Mama yangu Tanzania -sensa 2022

Mama yangu Tanzania -sensa 2022

Ivan conspicuous

Senior Member
Joined
Jun 19, 2022
Posts
103
Reaction score
83
Ni rushwa, ufisadi na upendeleo wa kutisha.

Behold! Behold!
Tazama! Tazama!
Na. 164. Tabitha Nyansika Getama karani wa sensa kata ya kivule wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar Es Salaam ~ mtoto wa Diwani wa kata ya kivule.

Na. 174. Yusuph Nyansika Getama karani wa sensa kata ya kivule wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam ~ mtoto wa Diwani Kata ya kivule.

Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake aliwahi kusema " chagueni mgombea atakaekidhi matarajio ya wananchi sio matarajio yako wewe mpiga kura". Sensa ya mwaka huu ni ya kukidhi matarajio ya watawala na watoto wao (nepotism). Mwaka huu kitaeleweka vinginevyo ondoa hizi namba kabla ya KESHO ambayo Ni cku ya semina. Rudisha majina mliyoyahujumu kwa kuyafisidi.

Mama SAMIA fahamu kuwa watawala huku chini wanaharibu taswira nzuri ya nchi yetu Tanzania. Huu mchakato unaharibiwa Mheshimiwa Rais nakuomba uchukue hatua kunusuru mchakato huu. Wakuu wa wilaya wao wanapitisha bila kupitia jina moja baada ya jingine. Mimi nimepitia na ninaendelea kupitia na kama kweli hatua yoyote haitachukuliwa nitaamini Ile barua ya UVCCM Mbeya.
 
Boss hii nchi ya kisenge sana bila connection wewe sawa na mkenya tu morogoro pia tunapitia iyo kitu kuanzia postikodi hadi sensa wanaopata ni walewale wenye connection na watendaji wa kata na waume zao na familia zao, mi nipo kata ya kihonda morogoro , afisa mtendaji wa hapa ni balaa ana mume wake kwenye postikodi aliapply na alipata ata na hii ya sensa kapata tena kwa connection ya mke wake, kwanza majina walitoa usiku kama matokeo ya form 6😀😀 na waliopata ni kwa connection, hii nchi imekuwa ya ovyo sana bila connection haupati kazi ata uwe na GPA ya 5 labda upate kwa probability ila haki hakuna fursa za kata zipo mikononi mwa afisa watendaji na watu wao, Elimu pekee haisaidii tena, mi na bachelor degree yangu nakosa ukarani anapewa form 4 aliyezingua kabisa😀😀kuna familia watu wote waliapply na wamepata eti😀😀
 
Ndo maana kuna watu walisepaga zao ughaibuni baada ya kuona tz miyeyusho
 
Back
Top Bottom