Mama wa Kambo adhulumu mali za watoto wa Marehemu (Hadithi ya kweli)

jokielias

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
1,203
Reaction score
359
Habari wana JF. Hii ni mara ya pili ninarudia kuandika kisa hiki kilichotokea kwa Marehemu profesa Mmoja kwa jina tunamhifadhi. NI vizuri kuandika hii hadithi ili Jamii iweze kutambua uzembe wa kina baba ambao hawaandiki wosia mapema matokeo yake wanaacha majanga kwa watoto.

Kuna Professa Mmoja hapa Dar alifariki Mwaka 2012. Katika Maisha yake Marehemu Alioa Mwaka 1984 na mwanamke mzungu na kuzaa naye watoto wawili. waliishi kwa pamoja mpaka walipotengana mwaka 1990. Huyo Mwanamke mzungu alirudi kwao ulaya na kumwacha Professa na watoto wake wote wawili wakiishi pamoja na mali walizokuwa nazo kipindi hicho ikiwemo magari nyumba mikocheni na viwanja .
Huyo profesa alioa tena mwaka 2005 na Mama mwingine. walizaa mtoto mmoja wa kike. Huyo Professa naye alimjengea Nyumba na Kumnunulia viwanja huyo Mke wa pili. Kwa bahati mbaya Huyo professa alifariki mwaka 2012. Migogoro ilibuka baina ya Ndugu wa upande wa huyo Mama wa kambo na ndugu wa marehemu wanaowatetea watoto kwanza wa Marehemu.

Kikao cha ukoo kilikaa na kumteua msimamizi wa Mirathi ambaye alikuwa ni bamdogo wa hawa watoto wa kwanza.Yule Mama wa kambo alienda moja kwa moja Mahakama kuu kufungua shauri Mahakamani kuhusu kesi ya mirathi na alitaka Mahakama imteue yeye Mama wa kambo awe Msimamizi wa mirathi.

Kesi imeenda miaka 2 na hatimaye Judge akaamua achague wasimamizi wawili yaani mke wa pili wa professa na Bamdogo wa watoto wa marehemu wamechaguliwa kuwa wasimamizi.

Ndugu wameoona kukata rufaa itachelewesha muda na gharama wakaona njia ya kutatua tatizo hili ni kwamba wakae kikao cha pamoja na yule mke wa pili na kujadili mgawo wa mirathi iende vipi. lakini ukweli ni kwamba yule mke wa pili hawezi kukubali mali za marehemu zigawanywe kihalali kwa sababu naye ni msimamizi wa mirathi na vile vile ana ndugu na marafiki ambao wanamsapoti kwa nguvu zote lazima atataka asilimia kubwa ya mali iende kwake. kwahiyo kasheshe ipo katika hichi kikao wajadili vipi?

Nasikitikia hawa watoto wa mke wa kwanza maana sijui haki yao wataipata vipi na tayari ni machokoraa wa mtaa na ndugu zao wameishiwa sera na wanaonekana hawana ubavu wowote wa kumzuia huyu Mama wa kambo.

Mnakaribishwa kwa ushauri wenu. asante
Hii ni nyumba ambayo marehemu professa alijenga miaka ya 1988 na alikuwa akiishi na watoto wake wa kwanza. Hivi sasa Nyumba hio watoto wamenyanganywa na mama wa kambo. Na Mama wa kambo amekuwa akiitumia nyumba hio kwa maslahi yake binafsi pamoja na ndugu zake.

View attachment 176935
 
mbona kama umetoa hitimisho kabla hata ya mambo yenyewe??
hata kikao na mama bado. hamjajua atasema nini, atakataa au atakubali nini!
akienda na kukubali kugawa hizo mali mada yako itakuwa na maana tena??
 
Watoto wa bi mkubwa Wana Umri mkubwa tena zaidi ya miaka 28. Mapi naomba nikujibu yule mke wa pili alipambana vya kutosha ili apate kibali cha kusimamia mirathi ambacho kakipata. tetesi kutoka kwa watu na ndugu wanajua kwamba kama kikao hicho kikifanyika yule mama wa kambo hatakubali aachie mali ambazo zinawalenga watoto. kama huyu mama wa kambo alikuwa na malengo mazuri na hawa watoto wa mke wa kwanza basi angeshaachia zile mali za zamani kwa watoto. lakini toka Professa afariki hawa watoto hawajawahi kuonana na huyu mama wa kambo yaani wanaishi kwa ndugu zao. wakati huyu Mama wa kambo anakula bata anakaa kwenye nyumba ambayo ameikuta na anaendesha magari ya professa kwa raha zake. inasikitisha sana. kwahiyo hii mada niliyoitoa ina maana kubwa kwa jamii na ina fundisha vizuri.
 
NGoja maprofessor wa sheri waje hapa, nami niambulie mawili matatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…