Mama yake Uhuru Kenyatta aondolewa ulinzi

Mama yake Uhuru Kenyatta aondolewa ulinzi

Hapo mama analazimishwa amkanye Mwanaye (Uhuru) kwa sababu anatuhumiwa kum support Raila kuwalipa wahuni kuleta vurugu na uharibifu wa mali Kenya..sasa kama mwanao analipa watu wafanye vurugu hashindwi kulipa walinzi binafsi kukulinda...

Duuh ila kisasi siyo kitu kizuri..uvumilivu na uungwana unahitajika hapa.
Hapo wahuni watavamia nyumbani Kwa mama huyo, Kwa kisingizio police wote wapo kuzuia maandamano. So wakitaka ulinzi kusiwe na maandamano
 
sasa kama mtu analeta ujinga, na wewe ndio unamlinda, alitegemea nini? ondoa ulinzi kwa mwanae, na ondoa ulinzi kwake ili wajilinde wenyewe. uhuru alishaharibu sana, alitakiwa kunywea ili amalizie uzee wake vizuri. unaona kabisa jamaa ameshika rungu halafu bado unaleta bifu.
 
This is wrong in so many different levels....

Unaweza ukajiuliza kama alipewa hao walinzi kwanini leo waondolewe (Au ndio nikune nikukune)?!!

Ila swali kubwa zaidi je ni sawa hawa watu waendelee kulindwa / kuhudumiwa kwa kutumia Tax Payers money ?!! Yaani kwenye pensheni yake na marupurupu anakosa pesa ya kujiwekea ulinzi ?

Kwanini nasema hayo - (hili gap la have and have not linavyozidi kuongezeka na chuki baina ya matabaka inaongezeka) mambo kama haya ndio yataongeza chuki kwa wasionacho - kwamba iweje mimi nisiye na kitu najilinda alafu yule ambaye anaweza ku-afford walinzi ninamlipia walinzi ?

Hard Times are Coming ahead...
 

Serikali imeondoa walinzi wa aliyekuwa Mke wa Rais Mama Ngina Kenyatta katika nyumba yake ya Gatundu na Muthaiga.

Kulingana na maafisa, Mama Ngina, ambaye pia ni mamake Rais wa zamani Uhuru Kenyatta, maafisa wake wa ulinzi waliondolewa jioni ya leo muda wa saa kumi na moja jioni huku maafisa wa Kitengo cha Huduma ya Jumla na Polisi wa Utawala wakiambiwa waondoke na kuripoti katika kituo cha polisi kilicho karibu.

Kulingana na maafisa, Mke wa Rais wa zamani hakujulishwa chochote kabla ya utekelezaji.

Kabla ya kurejeshwa kwa mara ya kwanza mwaka jana, alikuwa na jumla ya walinzi 30 waliokuwa wakilinda majengo yake yote pamoja na mkuu wa zamani aliyekuwa mkaguzi mkuu.

Mama Uhuru aliachwa na walinzi nane, mwenye cheo kikubwa akiwa Sajenti Mkuu, ambao sasa wote wametakiwa kurepoti kwenye vituo vyao.

======

The government has withdrawn former First Lady Mama Ngina Kenyatta's security at her Gatundu and Muthaiga homes.

According to officials, Mama Ngina, who is also former President Uhuru Kenyatta's mother, had her security withdrawn this evening at about 5pm with officers from the General Service Unit and Administration Police told to leaveand report to the nearest police station.

According to officials, the former First Lady was not notified of the actions by the government, before implementation.

Before the first recall last year, she had a total of 30 officers guarding all her premises combined with the seniormost back then being a chief inspector

The former first lady was left with eight officers in total and the senior most being a senior sergeant, who have now all been recalled.
Inaelekea Ruto naye ni mtu wa visasi.
 
Back
Top Bottom