CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 245
- 314
1. Matibabu nje ya nchi kwa gharama za serikali. Haifai kulalamika kuwa jimboni matibabu ni duni wakati unatibiwa nje kwa gharama inayotosha kujenga zahanati yenye vifaa na madawa jimboni kwako. Ni heshima kususia hii huduma yenye ubaguzi na ubadhirifu.
2. Posho na marupurupu bungeni yasiyoendana na hali za wapiga kura. Ni ujuha kudai serikali haijaongeza mishahara wakati unashiriki kujiongezea posho na mafao kila kipindi. Ni dhambi mbunge wa darasa la 7 kujipangia maslahi ya mwezi yanayoweza kulipa madaktari 5 jimboni. Kususia malipo kama haya ni utume.
3. Kutumia ubunge kama sifa ya kukopa kufanya biashara binafsi. Ubunge si wa mtu ni dhamana ya wapiga kura. Kuitumia dhamana kukopa bila kushirikisha wamiliki wa hiyo dhamana sio sahihi.
4. Mfuko wa jimbo. Maendeleo ya jimbo yabaki chini ya bajeti ya Serikali. Mbunge kushiriki kugharamia maendeleo ni kosa kwa kuwa inadhoofisha jukumu la mbunge la kusimamia bajeti. Anajiwekea mazingira ya yeye naye kuhojiwa kuhusu matumizi. Anaweza kusinyaa kama katumia mfuko vibaya.
5. Safari za nje zisizoongeza tija. Hii ni uhujumu hivyo kususia uhujumu ni jambo jema.
6. Viongozi kung'ang'ania ofisini. Kung'ang'ania ofisi ni udikteta unaopaswa kususiwa popote na mfano mzuri ni kususia udikteta ndani ya chama chako. Huwezi kudai kuna udikteta serikalini ilhali udikteta chamani unaokubali.
7. Kutohudhuria vikao vya Bunge au kuvisusia. Bungeni mbunge anawakilisha wapiga kura na sio chama chake. Ni vyema kususa amri yoyote inayokutaka usiwakilishe wapiga kura wako waliokutuma bungeni uwawakilishe. Chama hakihitaji maji, zahanati, shule! Wanaohitaji ni waliokutuma ukawawakilishe bungeni. Ukisusa wanaokosa maji, shule, zahanati ni wapiga kura sio chama chako.
8. Kauli na vitendo vinavyokiuka maadili ya jamii. Kujitenga na kauli au nyendo zenye kushabikia vitendo kama ushoga na usagaji NI muhimu kuliko kukaa kimya kwa kuwa tu wahusika ni wa Chama chako.
9. Kauli za kuhujumu au kuitakia nchi mabaya au kuchochea vurugu. Ni busara kumsusa anayetoa kauli au kutenda matendo ya muelekeo huu. Mathalani ni vyema kujitenga na kauli kama "TUSILAUMIANE", "KITANUKA" , "WATANZANIA PIGANENI" n.k. Mtu huyo anastahili kususiwa. NI vyema kumsusia mtu anayeshabikia ndege ikamatwe maana mtu huyo anaweza kuja kulipua madaraja au kung'oa reli.
10. Ukwepaji Kodi. NI vyema kumsusia yeyote anayekwepa kodi bila kujali ni mwanachama au kiongozi wa chama chako.
Kama wapinzani wetu wangesusa haya nina uhakika wangekubalika kuliko ilivyo sasa. Hata jina "nyumbu" wasingeitwa.
Suseni mambo ya maana tutawaelewa.