Mama wema atoa ya moyoni kuhusu diamond

Mama wema atoa ya moyoni kuhusu diamond

Binti Magufuli

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2011
Posts
7,479
Reaction score
5,157
SIJUI ni hasira au nini! Mama mzazi wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Mariam Sepetu ‘Mama Wema’ amemshika uchawi mpenzi wa bintiye, Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku akilaani vikali kitendo cha kumrudia mwanaye akidai lengo lake ni kumharibia maisha, Ijumaa Wikienda lina mkasa kamili mkononi.

Mama Wema alitoa hisia zake hizo juzi jijini Dar es Salaam alipoongea kwa simu na paparazi wetu huku maneno yake yakiwekwa kwenye kumbukumbu ya kinasa sauti cha Global Publishers.

ALIANZAJE?
Mwanamke huyo mwenye msimamo uliopitiliza kuhusu bintiye Wema, aliwasiliana na paparazi wetu akisema siku hiyo anataka kutoa dukuduku lake kuhusu Diamond ambaye pia ni staa wa Bongo Fleva.
Mama Wema alisema taarifa alizonazo kuhusu staa huyo ni kwamba, juzikati alikwenda kwa mganga f’lani na kuzika kondoo watatu ili Wema aharibikiwe maisha.


Mamawemacrop.jpg
Mama mzazi wa Wema Sepetu, Mariam Sepetu.

“Mimi nimekerwa sana na huyo Diamond wenu. Najua hajamrudia Wema kwa mapenzi, amemrudia ili apate nafasi ya kumharibia maisha. Ni kijana hatari sana.
“Nina taarifa kutoka kwa watu wa karibu naye kwamba alikwenda kwa mganga akazika kondoo watatu ili mwanangu aharibikiwe.


“Simpendi na sitaki hata kumwona. Hana nia nzuri na mwanangu, najua. Kwanza mama Diamond (Sanura Kasim) hampendi Wema, anampenda Penny, nampongeza sana kwa uamuzi huo,” alisema mwanamke huyo.

AMSHANGAA DIAMOND KULALIA KITANDA CHA KIGOGO WA IKULU
Mama Wema ambaye anasifika kwa ubabe, alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa amesikia Diamond sasa analala na kula kwa Wema. Akatolea tamko kitendo hicho.
“Kama angekuwa mwanaume kweli ana pesa zake angekubali vipi kulala kwenye kitanda alichonunua mwanaume mwenzake (Clement)?


wema2.jpg
Wema.

“Hiyo ni akili kweli? Vitu anunue mwanaume mwenzako halafu wewe uje kutumia bila haya. Halafu nimesoma kwenye gazeti moja (Amani) eti atamnunulia Wema vitu vyote alivyonyang’anywa na Clement, mimi nasema hawezi kumnunulia kamwe, anamdanganya tu,” alisema mama Wema.

ANACHOTAMANI
Mama Wema hakuacha kutoa donge lililokaa juu ya moyo wake, alisema:
“Nimeshamaliza arobaini ya mume wangu (Mzee Isaac Sepetu). Natamani siku moja nimfuate Diamond popote alipo nikamtandike makofi mpaka ashike adabu yake mwana…(tusi).”


AMPA TAHADHARI YA KUMKATA NA PANGA
Paparazi wetu alimpomuuliza mama Wema kama yupo tayari kumkaribisha Diamond nyumbani kwake ili wayaongee na kuwekana sawa na abariki uhusiano wao wa kimapenzi, alikuja juu.
“Aje wapi? Aje aongee na nani? Asije akajaribu kuja nyumbani kwangu, haki ya Mungu tena nitamkata na panga, hivi yule…(tusi) ananijua hanijui?”


ASEMA HAKUNA MZAZI YEYOTE ANAYEKUBALI UHUSIANO WA DIAMOND NA MTOTO WAKE WA KIKE
Mama huyo alizidi kuweka wazi kuwa hakuna mzazi yeyote Tanzania mwenye uchungu na mwanaye anayeweza kuruhusu uhusiano wa Diamond na mtoto wake wa kike.


“Nataka kukwambia kwamba hakuna mzazi yeyote hapa Tanzania anayeweza kukubali ujinga anaoufanya Diamond kwa mwanaye wa kike. Ni mtu gani ambaye hapendi kabisa kuwa mtulivu zaidi ya kuwachafua wasichana? Mimi naumizwa sana na yeye,” alisema mama huyo huku akisisitiza maneno yake yaandikwe gazetini.

diamond.jpg
Diamond.

WEMA YAKIMSHINDA ARUDI NYUMBANI
Bi. Mariam alizidi kutoa ya moyoni mwake na kusema kuwa inawezekana Diamond anafanya hivyo akijua kuwa Wema hana pa kwenda akishamuacha mweupe baada ya kumharibia uhusiano wake na Clement.


“Najua Diamond anaamini akishamchezea Wema na kumwacha atakuwa akitangatanga, lakini akumbuke ana kwao na hakuna shida yoyote, Wema atarudi nyumbani hapa na kuendelea na maisha yake kama kawaida,” alisema mama Wema.

NDOA YAO WATAFUNGIA CHUMBANI
Akizidi kutiririka, mama wa staa huyo alisema kama Diamond atamuoa Wema (kitu ambacho hakiamini kabisa) basi ndoa hiyo itafungiwa chumbani na upande wa Diamond tu ndiyo watakaoshiriki lakini upande wake hakuna atakayehudhuria.


“Ndoa yao watafungia chumbani, si hadharani tena wakiwa ndugu wa upande mmoja tu wa Diamond, sisi hatuwezi kushiriki ng’oo, ndugu zangu wakijitokeza tu nitakuwa na panga mkononi, watakiona cha moto,” alisema mama huyo.

DIAMOND, WEMA
Juzi, Diamond alipigiwa simu zake zote za mkononi lakini hakuna iliyopokelewa, akatumiwa meseji yenye madai yote, hakujibu.


Kwa upande wake, Wema alisema mama yake ametoa maoni yake kama ambavyo angeweza kutoa mzazi yeyote katika mtazamo wake.
 
Huyu mama anaboha, jitu mama zima kutafuta umaarufu kunuka kupitia vigazeti uchwara kwa majina ya watoto Wema na Domo.

Huyu angekuwa ni mama yangu lazima tungemuitishia kikao cha ukoo mpuuzi sana.
 
Udaku mwingine bana...ukifuatilia na ku be inspired lazima utaonekana tahira
 
Huyu mama anaboha, jitu mama zima kutafuta umaarufu kunuka kupitia vigazeti uchwara kwa majina ya watoto Wema na Domo.

Huyu angekuwa ni mama yangu lazima tungemuitishia kikao cha ukoo mpuuzi sana.

Yule ni mzazi, na mzazi anapoona mwanae anaaribikiwa lazima awe mkali japokuwa wema kashindikana, mi naona yupo sahihi, diamond kamponza mwenzie matokeo yake wema kaachwa na vitu kanyang'anywa,huyo ndomo anasema atamjengea nyumba wema wakat yeye anaishi nyumba ya kupanga(japokuwa amejenga mjengo wa maana) anamuaribia mwenzie, ila wema anatakiwa ajitambue ndomo ni staa na suala la kuchezea mademu sio rahis kuacha,hona wema alivyoaibika gari hana,kampuni hana na diamond kamuacha..
 
Huyo Mama anataka umaarufu tu kwani since when amekuwa concerned sanaa na maisha ya mwanawe kwani huyo Clement hana mke ? Yaani badala ya kusisitiza mwanae asiwe mzinifu aolewe yeye anaona bor aendelee kuzini na akina Clement ? Mmmmxxxiiiueww..
 
Yule ni mzazi, na mzazi anapoona mwanae anaaribikiwa lazima awe mkali japokuwa wema kashindikana, mi naona yupo sahihi, diamond kamponza mwenzie matokeo yake wema kaachwa na vitu kanyang'anywa,huyo ndomo anasema atamjengea nyumba wema wakat yeye anaishi nyumba ya kupanga(japokuwa amejenga mjengo wa maana) anamuaribia mwenzie, ila wema anatakiwa ajitambue ndomo ni staa na suala la kuchezea mademu sio rahis kuacha,hona wema alivyoaibika gari hana,kampuni hana na diamond kamuacha..

Na wewe ni walewale tu ukiwa buku 7 fc hata akili zinaruka, kwahiyo hao kina Shigongo wanaotengeza pesa kwa kuuza habari za kijinga ndio wanamsaidia Wema?

Mama yake Wema hana adabu wala akili ndio maana hata ndoa yake ilimshinda. Like mother like daughter.
 
Na wewe ni walewale tu ukiwa buku 7 fc hata akili zinaruka, kwahiyo hao kina Shigongo wanaotengeza pesa kwa kuuza habari za kijinga ndio wanamsaidia Wema?

Mama yake Wema hana adabu wala akili ndio maana hata ndoa yake ilimshinda. Like mother like daughter.

Kwa kias chake wanamjenga na wanamsaidia, sasa sisi tungejuaje kama kanyang'anywa gari na vifaa vya ofisini?, hata yeye anafadhaika na ndo maan kakimbia nchi kwa muda, maana clement kamkosa na diamomd aliyemshobokea naye kamwaga
 
mmh mimi haya magazeti ya udaku wala siyaaminiga
 
mmh mimi haya magazeti ya udaku wala siyaaminiga

Don't even waste ur time, toleo lijalo utasikia Kanumba aonekana Tabata.....

Shigongo amefiwa na Baba yake lakini haandiki kufuru za kumfufuwa Baba yake ila anajisikia raha kuandika habari watu waliopoteza wapendwa wao na wanahitaji faraja na kusahau yaliyotokea. Halafu jinga hilihili eti linajifanya ni mlokole.
 
Wanauzi na wanaboa sana watu wanaojiona wazuri nakukosoa kazi ya Mungu. Binadam kaumbwa na Mungu wala hakuna mtu anayejichagulia aweje. Nn maana ya DOMO
 
huyu mama mara amsupport bintiye mara ageuka.....inawezekana Wema ameridhi tabia ya mamake enzi zake
 
Wanaiuzi sana watu wanaojiona wajan a. Binadam kaubwa na Mungu wala hakuna mtu anayejichagulia aweje. Nn maana ya kupata mtu. DOMO

Tulia kabla haujacoment na hata ukipost ujipe muda wa kusoma kile ulichopost na ndio maana kuna option ya kuedit.
 
Mama Wema Haoni hatari Wema kutembea na waume za watu ukizingatia wakati alipoanza kutoka na Mzee Sepetu alikuwa nae anatembea na mume wa mtu...
 
Najua wananipinga,ila naamini nitashinda (diamond voice) uswazi take away rmx...
"Nlikuwepo":bolt:
 
Back
Top Bottom