Mambo 10 yaliyopo Ulaya, hasa hasa Sweden, pengine kwako ni mageni, na ungependa kuyafahamu

Uwe na sababu za kufika kwanza. Sababu zipo nyingi. Masomo, tourist, kikazi, biashara n.k. Katika hizo sababu unaweza ipi?

Hapo ni kuja kibiashara kwanza kuchukua vitu used vya huko kama tv, fridge, na kadhalika unakuja bongo kupiga pesa tu maana bongo hata vyombo vya ndani used twende kazi tena ukitangaza umetoa ulaya vinaisha haraka sana
 
Uwe na sababu za kufika kwanza. Sababu zipo nyingi. Masomo, tourist, kikazi, biashara n.k. Katika hizo sababu unaweza ipi?
Kwenda tuul kutafuta maisha.
Ujue vijana wengi hatujui tunataka kwenda nje kutafuta Nini.
Yaani mtu atajua huko huko ili mradi katoka
 
Hapo ni kuja kibiashara kwanza kuchukua vitu used vya huko kama tv, fridge, na kadhalika unakuja bongo kupiga pesa tu maana bongo hata vyombo vya ndani used twende kazi tena ukitangaza umetoa ulaya vinaisha haraka sana
Hii aina ya baishara inabidi utafiti wa muda. Kubaini aina ya bidhaa specifically na uingizwaji wake ndani ya nchi. Namanisha masuala ya kodi n.k Mfano, nimwahi kufatilia kuhusu biashara ya used furniture, niliponda TRA nikagundua unaweza kupata hasara, maana sera ya kodi kwa furniture kwa mtizamo wangu ni kama inalinda bidhaa za ndani hivyo kodi yake nikaona ni kubwa. Kingine, hizi bidhaa used siyo kwamba utazitukua sehemu moja kwa kiwango unachotaka. Inaweza kukuchukuwa muda mrefu kukusanya mzigo wa kutosha maana inakubidi kukusanya kimoja kimoja kulingana na upatikanaji wake huko kwenye maduka used.
 

Machine machine used unaweza ukapiga bingo kikubwa kama usemavo utafiti uwe wa kutosha kabisa
 
Waliojanjaruka mapema walisafiri hadi uholanzi kuchukua baiskeli used kwa sasa wako mbali sisi tukua tunategemea mzee wetu magu atuvushe
 
Kwenda tuul kutafuta maisha.
Ujue vijana wengi hatujui tunataka kwenda nje kutafuta Nini.
Yaani mtu atajua huko huko ili mradi katoka
Kutokana na sera ya uhamiaji siku hizi, hali imebadilika Ulaya siyo kama zamani. Wenyeji wanaona kuna kipindi serikali zao ziliruhusu wahamiaji kwa kiwango kikubwa na madhara yake yameanza kujitokeza. Mafano, matukio mengi kuhusu criminal issues zinachangiwa sana na wahamiaji. Sisi watu wa kuja tunakuja na tamaduni zetu na kuharibu ustaarabu wa wnzetu na kusababisha shida. Kwahiyo uzamiaji kwa sasa si rahisi sana. Ila nisikukatishe tamaa. Kila jambo chini ya jua linawezekana. Kama unataka kutafuta maisha, nakushauri ujaribu ku-focus Uingireza, huko hutapata taabu ya lugha na kazi za vibarua ni nyingi zaidi. Huku kwingine kama Sweden utapata shida mpaka kwanza ujifunze lugha. KJazi za kuzungumza English ni chache. Wakazi wanazungumza English vizuri kabisa, ila wanalinda sana tamaduni zao including language.
 
Mpe connection ya jimama moja lugha atamfundisha huyohuyo.

Halafu zile mchongo za Au pair siku hizi Sweden hazipo?
 
Mambo ya ulimwengu uliostaarabika
 
Bongo maisha hayo wanaishi viongozi na familia zao pamoja na kikundi cha wateule wachache huku wananchi wanaolalamika wanaishia kuwauwa, kutekwa na wasiojulikana,kukashifiwa kwa matusi na masimango ya kila aina lakini cha ajabu wengine ndio wanawasifu hao watesi wao na kutaka wawe watawala wa milele na kudai hivyo ndivyo inavyostahili kuongoza Wabongo na kwamba eti Mbongo ukimchekea mambo hayaendi!
 
Sweden hawaruhusu kusafirisha fridge kwa sababu fridge nyingi za zamani zinatumia gas inayoitwa refrigrant R 116 ambayo inaharibu mazingira.Na wao kama Serikali hawaoni ni sawa morally kuziruhusu na kupeleka tatizo kwingine duniani. Fridge mpya zinatumia gas inayoitwa isubotane.Hizi ni ruhsa kusafirisha.
Kuhusu mambo mengine aliyosema mleta mada karibu yote ameelezea ukweli.Isipokuwa mishahara inasimamiwa na mkataba unaoitwa kollektivavtal. Mkataba huu unasimamia mishahara ya sekta zote hata binafsi ili kulinda wafanyakazi wasipunjwe na kupewa mishahara isiyokidhi mahitaji ya mfanyakazi.Kila sekta ipo huru kutoa mishahara zaidi ya mkataba lakini sio pungufu.
Kila mwaka waajiri wanakutana na wafanyakazi wao katika kikao kinachoitwa medarbetare samtal ili kuzungumzia ajira yao na kuongeza mishahara kutokana na wajibu wao kazini.Kuhusu lugha inafundishika kama nia ipo.Ukiwa na bidii ndani ya miezi 6 unakuwa umejifunza svenska(lugha ya kiswidish) kwa kiwango cha kueleweka.
 
Hamna lolote. Simulizi za kawaida za Watanzsnia Wasafisha vyoo mchana na Wasambazaji magazeti nyumba hadi nyumba asubuhi saa 9 usiku kila siku. Wameridhika na maisha ya milele ya kuwa vijakazi wa Wazungu.
 
Hamna lolote. Simulizi za kawaida za Watanzsnia Wasafisha vyoo mchana na Wasambazaji magazeti nyumba hadi nyumba asubuhi saa 9 usiku kila siku. Wameridhika na maisha ya milele ya kuwa vijakazi wa Wazungu.
Well kati ya hao wasafisha vyoo ulaya na wanapata kipato na kuishi kama binadamu anavyotakiwa kuishi, na hawa waliojichokea Bongo mpaka uchawa imekuwa ajira bora nani?

Ujuwe nilikuwa nakuonaga kama mtu muelewa na mwenye exposure kubwa kumbe sivyo,

Kwahiyo unataka kila mtu awe mwizi kama wewe mpaka viwango vya kusakwa na FBI?

Taarifa zako tunazo mtumishi, acha dharau.
 
Hamna lolote. Simulizi za kawaida za Watanzsnia Wasafisha vyoo mchana na Wasambazaji magazeti nyumba hadi nyumba asubuhi saa 9 usiku kila siku. Wameridhika na maisha ya milele ya kuwa vijakazi wa Wazungu.
Bora huko huo mshahara naweza kulisha familia na kutuma hela huku tz kwa ndugu na jamaa zake..niambie huyo msafisha choo wa tz ana maisha gani?

Tanzania ni nchi ya laana kuanzia viongozi wake.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi yetu wenyewe hatujamaliza tunaanza kushobokea mambo ya sweden.
 
Mkuu Matola. Well said.
 
Taratibu mkuu
 
Mpe connection ya jimama moja lugha atamfundisha huyohuyo.

Halafu zile mchongo za Au pair siku hizi Sweden hazipo?
Au pair Mkuu sina ufahamu nayo.

Mkuu, najuwa wewe ni senior kwenye masuala ya nchi za Ng'ambo kutokana na utafiti wangu humu JF. Ila mKuu siku hizi Sweden mambo yamebadilika, hata hiyo ya kutafuta ji-Mama siyo rahisi kama zamani. Yaani sera kuhusu wahamiaji zinaendelea kubanwa siku hadi siku. Hata ukipata mchumba, kwa sasa hupewi uraia mpaka huyo mchumba wako naye aje kwenu na kipindi cha kuomba ukazi urudi kwenu kwanza.
 
Sheria hiyo ya kuomba ukazi kwa kupata mke au mume anhörig invandring haijabadilishwa sana.Kilichoongezeka ni kwamba ukipata mchumba mume au mke ni lazima uwe na kipato cha kuwatosheleza na makazi.Sharti halikuwepo mwanzoni.Kuomba ukazi unafanya ukiwa nyumbani.Migrationsverket hawapokei maombi ukiwa Sweden.Maombi yanafanyika kwenye ubalozi wa Sweden Tanzania. Migrationsverket(Idara ya Uhamiaji) wanapokea maombi yako kutoka ubalozini.Interview unafanyia ubalozini.Sharti muhimu ni lazima uwe na passport kabla ya interview kurahisisha mchakato.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…