Mambo (10) kumi usiyo yajua kuhusu Rais John Pombe Magufuli

Umesahau haya mengine muhimu.
11. Toka amekuwa rais kwa kubebwa na Mkapa, serikali yake imehusika na kupotea kwa watu wengi waliomkosoa kidogo tu.
12. Hana karama ya uongozi, sio msikivu yupo na hasira nyingi
13 Ni mbinafsi, mkabila, mdini, na pia anajichukulia fedha za serikali kama zake. Ana sifa ya kupendelea ndugu zake (Nepotism) hasa kwenye madaraka hata kama hawana qualifications.
15 Haeleweki....Yaani ni kigeugeu.
16 Siyo mkweli, kwa maana ya kuwa ni muongo sana.
17 Anasikiliza hearsay bila kuwa na ushahidi na anadanganyika kirahisi.
18 Hana sifa za kuwa rais..........
 
Ahsante kwa mawazo yako mkuu.
 
18 Lakini ni Rais wa Tanzania na Kuna uwezekano wa kushinda tena urais kwa Mara nyingine.

17 Amedanganyika kwenye lipi toa mfano hai usio na shaka.

16 Toa mfano wa angalau vitu vinne alivyo danganya ( visiwe vya kisera ama ilani ya uchaguzi mana anaweza kuwa ameahidi Ila mabadiliko ya sera ama budget isitoshe kutekeleza kila ahadi)

15 Ukigeu geu wake ni katika yepi, lete ushahidi tuone Kama vinahusiana na huo ukigeu geu, isije kuwa ni kubadili kwake mawazo kwa kuvishitukia baadhi ya vitu kuwa havina tija ndopo wewe akatafsiri kuwa ni kigeu geu.

14 Ni ndugu yake yupi aliye mteua bili kuwa na Qualifications na ufanisi wake wa kazi huko alikoteuliwa hadi sasa ukoje?
Ukabila na udini ni kitu kisicho na ushahidi kwake au labda wewe ulete huo ushadi unao mtuhumu nao katika hayo.
Si mbinafsi hata kidogo bali mtu mwenye msimamo juu ya nini anakiamiani bila kuyumbishwa.

13 Karama ya Uongozi si kuwa mpole tu kwenye kila kitu bali ukali ni kitu muhumu hasa ukigundua kuwa nyakati na mazingira ya kiongozi ulio nayo hayahitaji upole bali ukali na misimamo mikali ndio njia sasa. Mfano issues za Madawa ya kulevya, Vyeti fake na watumishi hewa, mafisadi, watumishi wazembe serikalini, mgogoro wa Kenya unao endelea n.k vitu Kama hivi havihitaji upole ndio manaviongozi wapole walio mtangulia viliwashinda.
Yote kwa yote mapungufu lazima yawepo kwa kiongozi yoyote yule mfano kwenye issue ya korosho kulikuwa na mapungufu.

12 una ushahidi upi kuwa hao watu walio potea ni yeye ndio kahusika? Wewe ukigombana na jirani yako Kisha asubuhi akipotea vipi tuseme moja kwa moja bila ushahidi kuwa ni wewe ndio muhusika?
Kupotea kwa watu, vifo vya utata na utekaji sio kitu kigeni katika nchi hii.
Kifo Cha Chacha wangwe, Mwangosi, kutekwa na kupigwa na kwa Dr Ulimboka navyo alikuwa ni yeye kahusika
?
 
Shambulio la Lisu hapo inakaaje? Au niko nje ya mada?
Kama utakuwa na ushahidi kuwa yeye ndio kashambulia huyo Lissu basi waka hapa itakuwa ni ndani ya mada mkuu.
 
Alisema alienda misiri alienda kwa usafiri upi?
 
Kama utakuwa na ushahidi kuwa yeye ndio kashambulia huyo Lissu basi waka hapa itakuwa ni ndani ya mada mkuu.

Ushahidi kisha upelekwe taasisi gani hapa nchini?
 
pia alitangaza kumwozesha mama yake kwa mahari ya kuku jogoo.
 
Ushahidi kisha upelekwe taasisi gani hapa nchini?
Hizo nyingine ni potojo tunachotaka si maneno maneno bali weka ushahidi Kwanza alafu hayo ya mahakama ni baada usitulazimishe unachokiamini wewe ndio kiwe sahihi kwetu.
 
Hizo nyingine ni potojo tunachotaka si maneno maneno bali weka ushahidi Kwanza alafu hayo ya mahakama ni baada usitulazimishe unachokiamini wewe ndio kiwe sahihi kwetu.

Nani anayekulazimisha. Hakuna mtu yoyote anayekulazimisha, bali habari ndio hiyo.
 
Tumbo linapotumika kuliko ubongo, M. Ayo na we unataka uteuzi, tumeyaona kwa Hassan Tumba, tukayaona kwa Magulugulu Machembe, kaza spana wako wengi kwenye foleni ya kutumbuliwa utapata nafasi.
 
Nani anayekulazimisha. Hakuna mtu yoyote anayekulazimisha, bali habari ndio hiyo.
Hiyo haiwezi kuwa habari bila ushahidi badala yake itakuwa ni njia ya kutafutia huruma tu kwa watanzania basi, hamna kitu hapo
 
Hiyo haiwezi kuwa habari bila ushahidi badala yake itakuwa ni njia ya kutafutia huruma tu kwa watanzania basi, hamna kitu hapo

Nimekuambia ushahidi kisha uupeleke wapi, labda nje ya nchi, ila sio kwa hawa hawa wahusika fullstop.
 
Nimekuambia ushahidi kisha uupeleke wapi, labda nje ya nchi, ila sio kwa hawa hawa wahusika fullstop.
Nimekwambia Cha Kwanza ni ushahidi uwekwe wazi Kwanza Kama unao na si kumtuhumu mtu kwa mihemko, we Kama una ushahidi weka hapa na Kama huna basi hahusiki huyo.
 
Eti JK mwanajeshi na Pinda kachero wamuogope mtu ambaye hajawahi kuwa hata kuruta.
Hao walikuwa na mamlaka hata ya kumpoteza wangeamua
 
Dah hivi kumbe magufuli hapendwi hivi?
 
Napenda misimamo yake akiamulia Jambo lazima alitimize bila mashaka yoyote, Ila hyo number Tisa na kumi imenifuraisha jinsi alivo wapa displine hao vijana wasiojielewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…