Huwa hatuachi mwanaume kwa makosa yake ya nyuma, ingekuwa Mimi hata angekuwa na watoto 7 kila mmoja na mama yake, simuachi
Ni sahihi kabisa alikosea kumdanganya, lakini jiulize, Kama alimdanganya zamani, na amekuwa mwema kiasi Cha kufurahia maisha yake, kuondoka kunamsaidia kiasi gani ukilinganisha na kubaki?
Lakini pia jiulize, yeye akiondoka leo, (akiwa na watoto wake 3) ataolewa tena? Au ataishi pasipokuwa na mahusiano mengine mpaka anakufa?
Kama atakuwa na mahusiano mengine, huyo atakayempata atakuwa mwanaume wa aina gani? Mume wa mtu? Au atapata wa kwake peke yake?
Wanawake Kuna wakati wanahitaji kutulia sana kabla ya kuamua, kwa sababu Kuna wakati unaachana na mumeo then unaenda kuwa mchepuko wa mume wa mtu mwingine, unakuwa mtu wa kuonjwa na kila mwanaume coz huwezi kuwa na mume wa mtu maisha yote!
Ni mtazamo wangu tu, wengine sijui watakuwa na mtazamo gani
ameshaombwa msamaha, muungwana akishavuliwa nguo hasimami huchutama and yes kijana amechutama
mbona iko wazi alifichwa isilete shida inauma lakini ukiacha hilo kuna jingine la kuhatarisha ndoa yake lililotokea had aconclude waachane??
asiache mbachao kwa msala upitao, hilo nalo litapita akae alee familia yake na mumewe, asamehe wameshakiri kukosea awasamehe ndio ubinaadam na uungwana huo
halaf hata akisamehe sio kwamba wataganda hapo maisha lazima yatasonga tu muhimu uhai.
Huwa hatuachi mwanaume kwa makosa yake ya nyuma, ingekuwa Mimi hata angekuwa na watoto 7 kila mmoja na mama yake, simuachi
Hapo ni mapicha picha tu. Hakuna ndoa. Aliyeoa ni mume wa mtu nae kaoa mke wa mtu. Vijana wa siku hizi wanakuwa na.watoto wa kila rangi/kabila[emoji23][emoji23][emoji23].
Halafu wanawake wanapenda kuonekana wasafi sana hapo huyo no4 anataka kuonekana hana hatia kuzaa mapema ila mwenzio ndo anahitaji hukumu ya kuza mapema.
Pia huyo mama wa huyo mwanaume nae hakuna mzazi hapo. Toto lako linazaa kama kuku sehemu tofauti tofauti bado unapokea vifaranga vyake bila ya kumkanya au kumwongoza lipi la kufanya.
Sent from my PBAT00 using JamiiForums mobile app
Ikiwa mwanaume amekiri kosa na amekuowa na anakupa furaha you better keep him. Ukiiona dhahabu inangaa shingoni historia yake ilikuwa matopeni.
Ndukiiiii [emoji2089][emoji2089][emoji2089]
huyo rafikio hajakua kiakili, hapo mbona hamna jambo kubwa la kuvunja ndoa? ni bora hao watoto mumewe angewapata kwa siri wakiwa ndoani bt kwa hili akivunja ndoa mbeleni atajuta sana
Naona kama mke wa ndoa yeye ndie anafanya maisha yanakuwa magumu.
Yes ni kweli kudanganywa kunauma hasa kwa watu uliowaamini.laki sasa..si kaombwa msamaha?
Ingekuwa huyo mumewe kazaa hao watoto wa nje akiwa ndoani kweli ningesema huyo mke anahaki ya kulia mda wote huo.sasa mtu aliyafanya yote hayo akiwa hakujui wala kutegemea kukujua halafu unajiliza namna hiyo huo ni upoyoyo aiseh..labda kama kama analia kwa lengo la kusafisha macho hapo sawa aende kulia kwa kiasi ya 5G.
Aiseh baadhi ya wanawake bhana..kuna vitu si vya kuumiza navyokichwa ni kutumia akili tu.
ushauri wangu:
mwambie kama anajiona na kujihisi yeye ni malaika binadamu si kiumbe sahihi kwake,basi aende mbinguni akaishi na malaika wenzake fullstop
Mi naona huyu anasumbuliwa na kuwaza mali ya mwanaume vp kam hao watoto wengine itabid wapate mgao
Ni swala la tamaa za mali
Kwa hiyo na yeye anataka kuongoza single mother wa 4 anyway kastori Kama kanafanana na kastori kangu ila nauhakika yangu ila Mungu ni mkuu itavukwa
Kumbe tuko wengi mi kiukweli sitawaacha wanangu wafanye ujinga niliofanya inaniumiza sana kila siku usiku na mchana nyege za miaka 19-24 na jinsi watoto wakike wanavyoachwa sasa hivi ni hatari sana yaani umekaa zako ghafla kademu wala hamjazoeana kivile anakwambia nataka nije kwako tukae wiki mbili. Kwa umri ule na moto ule yaani akili inawaza showshow wala hujui Mambo ya mtoto wala kitu chochote. Kiukweli changamoto ni kubwa nani hatari sana mtu unamiaka 29 una watoto 7 halafu kila mmoja na mama yake wala hauna connection na hata mmoja sijui hii laana itafutikaje. Mungu turehemu vijana wa leo.
Mwambie aache ufala anacholilia nini sasa,. Afunike yaliyopita wako na ukurasa mpya. Hapo wameona wazazi
Sijaona kosa la mwanaume! Mnisamehe wanawake wenzangu.
Kama hao watoto wote amekuta wamezaliwa, sioni haja ya yeye kujiumiza kwa kulia lia.
Ni ngumu ila ni maumivu yatapita.
Ni kosa ambalo lipo kwa "baadhi" ya wanaume wengi.
Ni kosa ambalo mimi kama mimi litaniumiza kibinaadamu ila katu halitavunja ndoa yangu.
Ni kosa ambalo kiasi fulani litapoteza ile furaha ya kawaida iliyokuwepo kwa muda fulani ila sitaruhusu furaha itoweke daima.
Mume alificha ili kuhofia kutokumpoteza mwanamke anayempenda.
Ameshajua, aumie alieeee ila ahakikishe ndoa inaendelea. Maisha yaendelee
Mama mkwe hana kosa kabisaaa
Tena mwambie aangalie siku wakichoka kumbembeleza watamuacha aamue lolote halafu aje duniani huku akutane na hawa wanaume ambao unagundua mauchafu yao na ndio unakuwa umefungulia mlango wa kukuonesha dhahir madhambi yao mengine