Mama yupo sana sio wakati mzuri wa katiba mpya

Mama yupo sana sio wakati mzuri wa katiba mpya

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Mimi ni mdau ambaye natamani katiba mpya lakini sio wakati wake. Kwenye janga la Corona na baada ya kimpoteza Raisi huwezi kudakia katiba mpya maana watu watakuwa wanajadili wakiwa na matatizo mengi sana mengine vichwani.

Ushauri wangu ni kwamba vitu ambavyo wanaweza kufanya bila katiba mpya

1. Tume huru
2. Sera ya diaspora

Mama anaweza kufanya hivi bila kubadilisha katiba. Kwa sasa ukweli huwezi kuingiza mijadala ya kugawanya nchi wakati wewe ni Raisi mpya yeye sio mjinga
 
We nimudau wa katiba mpya ila hautaki katiba mpya kwa sasa. Kama tulifanya uchaguzi na corona akiwepo leo kazuia nini juu ya mchakato wa katiba mpya?
 
Iwapo Mungu wetu wa mbinguni amepanga tupate katiba mpya,
Lazima iwe..........,.......,....,........,..
 
Mimi ni mdau ambaye natamani katiba mpya lakini sio wakati wake. Kwenye janga la Corona na baada ya kimpoteza Raisi huwezi kudakia katiba mpya maana watu watakuwa wanajadili wakiwa na matatizo mengi sana mengine vichwani...
Issue sio Mama kuwepo sana. Bali issue ni kutenda kazi za kiongoza nchi kwa kufuata katiba. Kama hata hii mbaya iliyopo bado anaikanyaga je! Hiyo mpya ataiheshimu?
Mikutano ya vyama vya siasa ni takwa la kikatiba. Mama kachemka ati apewe muda?? Kweli??
 
Mimi ni mdau ambaye natamani katiba mpya lakini sio wakati wake. Kwenye janga la Corona na baada ya kimpoteza Raisi huwezi kudakia katiba mpya maana watu watakuwa wanajadili wakiwa na matatizo mengi sana mengine vichwani.

Ushauri wangu ni kwamba vitu ambavyo wanaweza kufanya bila katiba mpya

1. Tume huru
2. Sera ya diaspora

Mama anaweza kufanya hivi bila kubadilisha katiba. Kwa sasa ukweli huwezi kuingiza mijadala ya kugawanya nchi wakati wewe ni Raisi mpya yeye sio mjinga

..Katiba yetu ya sasa hivi inaruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

..Mama Samia kazuia mikutano hiyo, akidai wabunge peke yao ndio wafanye mikutano.

..kila mtu anajua kwa upande wa Tanganyika kuna mbunge mmoja tu toka upinzani.

..Je, uamuzi huo ni sahihi?
 
Back
Top Bottom