Mama yake Diamond Arejeshwa toka India, Afya yake kwa sasa inatia Moyo

Mama yake Diamond Arejeshwa toka India, Afya yake kwa sasa inatia Moyo

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Mungu ni mkubwa :Mama mzazi wa Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’, amerejeshwa Bongo kutoka India ambapo afya yake imetengemaa.
Habari kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya familia ya jamaa huyo, kimesema kwamba tayari
Sandra amesharejea katika hali yake ya kawaida na ndiyo maana akarudi Bongo baada ya kulazwa hospitalini nchini India kwa kusumbuliwa na ugonjwa wa kupooza.

Mwanafamilia huyo alisema kwamba, Diamond na mama yake walirejea nchini wikiendi iliyopita baada ya kufanyiwa matibabu ya kina na madaktari kujiridhisha kwa hali ya juu dhidi ya afya yake ambapo waligundua hali aliyonayo kwa sasa imetengemaa hivyo wakamruhusu kurejea kuungana na familia yake.

Habari zilieleza kuwa kwa sasa bimkubwa huyo yupo fiti na anaendelea na mazoezi ya kawaida huku akimalizia dawa alizopewa na wataalam hao wa afya.
 
Hongera sana Diamond kwa kumuuguza mama yako,
Nanyi vijana wengine muige kutoka kwa mwenzenu.
 
Sio madaktari?

Kwani mungu Si hadi kwao tandale yupo?

Mungu ni muweza ya yote...

kwani wangapi walienda india na hawajarudi...unadhani madaktari wa india ndiyo wamemponya peke yao bila Mungu ambae yeye ndiyo anaamua muda gani amchukue kiumbe chake....
 
Sio madaktari?

Kwani mungu Si hadi kwao tandale yupo?

Mungu ndiye wa kushukuriwa hata kama madaktari ndo wamefanya kazi ya kibinadamu ya kumtibu lakini Mungu ndiye kampa uhai. Hivyo ndivyo ninavyoamini mimi.
 
Back
Top Bottom