Mama'ake anapodandia bili ya mwanawe!


sasa mtu ameolewa na maisha yake tumfanyeje? akiumwa ndio tunampeleka hospital, akitaka tumpikie we will do that, ni vile ye mwenyewe kakatalia, unasema atatuchukia?? imagine huwa we are praying yasijetokea, coz mwisho wa cku she is our blood! na ameolewa na mdhungu, but the guy yupo so strictly kwamba matumizi yamtoto yapelekwe home and not money, mkewe atahudumia mwenyewe. HATAKI KABISA KUSIKIA AMETUMIWA PESA!
 
ruta kwa kuona hoja yako ya laki saba imepigwa chini na strong woman wa jf umeamua wazi kumsingizia mwanamke mwenzetu kwa kudai hiyo 2.1 milion si ndio eeeh!!.kama ww ni mmoja wa mawaziri waliotemwa na jk hata sion tabu kudai hiyo pesa ati.
 

ummu kulthum angalau huyo wa akaka yako alikuwa ni mke huyu siye ni mtu baki tu ambaye tulifanya maamuzi fulani miaka michache iliyopita....................sasa kaja juu hataki utani.....lol
 
Last edited by a moderator:

Pole in that case, blackmailing ni saizi yake; she knows how to play her cards well!

Ni ndege mjanja kanaswa kwenye tundu bovu! Ila kwa mnavyotutenda, bora wengine watulipizie kidogo! LOL
 
Last edited by a moderator:

[MENTION]Buswelo[/MENTION].....................u are very wise wawe na hata wanajua kusema asante kwa yote yale tuliyowafanyia badala ya kuona huu sasa umekuwa mradi wa kivuno cha bei poa..........
 
Ukute anakulipisha na uchakavu ('depreciation') uliomsababishia kwa kumzalisha. Kwa wengine kuzaa kunawachakaza kweli!

na huyo anayeishi naye mbona hambandiki hizo gharama za kuchakaa....................hivi ni nani humchakaza mwenzio.................mimi naona ndiye niliachwa nyan'ganyan'ga
 

haya kaka ruta nimekusoma.pole kwa matatizo,matatizo ni sehemu mojawapo ya maisha,hope u wil handle it.goodluk
 

lemonade huo muda uko wapi...........na isitoshe tuna makubaliano ambayo kila mwezi anatumiwa tatizo anadai hazitoshi ataka mara tatu yake......................
 
Last edited by a moderator:

Kigarama it is tough being a man of substance and means......................
 
Last edited by a moderator:
lemonade huo muda uko wapi...........na isitoshe tuna makubaliano ambayo kila mwezi anatumiwa tatizo anadai hazitoshi ataka mara tatu yake......................

Kwakuwa unataka kuprotect jina lako inabidi uwe kondoo tu, labda ujaribu kurenagotiate.
Otherwise tazama jinsi ya kutumia intelejensia kwakuwa inaonekana wewe ni "mtu fulani" so utakuwa na maujanja ya kumbana
 
Last edited by a moderator:
Kwakuwa unataka kuprotect jina lako inabidi uwe kondoo tu, labda ujaribu kurenagotiate.
Otherwise tazama jinsi ya kutumia intelejensia kwakuwa inaonekana wewe ni "mtu fulani" so utakuwa na maujanja ya kumbana
[MENTION]
Lemonade[/MENTION] nakushukuru sana kwa ushauri wako mzuri.......................nitauzingatia.
 
Haika..........mie siyo hit and run hata chembe kila kitu kilikusudiwa ni mtu baadaye kunibadilishia somo kinyume na makubaliano yetu ya awali...............ninajilaumu kwanini sikuyaandika...........

Haswaaaaa, Makubalioano hayo hayo ndio niliataka kuongelea, siku hizi wasichana wachache sana wa umri wa over 20 wanaweza kujishtukia wana mimba bila kuua na kushindwa kufanya maamuzi ya kibinafsi zaidi.
Hivyo huo wa kwenu nahisi ulikuwa ni uamuzi wa watu wawili wazima, wenye utashi (uliokufa kwa muda) mkaamua kufanya mlilofanya.
Lakini kwa kuwa maamuzi yenu hayakusimama kwenye kweli, hayo ndio matokeo yake.
Kwa kawaida, maisha tangu vizazi vingi kiasi vilivyopita, mtoto anatakiwa azaliwe kwenye mazingira ya familia yenye baba mwanaume na mama mwanamke, wenye misimamo thabiti ya familia, hawajui kila kitu, lakini wamechagua kumsaidia Mungu na ulimwengu, kuongeza kizazi cha binaadamu, na kulea mtu ambaye atakuwa tegemeo la viumbe.
Shorkcut zilizopo siku hizi, hakuna wa kuzicontrol, ila ni wewe na utashi wako,
Na ujue sheria ya mungu ilvyo ya ajabu, kwa mtazamo wa kawaida, ni ngumu, ila kwa undani ni rahisi na shortcut kuliko zingine zote.
Hapa sisemei Dini,
Mtu yoyote akifuata utashi wake wa ndani, bila kuwa mnafiki, mbinafsi, huwezi kufanya maamuzi kama hayo. Kamwe!!!
Ila kwa udhaifu wetu, mara kwa mara tunarudia makosa yale yale.
Makovu lazima yawe machoni mwako, lazima ujifunze kuishi na matokeo ya makosa yako.
Yeye, dada, sitaki kumgusia, sitaki kuficha makosa yako kwa ajili ya makosa ya mtu mwingine, asingekuwa yeye angekuwa mwiningine, ila wewe uko hapa. Next time nadhani utaamua vingine, na pia wadogo zako, sidhani kama unaweza kuwashauri kuwa its okay kufanya maamuzi kama yako. (that is a good thing to the future generation)
 

Mpangie mwana chumba, ajitenge na mamaye,
hadi apate mchumba, hapa si wewe ni yeye,
tajitenga na ushamba, ka meno na kiseyeye,
VYA MLEVI VISHALIWA, MGEMA ATAPATAPA.

tashibisha vya mlevi, tumbole kuning'inia,
wala huu si uchimvi, wahenga wanatambua,
ngadu wala sii mwivi, mwendowe tu sio nia,
VYA MLEVI VISHALIWA, MGEMA ATAPATAPA.

Mgema atapatapa, zamu imemuwadia,
eti harufu ya papa, ndio anasingizia?
kitaa anajitapa, kama jaji rugazia!
VYA MLEVI VISHALIWA, MGEMA ANATAPATAPA.

kakongorokea mediko, kaponzewa na mwanao!
simchumie viboko, akageuka kideo,
ambebe kwa mbeleko, kama mbege kwa kileo.
VYA MLEVI VISHALIWA, MGEMA ANATAPATAPA.

Kaditama wa aama! sumari nagongomeka,
mwanao kwake mama, utumbo umeungika,
takulaje vya shirima, mwanao macho tumbuka?
KUZIZOA SIFA KWA MWANA, MTUNZE NA MAMAYE. Rutashubanyuma
 
Last edited by a moderator:
lemonade huo muda uko wapi...........na isitoshe tuna makubaliano ambayo kila mwezi anatumiwa tatizo anadai hazitoshi ataka mara tatu yake......................

Mkuu mbona wapata shida na kuianika akili yako kirahisi hivi, gharama ya upendo mmejaaliwa MTOTO, Hasara ya chuki timiza wajibu mchungu. hatuung'oi mwiba kwa kuushindilia utokee upande wa pili wa mguu!
 
Last edited by a moderator:
Pole in that case, blackmailing ni saizi yake; she knows how to play her cards well!

Ni ndege mjanja kanaswa kwenye tundu bovu! Ila kwa mnavyotutenda, bora wengine watulipizie kidogo! LOL

Kaunga kisasi siyo chako hata siku moja..........Mwachie Muumba
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mbona wapata shida na kuianika akili yako kirahisi hivi, gharama ya upendo mmejaaliwa MTOTO, Hasara ya chuki timiza wajibu mchungu. hatuung'oi mwiba kwa kuushindilia utokee upande wa pili wa mguu!

jogi mawzo mazuri sana....................lakini msumari unapong'ang'ania mguuni unaufanyaje?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…