Mamake Lulu Na Kanumba Wala Kiapo Cha Kimila

Mamake Lulu Na Kanumba Wala Kiapo Cha Kimila

Ibrahim300

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2010
Posts
390
Reaction score
68
LULUMAMAYAKENAMAMAKANUMBANA3.JPG
ULE udugu wa ukubwani kati ya wazazi wa mastaa wa filamu Bongo, Lucresia Karugila ‘Mama Lulu' na Flora Mtegoa ‘Mama Kanumba' umezidi kukua kufuatia kwenda Bukoba, Kagera kwa ajili ya kula kiapo cha kuimarisha undugu huo.Wazazi hao wawili walijikuta katika undugu kufuatia Elizabeth Michael ‘Lulu' kupata mkasa wa kifo cha aliyekuwa nyota wa filamu, marehemu Steven Kanumba kilichotokea Aprili 7, 2012.

Lulu alidakwa akihusishwa na kifo hicho na kuswekwa mahabusu mpaka mwaka jana alipoachiwa kwa dhamana na mahakama kuu huku kesi hiyo ikiwa kwenye mchakato wa kuanza kusikilizwa.
Tangu kuachiwa kwa Lulu, Mama Kanumba amekuwa karibu na staa huyo akisahau yaliyotokea. Ukaribu wa Mama Kanumba kwa Lulu ukajikuta ukiunga moja kwa moja kwa mama wa Lulu ambapo wote watangaza wamekuwa ndugu.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"]
mamalulu.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Lucreshia Kalugira[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar, Mama Lulu alisema yeye na Mama Kanumba wanaondoka leo (Jumanne) kwa ndege kwenda Bukoba ambako, mbali na kumuuguza mama mzazi wa Mama Kanumba ‘Bibi Kanumba', lakini pia wataitumia nafasi hiyo kula kiapo cha kimila ili udugu wao uwe wa damu.
"Tunaondoka Jumanne kwa ndege, tunakwenda Bukoba. Kule kuna kumjulia hali bibi wa Kanumba ambaye anaumwa, lakini pia tutaitumia nafasi hiyo kula kiapo cha kimila ili undugu wangu na Mama Kanumba udumu mpaka kifo," alisema Mama Lulu.
Kuhusu kuwepo madai kwamba, yeye na Mama Kanumba wapo ndani ya bifu zito, Mama Lulu alikanusha akisema haitatokea.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
"Mimi na Mama Kanumba tuwe na bifu? Haitatokea. Ndiyo maana tumefikia hatua hiyo ya kula kiapo cha kimila," alisema Mama Lulu.
Kwa mila na desturi za makabila mengi Tanzania, watu wanapopenda kiasi cha kula kiapo kuwa ndugu (yamini) kila mmoja huchanjwa kidole kisha kuunganisha na cha mwenzake huku damu zikitoka.
Baada ya hapo, kila mmoja hunyonya kidole hicho chenye damu tendo ambali huaminika kuwa ndilo huunganisha undugu kuwa kama wa damu. Wazazi hao wote ni wenyeji wa Mkoa wa Kagera.

Stori imedondoshwa kutoka bkuHABARI
 
Ina maana huyu mama yake Kanumba tangu alipokuja kwenye wa mwanaye amegandiamo Darisalaam?

Hawa kina mama hasara tupu, yani hapo amekosekana mama yake Wema tu.
 
Kweli pesa shetani hivi niwaulize wanawake,unaweza kufanya undugu na mtu aliyesababisha kifo cha mwanao wa pekee wa kiume hata kama umemsamehe?hivi huyu mama anajisikiaje akiwa karibu na Lulu?kusamehe kupo lakini huyu ni vihela anavyopewa na Lulu ndo vinamfanya amsahau Kanumba!Samehe then mpotezee usiwe naye karibu unless kama haukua na feelings na mwanao
 
View attachment 133559
ULE udugu wa ukubwani kati ya wazazi wa mastaa wa filamu Bongo, Lucresia Karugila ‘Mama Lulu’ na Flora Mtegoa ‘Mama Kanumba’ umezidi kukua kufuatia kwenda Bukoba, Kagera kwa ajili ya kula kiapo cha kuimarisha undugu huo.Wazazi hao wawili walijikuta katika undugu kufuatia Elizabeth Michael ‘Lulu’ kupata mkasa wa kifo cha aliyekuwa nyota wa filamu, marehemu Steven Kanumba kilichotokea Aprili 7, 2012.

Lulu alidakwa akihusishwa na kifo hicho na kuswekwa mahabusu mpaka mwaka jana alipoachiwa kwa dhamana na mahakama kuu huku kesi hiyo ikiwa kwenye mchakato wa kuanza kusikilizwa.
Tangu kuachiwa kwa Lulu, Mama Kanumba amekuwa karibu na staa huyo akisahau yaliyotokea. Ukaribu wa Mama Kanumba kwa Lulu ukajikuta ukiunga moja kwa moja kwa mama wa Lulu ambapo wote watangaza wamekuwa ndugu.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"]
mamalulu.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Lucreshia Kalugira[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar, Mama Lulu alisema yeye na Mama Kanumba wanaondoka leo (Jumanne) kwa ndege kwenda Bukoba ambako, mbali na kumuuguza mama mzazi wa Mama Kanumba ‘Bibi Kanumba’, lakini pia wataitumia nafasi hiyo kula kiapo cha kimila ili udugu wao uwe wa damu.
“Tunaondoka Jumanne kwa ndege, tunakwenda Bukoba. Kule kuna kumjulia hali bibi wa Kanumba ambaye anaumwa, lakini pia tutaitumia nafasi hiyo kula kiapo cha kimila ili undugu wangu na Mama Kanumba udumu mpaka kifo,” alisema Mama Lulu.
Kuhusu kuwepo madai kwamba, yeye na Mama Kanumba wapo ndani ya bifu zito, Mama Lulu alikanusha akisema haitatokea.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
“Mimi na Mama Kanumba tuwe na bifu? Haitatokea. Ndiyo maana tumefikia hatua hiyo ya kula kiapo cha kimila,” alisema Mama Lulu.
Kwa mila na desturi za makabila mengi Tanzania, watu wanapopenda kiasi cha kula kiapo kuwa ndugu (yamini) kila mmoja huchanjwa kidole kisha kuunganisha na cha mwenzake huku damu zikitoka.
Baada ya hapo, kila mmoja hunyonya kidole hicho chenye damu tendo ambali huaminika kuwa ndilo huunganisha undugu kuwa kama wa damu. Wazazi hao wote ni wenyeji wa Mkoa wa Kagera.

Stori imedondoshwa kutoka bkuHABARI

Kumbe lulu kafanana na mama akeee
 
afuu huyu mama kanumba tokea mwanae afariki naona kapagawa vibaya mmh!
 
Ina maana huyu mama yake Kanumba tangu alipokuja kwenye wa mwanaye amegandiamo Darisalaam?

Hawa kina mama hasara tupu, yani hapo amekosekana mama yake Wema tu.

mkuu umetukimbia kabisa siasani kulikoni?
 
Ina maana huyu mama yake Kanumba tangu alipokuja kwenye wa mwanaye amegandiamo Darisalaam?

Hawa kina mama hasara tupu, yani hapo amekosekana mama yake Wema tu.

leo ndege bk airport hazijatua kutokana na hali ya hewa aaaaa
 
Ina maana huyu mama yake Kanumba tangu alipokuja kwenye wa mwanaye amegandiamo Darisalaam?

Hawa kina mama hasara tupu, yani hapo amekosekana mama yake Wema tu.

Hahahahaaa umemaliza kila kitu. nimecheka hapo aliekosekana pangenogaje?
 
Ni kweli kabis hawa mama hasara sana, inabidi mama wema, mama lulu na mama kanumba waunde chama chao
 
Ni kweli kabis hawa mama hasara sana, inabidi mama wema, mama lulu na mama kanumba waunde chama chao

Bahati mbaya mama wema si MHAYA, si unawajua wahaya kwa ubaguzi akijiunga watamnyanyapaa balaa, waache waapizane wenyewe wala SENENE hao…!
 
Kweli huyu mama anatafuta umarufu kupitia jina la marehemu mwanae. Mbona kabla kanumba hajafa alikuwa hauzi sura kwenye media hivyo? Hajarudi tu Bukoba? Aende bk akapalilie migomba, au ameonja utamu wa dar?
 
mnaoleta habari zao ndo mnafanya watu wawsfikitie.acheni ukenge kutupotezea mida.
 
Kweli pesa shetani hivi niwaulize wanawake,unaweza kufanya undugu na mtu aliyesababisha kifo cha mwanao wa pekee wa kiume hata kama umemsamehe?hivi huyu mama anajisikiaje akiwa karibu na Lulu?kusamehe kupo lakini huyu ni vihela anavyopewa na Lulu ndo vinamfanya amsahau Kanumba!Samehe then mpotezee usiwe naye karibu unless kama haukua na feelings na mwanao

hata asipomsemee au amsamehe na kumkalia mbali Kanumba hawezi harudi, bora aupe moyo wake amani asahau yote.
 
Back
Top Bottom