Ni sahihi kabisa alikosea kumdanganya, lakini jiulize, Kama alimdanganya zamani, na amekuwa mwema kiasi Cha kufurahia maisha yake, kuondoka kunamsaidia kiasi gani ukilinganisha na kubaki?
Lakini pia jiulize, yeye akiondoka leo, (akiwa na watoto wake 3) ataolewa tena? Au ataishi pasipokuwa na mahusiano mengine mpaka anakufa?
Kama atakuwa na mahusiano mengine, huyo atakayempata atakuwa mwanaume wa aina gani? Mume wa mtu? Au atapata wa kwake peke yake?
Wanawake Kuna wakati wanahitaji kutulia sana kabla ya kuamua, kwa sababu Kuna wakati unaachana na mumeo then unaenda kuwa mchepuko wa mume wa mtu mwingine, unakuwa mtu wa kuonjwa na kila mwanaume coz huwezi kuwa na mume wa mtu maisha yote!
Ni mtazamo wangu tu, wengine sijui watakuwa na mtazamo gani