Mama watoto kila siku anaota anafanya mapenzi na watu tofautitofauti

Mama watoto kila siku anaota anafanya mapenzi na watu tofautitofauti

Mke wangu ana ujauzito wa miezi mitatu, lakini tangu amekuwa na mimba
amekuwa akiendelea kupata hedhi, Pia anaota anafanya mapenzi na watu tofautitofauti kila siku.
Na kuanzia amekuwa mjamzito, nimepoteza kabisa uwezo wangu wa kiume, jogoo hawiki kabisa
toa kwanza picha yako hiyo nikujibu
 
Mkeo atakuwa mtamu sana ndo maana majini yanampiga katerero daily.. Okoka kuepukana na mapepo haya... Nenda mlima wa moto ukaombewee
 
Nendeni kwa mganga especially mtoto wa sheikh Yahya Hussein hapo Magomeni bila hivyo matatizo yataendelea kwani si kwa kelele za maombi wala usanii wa kulia na ngoma kwa wingi

Nashauri hata uwe mbali wahi hapo kwa huyo mtoto wa Magomeni ili umaliziwe tatizo lako usidanganywe kwa maombi kwa waombaji wenyewe ni mamluki na wezi na hawana tena nguvu za imani toka kwa Mungu
Nilipoanza kusoma nilijua unatania!
 
Ni majini Mahaba ( spiritual Husbands) mpeleke kwa WALOKOLE akaombewe, wala usimchukie sio yeye na hayo mashetani yanakufanya wewe usiwe na hamu nae. Faqnya hima kabla madhara hayajawa makubwa zaidi
 
acha ujinga nenda kwa gyno haraka, hasa hilo la kutoka damu wakati mja mzito sio dalili nzuri, anaweza poteza ujauzito huo.

Japo kuna baadhi ya wanawake wachache ambao hupata hedhi hadi miezi 5 au 6 ya ujauzito.

Kuhusu kuota anafanya mapenzi na watu tofauti inaweza tokana na wewe kushindwa kumkuna kisawa sawa sababu jogoo wako hawiki. Sambamba na jogoo wako kutowika, kuna baadhi ya wanawake hamu ya ngono huongezeka maradufu wakati wa ujauzito au akishajifungua. Inawezekana hivyo vyote viwili vinapelekea mke kuwaza ngono muda mwingi mwishowe anaota.

Ukishaenda hospitali, uchanganye na sala utafanikiwa. Hata tunapokuwa waumini wazuri tutumie na akili za hospitali hata hao madaktari wanatimiza mipango ya Mungu.

Wewe kaka kuhusu jogoo kutokuwika, inawezekana umejijaza hofu ya majini mahaba, hedhi ya mkeo na mimba, utawikaje sasa?
nakubaliana na mawazo na uashuri mwingi mzuri ulitolewa ukiwemo huu hapa juu.lakini napenda kuongeza yafuatayo
jana nilikuwa kwenye semina moja ya dini mwalimu mmoja anaitwa pallangyo alieleza vizuri kuhusu tumbo la uzazi na nikaelewa mengi japo nilienda siku chache wanawake wengi wanamatatizo mno ya kuingiliwa na mapepo kupitia tumbo la uzazi. hivyo kama uko dar unaweza kwenda kanisa la lutheran kimara unaweza kupewa ushauri au huduma kupitia mafundisho na tatizo kwa kiasi fulani kama ni la mapepo likaisha hasa lako kama lipo hivyo ( usiogope hawaubiri lokole wananafundisha neno la mungu na wala hutalazimishwa kuokoka ) pole sana
 
Huyo anatakiwa kuombewa na watu waliookoka( Spiritual husbands ndio wanaleta hayo matatizo)
 
ndugu yangu hiyo ni mikakati ya ibilisi. Ingia kwenye maombi au nenda kwenye huduma ya kiroho iliyopo karibu nawe.
 
Mpeleke Hospital mkeo haraka achana na story za majini, ebu fugua mawazo yako na kua mwanamme mwenye mamuzi sahihi,mganga atakwambia mkeo umuwache alale kwake wewe urejee nyumbani baada ya siku 3 ukamchukue,kesha jifaidia vyakutosha.....
 
Back
Top Bottom