Mama wa mchumba wangu ananikuwadia kwa mdogo wake

Mama wa mchumba wangu ananikuwadia kwa mdogo wake

I AM NO ONE

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2020
Posts
389
Reaction score
576
Habari, nina stori moja leo ambayo inaniumiza kichwa kabisa kuhusu mama wa mchumba wangu simuelewi hata kidgo ana nia gani na mimi.Juzi flani hivi nilikwenda kumsalimia alikuwa anaumwa nikafika kwake kwenda kumjulia hali ila kwa mda huo nilioenda mpenz wangu hakuwepo ambae ni binti yake alikuwa bado hajarud kutoka kazin.Nilivofika nikamkuta mdogo wake na mama mkwe wangu mtarajiwa pamoja na mama mkwe wangu mwenyewe wakiwa wameketi njee ya nyumba.

Nikawasilimia vizuri kabisa nikatoa vimzigo nilivo nunua nikawapa pale kama pole tukawa tunapiga stor zingine tu za kawaida mda kidg mdog wake akanyanyuka akaingia ndani tukawa wawili tu nje.akaniambia mwenzako bado hajarud kutoka kazini nikamwambia hta hivo nimewasiliana nae kaniambia yupo njiana anarudi nyumbani,akaniuliza hiv umempendea nini mwanangu kwanza hilo swali alivoniuliza moyo ulistuka paa nikasema kuna nn tena nikatizama chini nikamjibu mama unajua mapenzi huwa ni hayaelezeki na mimi sijui hta nilichompendea nimekjikuta nina amani moyoni mwangu kabisa kuhusu mwanao hivo yan.akaniambia hiv hujamwaona flani ambae sasa ni mdogo wake nikamwambia nimemuona mbona ni mzuri sana kuliko mchumba wako mmmh nikaguna nikasema ndio mzuri kwan hajaolewa nikamuuliza? akaniambia bado hajaolewa tena huyu ndo anakufaa zaid kuliko hta huyo unae mng'ang'ania ..

sasa baadae nilivota pale kwa yale mazungumzo yalinichanganya kdg..ila sasa mdogo wake anamiaka 31 mwanae anamiaka 24 mdogo wake kutokana na stori anazonipa demu wangu ananiambia huwa analalamika sana haolewi hana bahati alafu kazalishwa mtt mmoja na jamaa flani alafu pia sasa mbali na hapo kapangiwa nuyumba na mume wa mtu ila bado anataka kuolewa anasema yeye kachoka kuwa hawara umri umeenda sana.

sasa ulewa wangu ni kwamba huyu mama anataka kumpa neema mdogo wake kwakuwa mwanae bado binti hajazaa anaweza pata tu mwingine ila mimi ndo nijikanyage nikaopoe huo mzigo ambao tyar ushasoma kilometa za kutosha .
 
Huyo Mama mkwe wako huyo anakaa na mumewe au yeye nd'o kiongozi wa familia?

Mchumba wako kalelewa na huyu Mama pekee au kapata na malezi ya Baba?

Ikiwa mchumba wako kalelewa na huyu mama pekee,
Kuna tatizo kubwa sana hapo hata kwa mchumba wako utakuja kuliona.
 
Yawezekana unategwa ili uonekane mkwe wa aina gani.. mkwe anaekula wakweze au mkwe mkwekwe.. hufikirii hata ukimuacha huyo binti ukachukua huyo itakuwa si adabu!!.. Yani demu wako aje akuvue cheo Cha u baby mpk akuite baba mdogo,isitoshe hata nyeti zako anazijua!..

Shituka we Kobe utakosa mke komalia hapohapo.
 
mzee wao alivuta
 
hapa huyu mama sio mtu mzuri kabisa aise kama nanitega ki hv
 
Mama achana naee assume alikuwa anajifurahisha tuu...!! Kausha hata demu usimwambie ila akizidi kukomalia mchane ukweliii kuwa huwezi Oa mwanamke mwenye mtoto
 
Mama achana naee assume alikuwa anajifurahisha tuu...!! Kausha hata demu usimwambie ila akizidi kukomalia mchane ukweliii kuwa huwezi Oa mwanamke mwenye mtoto
yan mzee baba demu wangu sijamwambia lolote nimekausha kimya kabisa yan maana mpk daki hii nikisema ntaharibu mipango mingi sana
 
Back
Top Bottom