FAJES
JF-Expert Member
- Oct 29, 2017
- 720
- 644
Wakuu, heshima kwenu.!
Kama ilivyo ada, JF ni kisima cha habari, stories, ucheshi na mengineyo. Ili kuifanya JF iendelee kuwa kisima cha taarifa, naomba nami leo ku-share mawili matatu kuhusu mada tajwa hapo juu.
1) Kwa muda wote niliopo huku, miaka mitatu sasa, nimesafiri na kutembea maeneo mbalimbali. Safari za muda mrefu na fupi. Kwakweli sijawahi kushuhudia ajali ya barabarani. Simanishi kuwa ajali hazipo kabisa, ila ni kwa kiwango kidogo sana. Kwa mujibu wa utafiti wangu mfupi usio rasmi, nimegundua hii inatokana na sababu zifuatazo,
i) Leseni za udereva zinatolewa kwa njia ambayo ipo high secured. Yaani hata kama una leseni ya bongo, na una experience ya kuendesha kwa miaka 10, lazima ufanyiwe majaribio kabla ya kupewa leseni ya huku. Endapo utakosea hata kosa moja tu wakati wa majaribio, mfano kuchelewa kuwasha indicator kabla ya kukata kona, au ukaendesha gari huku umeegesha mkono dirishani kama ifanyikavyo bongo, hakika hautapewa leseni na inabidi urudie tena majaribio. Aidha, leseni mpya zinatolewa kwa mafunzo ambayo lazima uwe very compentent. Kwa ufupi wakuu ni kwamba, leseni hazitolewi kama njugu.
ii) Ikibainika umeendesha gari huku umekunywa pombe kwa kiasi kisichoruhusiwa, fine yake inaweza kukaribia nusu ya kipato chako cha mwezi. Kuna baadhi ya magari, hususan magari ya makampuni, ili uweze kuliendesha, lazima ufanye test ya kucheki kama umekunywa pombe. Usipofanya hiyo test ambayo ipo kwenye mfumo wa gari, hiyo gari haitoondoka wala kuwaka.
iii) Magari yote yanayotembea barabarani lazima yakaguliwe kila mwaka ili kujua kama bado yanakidhi vigezo vya kuwa barabarani.
iv) Njia nyingi hasa high way, ni one-way. Hizi ni barabara hasa zinazotoka mji mmoja kwenda mwingine. Baadhi ya miji, hata barabara za ndani zina mfumo huu. Yaani magari yanayoenda upande mmoja hayakutani na yanayokuja upande mwingine. Madereva wanafahamu nachomaanisha.
v) Barabara zina standard kiwango cha juu. Yaani ikitokea uharibifu tu mahala, haraka sana inafanyiwa marekebisho.
2) Kwa muda wa miaka mitatu sasa, tangu niwepo huku (Sweden na Uholanzi), hakuna hata sekunde moja ambapo umeme na maji vimekatika. Hebu imagine huko Kilosa, Ileje, Nyapande, Nkasi, Ludewa, Liwale, Ngara, Uvinza, Makete kuwe na access ya umeme na maji ndani ya nyumba 24 hours/7 days. Maisha yangekuwaje? Raha si raha? Ha ha haa.!
3) Intrnent ni huduma muhimu kwa kila nyumba kama ilivyo umeme na maji. Namanisha kuwa, kila nyumba imeungunishiwa mfumo wa kupata internet.
4) Huduma za Elimu na Afya kwa Sweden ni bure kuanzia vidudu hadi University. Elimu kwa Uholanzi (Kwa chuo) unalipia kidogo, ila siyo gharama kubwa kivile.
5) Sweden ukiwa mgonjwa ukapelekwa hosp unapatiwa na huduma ya chakula. Ni bure, haulipii. Muhimu uwe mkazi au raia. Pesa zinatoka kwenye Tax unayolipa. Hapa ndipo kuna hoja kwamba, wanalipa Tax kubwa, mfano kwenye mji ambao huwa naishi, Tax ni almost 30% ya kipato chako.
5) Shughuli zote zimewekwa kwenye mfumo rasmi chini ya makampuni. Kwa ufupi hakuna eti ile kusema hii kazi i.e anapewa fundi locally na kuanza kujenga kwa kuwatafuta vibarua mtaani kienyeji. Namanisha kuwa, kila kazi, iwe ni kupanda maua, kupaka rangi, usafi, kusafisha vioo kwenye majumba n.k zipo kwenye mfumo rasmi. Na kila anayefanya kazi anaajiriwa katika mfumo rasmi. Nadhani hii njia inafanya hizi nchi za wenzetu kila mtu kuhakikisha analipa kodi.
6) Kila anayeajiriwa, hata iwe non-professional job, kwa kiasi kikubwa, mshahara anaolipwa mtu unamwezesha kukidhi maisha katika standard ya kawaida. Yaani anaweza kula chakula, kulipia rent, usafiri, n.k kwa mwezi mzima na akabakisha chenji kidogo. Nasisitiza kuwa ni kwa kiasi kikubwa, kulingana na uexperience niliyonayo. Huenda kuna baadhi ya kazi (zitakuwa chache sana) mtu anaweeza kulipwa below the standard. Wenzetu wana standard za mishahara kwa nchi nzima. Siyo kila mtu kujipangia tu.
7) Train na mabasi ya Public ndani na nje ya mji yana ratiba zinazofahamika. Mfano, kila baada ya robo saa gari inapita kwenye kituo. Kuwe na abiria ama hakuna abiria muda ukifika basi lazima liondoke/kusafiri kama ilivyopangwa. Hii ni kwa sababu, Serikali ina- provide subsdy kwenye sekta za usafiri. Kwahiyo kama kampuni itapata hasara, serikali inafanya ku-top up ili sekta hiyo iendelee ku-survive.
8) Hakuna masuala ya mfanyakazi wa ndani kumuangalia mtoto ama mtu mzee kama bongo. Hii ni kwa sababu, mama akijifungua, mama anapewa maternity leave na baba anapewa partenity leave ambapo kwa ujumla wake vikichanganywa inafikia mwaka mmoja. Hivyo mtoto atalelewa na wazazi mpaka afikishe mwaka mmoja. Baada ya hapo anapelekwa kwenye baby care center ambako anapelekwa asubuhi na kuchulkuliwa mchana. Kwa Wazee, akishafikisha umri wa kutojiweza, anapelekwa kuhudumiwa kwenye community center ambako pension yake itatumika kumuhudumia.
9) Kiwango cha ukosefu wa ajira ni kiasi kidogo sana. Yaani si rahisi kukuta mkazi yupo home muda mrefu bila kazi yoyote. Sisemi kuwa hakuna wasiokuwa na ajira, ila ni kwa kiasi kidogo sana. Suala la gharama za maisha ni jukumu la baba na mama. Sio kama sisi eti kazi ya kutafuta mahitaji ni suala la baba peke yake. Huku suala la usawa linafanyika kwa vitendo. Hii mada ya usawa nitaijadili siku nyingine.
10) Pamoja na kodi kubwa wanayokatwa (atleast 30%), ila jamaa wanafaidi sana kodi yao. Yaani unakuta Serikali inampatia mzazi kiasi flani cha pesa kwa ajili ya huduma ya mtoto anapozaliwa mpaka anapokuwa mkubwa. Ha ha haa. Kwa lugha fupi ni kuwa, kila mtoto analipwa kiasi flani cha pesa mpaka afikishe umri mkubwa. Siyo kiasi kikubwa, ila kinamwezesha kuishi.
Kwa leo naomba niishiea hapa. Leo nimezungumzia upande wa +ve side, siku nyingine nitazungumzia -ve side pia. Haya niliyosema simanishi kuwa nchi za Ulaya wanaishi kama Mbinguni, na kwenyewe kuna shida zake nyingi tu.
Kama kuna mahala nimeteleza kidogo, basi ni sahihi kukosolewa na kurekebisha jambo ambalo naweza kuwa nime-overlook. Ila nilichokisema kina uhalisia mkubwa zaidi ya 90% maana ni mambo niliyoyaona na kusimuliwa.
NB: Siasa za huku kwa kiasi kikubwa, zimejikita kwenye sera za kupunguza wahamiaji ( Yaani malalamiko kuwa wahamiaji ni wengi yamekuwa makubwa sana miongoni mwa raia). Siasa nyingine zimejikitia kwenye masuala ya mabadilkiko ya Tabia ya nchi (Climate change). Yaani sisi Afrika tukiwa tunataka labda kuandamana kwa ajili ya kupatiwa huduma za msingi za maisha, huku wenzetu wameanza kuandamana kushinikiza Serikali zao zichukuwe hatua dhidi ya Mabadiliko ya Tabia ya Nchi . Naomba hii iwe mada ya siku nyingine pia.
Ahsanteni.