Eliachim simpasa,
Mbunge wa zamani wa jimbo la mbozi mashariki alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya maadili ya bunge. Mama terry alisema kuwa dodoma huwa kunajaa machanguadoa kipindi cha vikao vya bunge, na baada ya bunge kumalizika machangu wanarudi jijini. Hakusema kuwa wabunge wanatembea na machangudoa.
Aliachim Simpasa, kwa madaraka aliyokuwa nayo alimwita Mhavile na Mama Terry na kuwahoji kwa zaidi ya masaa matano. Aliwatuhumu kuwa mhavile amemruhusu Mama Terry kuitumia Radio 1, kulidhalilisha bunge na wabunge.. Mama terry alituhumiwa kuwatukana wabunge na kuwakosea heshima.
Baada ya hapo Mhavile aliambiwa mama terry asiguse tena radio 1.. Na sauti yake ikisikika tu... Ndio ungekuwa mwisho wa kituo hicho cha radio.
Kuanzia hapo mama terry hatukusikia tena...
Kuna wakati zikaja taarifa zake kupitia magazeti kuwa mtoto wake amewakamatishia watu mbwa... Mbwa wa mama terry wameng'ata na kujeruhi....
Kesi ikawa kesi......
Hadi leo tunajiuliza muelimisha rika wetu huyu wa juisi za maganda ya viazi yuko wapi??Mwenye jibu atumwagie uwanjani..