Mambo 10 yakujua kabla ya kuingia kwenye huu mfumo wa biashara unaolipa kuliko mifumo yote

Dream big

Member
Joined
Jun 18, 2014
Posts
68
Reaction score
14
UTANGULIZI
Kwanza kabisa nitoe angalizo vyote nitavyo viongea kwenye thread hii sijalenga kampuni yeyote(ndio maana sitotaja jina kabisa la kampuni yeyote) bali huu ni uchunguzi binafsi nilio ufanya ndani ya miaka mitatu na niliouandikia na kitabu na ninatoa ushauri huu kuwasaidia watu kupata yale wanayo fichwa kwenye semina nyingi za networking market ili kupunguza maumivu yasiyo na lazima na hasara inayoweza kuepukika mapema.
Biashara ya mtandao ni biashara inayo lipa watu kutokana na kueneza habari kuhusu bidhaa au huduma flani,na kuendelea kulipwa pale waliowaalika wakiendelea kuwafahamisha wenzao kuhusu bidhaa husika wakazitumia
Natumai wengi wao sio neno geni kwani kwasasa ndo imeshika kasi duniani.
Ila unazijua changamoto zake?
Twende taratibu hatua kwa hatua tuziangalie changamoto zenyewe,
CHANGAMOTO

1.Kuna changamoto ya bei,tumeona makampuni mengi ya kiuza bidhaa zao kwa bei kubwa kiasi kwamba mtu wa kipato cha kati na chini anashindwa kuwekeza,kwanini kwanza hizo bidhaa atamuuzia nani?kwa bei husika haswa ukizingatia na maisha yetu sisi watanzania wengi ni ya kipato cha kati,

2.Masharti ya kununua bidhaa zao ili kutimiza point flani uweze kulipwa kwa mwezi husika,hili nalo limekuwa kikwazo kikubwa cha watu kuwekeza nilipata kuambiwa na ndugu yangu aliejiunga kwenye biashara flani ya mtandao kwa lengo la kujiingizia kipato ila akakuta kila kukicha analazimika kununua bidhaa nyingi asizo na matumizi nazo ilimradi tu atimize sharti

3.Wanao faidika zaidi ni wale tu wanao jishuhulisha kwa mwezi husika bila kujali jitihada mtu alizo zifanya kwa miezi ya nyuma kuingiza watu,hii hufanya wengi washindwe kwani miezi ya kibiashara haifanani kuna mingine inakua mizuri na mingine migumu,na kumbuka hii ni biashara kama biashara nyingine

4.Hakuna sera nzuri za kuwa reward leaders,Hivi ulisha jiuliza kwanini watu wanazidi kupungua pale level za uongozi zina zidi kupanda,mimi nina mtu ninaye mjua ambaye tangia miaka mitatu ilio pita yuko kwenye level hiyo hiyo ya umeneja na,kuna changamoto kubwa hapo wanayo waficha ikiwemo ugumu wa kufikia level flani n.k
5.Watu wanao waalika wengi wana base kwenye kumpata mtu na kumuingiza(recruiter) na sio kumuelekeza vya
kutosha mtu faida na hasara za biashara husika(coaching)

6.Watu wengi wanao jiingiza matarajio yao ni kupata fedha ya haraka na hii ni kutokana na semina wanazopewa kunakishiwa na faida kubwa kubwa mtu atazo weza kupata pale atakapo jiunga na biashara husika kama magari nyumba za kifahari na tripu za kila kipindi bila kuonyesha ni njia gani mtu anaweza kupita kufikia huko,

7.Kutokutajiwa bei ya bidhaa moja baada ya nyingine kwenye semina,hii ni mbaya kuwaeleza watu umuhimu wa bidhaa ni hatua moja ila haswa kuhusu bei ya bidhaa moja moja ndio jambo zuri zaidi,Mfano kipindi nilipata fursa ya kuhudhuria semina ya kampuni flani,nilipata kujua kuhusu dawa ya mswaki ila ki uhalisia sikujua inauzwa shilingi ngapi ambako kiuhalisia hilo lilitakiwa lipewe kipaumbele baada ya kufanya uchunguzi wangu mwenyewe nikaja kugundua dawa ile inauzwa T.sh 15,000/,embu angalia kama ni mtu alitaka kununua kwa kuuza angehasiriwa kiasi gani

8. Watu kutembeza bidhaa kama wamachinga,nilijisikia aibu sana nilipo ambiwa kuna maprofesa wameacha kazi na wanatembeza bidhaa mtaani kama wasiosoma,iko wapi thamani ya proffesional zetu kama ndo hivo?

9. Kuwepo na bidhaa zinazazo fanya kazi kama hizo zinazo tangazwa kwa bei ndogo(substute)na hizo nyingine zinazo kuja zinaonekana kama zina jaribu kujionyesha kuwa na sisi tuko(me too product),mfano biashara nyingi za mtandao kwasasa nchini zinadili dili na bidhaa zisizo na kemikali ukiangalia kwasasa nchini makampuni mengi yamekwisha ibuka yenye bidhaa kama hizo tena kwa bei poa

10.Ni biashara unayo fanya siku nzima na sio muda wa ziada,kiukweli kwenye biashara nyingi za mtandao zilizoko nnchini ukitaka ufanikiwe lazima utumie muda mwingi ukijishuhulisha nayo,tuchukue mfano rahisi inawezekanaje kupata wateja wanao taka kununua bidhaa za afya bila kuwa na mizunguko mirefu ya kuwatafuta,pia mzunguko huwa mrefu zaidi kutokana na bei husika

Wadau naomba niyatoe tu hayo machache ila yako mengi sana hata nyie mwaweza kuendelea kuyatoa chini ili tuwasaidie watanzania


SULUHISHO LA CHANGAMOTO TAJWA HAPO JUU:

SULUHISHO LA JUMLA

Kiukweli wadau suluhisho kubwa la changamoto tajwa hapo juu ni mtu kuwa makini na kufanya uchunguzi wa kutosha kwa kupitia changamoto tajwa hapo juu.
Kumbuka biashara ya mtandao ni kama biashara nyingine sio kila mtu anaweza kufanya.
"SOMETIME IN LIFE IS NOW OR NEVER"
 
mambo ya Gnld, forever living, oil frame ,na mengnee skuiz yanawadakaa wanafunz wa vyuooo balaha

kuna rafiki zangu wananisumbua ile mbaya hapa Dodoma.
Hadi kupokea calls zao naogopa.
 
Umeeleza vyema sana mkuu.. tutakutafuta InshaAllah
 
kuna rafiki zangu wananisumbua ile mbaya hapa Dodoma.
Hadi kupokea calls zao naogopa.
Pole sana mdau,ila wanalazimika kufanya hivyo sababu ya hivyo nilivyo taja hapo juu,wasipotimiza idadi flani kwa mwezi husika hawalipwi so unakuta mtu anazunguka na mwezi unakaribia kuisha hajafikia lengo inakuwa ni usumbufu na hiyo sio nzuri kwani sheria kuu ya biashara ya mtandao ni lazima kwanza unayetaka kumwambia kuhusu fursa husika awe na interest nacho kwani mtu akifanya kitu bila kuwa na interest nacho mara nyingi matokeo yake huwa afifu au hayatokei kabisa,hapo ndiko uadui unako anzia.Nategemea umakini utaongezeka sana kwa sasa kwenye hilo
Stay blessed
 
Mkuu nadhani suluhiaho la kutafuta watu WA kuwauzia product Ni kutumia online marketing sababu unaweza fanya biashara world wide
 
nilikuwa sifahamu vizuri mkuu umenifumbua macho sana na nimeelewa vilivyo hapa

asante sana kwa huu uzi best
 
Mkuu nadhani suluhiaho la kutafuta watu WA kuwauzia product Ni kutumia online marketing sababu unaweza fanya biashara world wide

Ni kweli japo chalenge is still there,unatumia online marketing kwa offline product,ingekuwa super sana kama vyote viwili vingeenda kwasambamba as the U.SA ndo mfumo mpya wa networking wanao utumia
 
Nimekusoma mkuu,mimi nataka kujua wewe unauza product gani?kwani haiwezekani mimi kununua kwa matumizi binafsi?
 
Inavutia, Ila sasa kama ilivyo kanuni ya msumeno, Nidondoshee changamoto zilizopo kwenye hiyo biashara yako nipime kama naweza kukutafuta ama lah, Na pili, dadavua; nafaidikaje tofauti na huko kwingine?
 
Nimekusoma mkuu,mimi nataka kujua wewe unauza product gani?kwani haiwezekani mimi kununua kwa matumizi binafsi?

Bidha ziko kwenye mfumo Wa kudownloadiwa ni software
Ndio inawezekana kutumiwa kwa matumizi binafsi
Maelezo zaidi;0712223052
 
Inavutia, Ila sasa kama ilivyo kanuni ya msumeno, Nidondoshee changamoto zilizopo kwenye hiyo biashara yako nipime kama naweza kukutafuta ama lah, Na pili, dadavua; nafaidikaje tofauti na huko kwingine?

Kama nilivyotangulia kusema hii biashara imetatua changamoto zote tajwa hapo juu,ila changamoto iliyo baki ni changamoto ya mtu binafsi ya uoga,ambayo hichi ndicho kinacho kwamisha watu wengi kusonga mbele,Uoga wa kushindwa ni mkubwa kuliko shauku ya faida watayo ipata baada ya kufanikiwa kwao,na hili limesha tatuliwa na kampuni imesema wazi iwapo mtu hatorizika na mfumo huu wa biashara basi atarudishiwa fedha yake mara moja aliyo lipa,ila pia kwa mwezi huu wa tisa nimetangaza wazi watakao weza kuniletea watu watatu wakajiunga chini yangu mtu huyo mimi namlipia gharama zote za kujiunga
PILI:faida ziko nyingi kwani hii ni biashara pekee ya mtandao yenye malipo tofauti tofauti ya aina saba,nikimaanisha kwa kila mtu mmoja unaemwingiza unalipwa mara saba,cha kushangaza ni kila mwezi na siyo tu kwa utao waingiza bali wale watao ingizwa na watu wako pia,Pia ukisha lipa mara moja ukaingiza watu watatu hutakaa ulipie tena milele
aise ziko nyingi sana mdau,ndo maana nikasema nimeandikia kitabu na mpaka uelewe ndipo utapo ingia,
Karibu tukufundishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…