Mercy Kanini kutoka Juja, Kiambu County, amejifungua watoto watano kwa njia ya kawaida katika Hospitali ya Thika Level Five, katika tukio adimu kuwahi kurekodiwa nchini Kenya.
Kanini alieleza kuwa alijifungua mtoto wa kwanza muda mfupi baada ya kufika hospitalini, huku madaktari wakijiandaa kumpeleka theatre kwa ajili ya upasuaji. Hata hivyo, baada ya kufanyiwa uchunguzi, aliruhusiwa kuendelea kujifungua kwa njia ya kawaida.
Watoto hao, ambao ni quintuplets, waliwekwa katika nursery kwa uangalizi wa karibu. Watoto watano kwa pamoja mara nyingi huzaliwa kabla ya wakati na huhitaji huduma maalum kutokana na uzito mdogo na changamoto nyingine za kiafya.
Kanini alisema hii ni mimba yake ya tatu, akiwa tayari ana mtoto wa kiume na wa kike. Alimshukuru madaktari na wauguzi kwa huduma waliompa yeye pamoja na watoto wake.
Mumewe, Evans Nyamhanga, alisema alitarajia kupata watoto wanne lakini aliona mtoto wa tano kama baraka na muujiza.
Hata hivyo, familia hiyo inakabiliwa na changamoto ya gharama za kuwahudumia watoto hao watano na imeomba msaada kutoka kwa serikali ya Kaunti ya Kiambu na watu wengine wenye nia ya kusaidia.
Source: TheStar.co.ke