikubwa iliyowafika
Waislam wa Tanzania.

Baada ya Sophia Kawawa kusema maneno yale katika ile hotuba yalifanyika
Maandamano makubwa Zanzibar ya kumpinga na mtu mmoja aliuawa na askari
walioamrishwa kuyazuia na wengine kadhaa katika waandamanaji kubakia vilema.


Baadhi ya washtakiwa 15 walisindikizwa na askari kwenda Chuo Cha Mafunzo
kutumikia kifungo chao.

Waandamanaji hawa walifikishwa mahamani na ilifanyika kesi iliyogusa
hisia za Waislam wengi Tanzania.

Mshtakiwa aliyetia fora kwa majibu yake mahakamani alikuwa Sheikh
Said Gwiji
ambae alikuwa katika wakati ule ni mwanafunzi wa Sheikh
Nassoro Bachu
kati ya masheikh vijana maarufu Zanzibar wakati ule.

Sheikh Gwiji na wenzake walihukumiwa kifungo sikumbuki miaka mingapi
lakini ni zaidi ya mwaka na walitumikia kifungo kile.

Nilifanya mahojiano na Sheikh Gwiji nyumbani kwake Zanzibar mwaka wa
2012 kwa ajili ya kipindi cha TV Imaan Zanzibar na kisa hiki cha Sofia
Kawawa
alikieleza kwa kirefu.


Kushoto Sheikh Said Gwiji akifanya mahijiano na Mwandishi
 
Mwaka 1977 unapelekwa UDSM...! Shikamoo. Sikutanii tena. Nashika adabu yangu. Na kama utapendezwa utakuwa unanituma dukani kibiriti au hata jagi la Maji ya Kunywa ndani, nitaleta!
Tena nywele zimebanwa na ribbon unajiona ni wewe tu
 
Asante sana mzee Mohamed Said kwa habari hii, wengi hatukuyafahamu haya.
 
Ni kweli kabisa mkuu, kwa mafanobhistoria ya Bi Titi Mohamed nilihadithiwa na mama yangu lakini mwaka 1964 sikuwepo duniani.
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…