Mambo 10 yaliyopo Ulaya, hasa hasa Sweden, pengine kwako ni mageni, na ungependa kuyafahamu

FAJES Mbona hujawaambia kwamba mtoto unapompeleka mtoto dagis (daycare) unampeleka yeye tu kama yeye, labda na kanguo ka kumbadilisha tu ila mahitaji yake mengi yooooote mpaka diapers atapata huko huko?
 
Inaitwa Red light street
 
Wenzetu wanaishi sisi tunasurvive
 
Siku za mwanzo jambo la kwanza kabisa lililonishangaza ni kuona namna wasichana wanavuta sigara kwa kiasi kikubwa. Nikadhani baridi inachangia ila naona imekuwa kama culture. Pombe pia wanapiga si mchezo. Japo si za kulewa. Uzuri Mkuu, kwa Sweden huwezi kununua pombe kama unavyopenda. Kuna maduka maalumu ya kununua pombe. Nadhani wangeacha iwe huru nguvu kazi ingeathirika sana kwa watu kunywa pombe na kushindwa kufanya kazi.

Kuhusu Sex mkuu naona pia ni kama culture sasa. Yaani wao wanafundishwa masuala ya reproductive health wakiwa bado wadogo. Hii ina advantages na disadvantages pia. Ndio maana kufanya abortion ni legal na haki ya mwanamke hata bila ridhaa ya Mzazi au Mpenzi wake. Maana huwezi kumuona binti mdogo mjauzito. Nadhani abortion na exposure ya early reproductive health vinawasaidia sana. Lasivyo kungekuwa na mimba nyingi za utotoni.
 
FAJES Mbona hujawaambia kwamba mtoto unapompeleka mtoto dagis (daycare) unampeleka yeye tu kama yeye, labda na kanguo ka kumbadilisha tu ila mahitaji yake mengi yooooote mpaka diapers atapata huko huko?
Mkuu ujue huwa nikisoma comments nyingi huko Quora wanapasifia sana Sweden kwa kuwa na system bora zaidi Duniani ya kulea mtoto na maternity + peternity leave. Ila kwakweli wapo juu sana. Yaani unazaa mtoto unapewa pesa na Serikali za kumtunza mtoto mpaka anakuwa mkubwa. Duh. Japo kodi ni kubwa ila wananufaika sana. Ndio maana Waarabu wa Asia, Wasomalia, Ethiopians na Eritreans wanachangamkia fursa hiyo. Unakuta wanazaa watoto wengi mpaka inakuwa tishio kwa wazawa wenye nchi yao. H aha haaa.
 
Mbona ndugu zetu Wasomali hujawataja?😁😁
Yani hayo mataifa wamefanya kuzaa kama mtaji. Hawajihangaishi kusoma hata SFI tu wala kutafuta kazi. Wanasubiria hela za social na monthly allowance za watoto.😏

Tukirudi kwenye issue ya watoto (kuanzia maternity/paternity leave, daycare, shule etc)na kama mmoja wa watu waliofaidi hiyo system kama mtoto na kama mzazi, acha tu wasifiwe kwasababu they deserve it!!! Na kodi wakate tu maana social services zote zinazotolewa na serikali ni FIRST CLASS. Hakuna longolongo wala ubabaishaji.
 
Umenikumbusha kitu mkuu. Ile kitu nyingine inaitwa tax return. Nyinyi wenye kazi za kudumu na uhakika wa kuishi Sweden on permanent basis unaweza usiielewe vizuri hii kitu faida yake maana mnapata return kidogo huenda isifike hata 1000kr. Ila ukifanya kazi za vibarua na ukawa hauna kazi ya permanent unaweza kupata tax return hadi 20,000 kr. Kwakweli Wazungu acha waitwe Wazungu tu. Japo ssi Waafrika tunawarushia sana mawe Wazungu ila mie huwa naita hizo ni chuki binafsi na athari za kung'ang'ania historia za ukoloni tu. Ila jamaa wapo mbali sana kwenye systems za kuendesha maisha ya mwanadamu, ukiachana na changamoto za hapa na pale.
 
Huko kuzuri kuishi binadamu
 
taratibu kaka karibu sweden tubebe boksi, huku Kalmar kamji kadogo kusini huku, ni peponi kwa ujumla
 
Itakuwa unamiaka zaidi ya 10 huko Sweden, Mkuu
 
I can imagine mtu unavyochekelea kama ukirudishiwa kiwango kikubwa hivyo.πŸ€—πŸ€—

Wenzetu wanaelewa kwamba kuna watu ambao ,ndio wamelipa tax, ila kutokana na kipato chao hawakupaswa kulipa that much. Yani system yao inam[I]favor[/I] mwananchi kwa kila hali na kila namna. Sisi sasa.....😱😱
 
Pamoja na shida zote hizi bado group letu tulivyokuwa huko wote tulikumbuka bongo.
 
iii) Magari yote yanayotembea barabarani lazima yakaguliwe kila mwaka ili kujua kama bado yanakidhi vigezo vya kuwa barabarani.
Hapa kwetu yanakaguliwa yakiwa nyumbani na ithibati inatolewa hata mkiwa bar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…