Mambo 11 niliyoyaona Simba vs Gwanengy Galaxy leo

Mambo 11 niliyoyaona Simba vs Gwanengy Galaxy leo

Ni kama kuna remote ina control wachezaji wasifunge. Ila ukweli hatuna timu lawama zote ni kwa viongozi wamefanya usajiri wa kipuuzi sana.
 
Hakuna uchawi hapo, wachezaji mliosajili uwezo mdogo na wazoefu wamechoka. Kocha apewe muda asajili wachezaji anaowataka. Uzuri ni kwamba kocha ni mzoefu wa soka la Africa.
Kocha akipewa nafasi ya kusajili viongozi watapataje dili lao na hao atakahitaji timu ina fedha za kutosha?
 
1. Simba haijawahi kucheza mchezo wowote wa kimataifa msimu huu na kushinda, kumbuka hata kufuzu walifuzu kwa goli la ugenii.

2. Sio jambo la kawaida kwa timu kama Simba kucheza mechi za kimataifa na kuishia sare.

3.Sikubaliani na hoja kuwa wachezaji wa Simba ni wazee ila nakubaliana na hoja kuwa hawa wachezaji kuna kitu kimefanyika kwa wachezaji ili timu isipate ushindi.

4.Kwa yanayoendelea katika timu hii Benchika amekuja kujidhalilisha na muda sio mrefu yatamkuta kama.Robertinho.

5.Ushindi wa Simba utaendelea kuwa sare hadi mambo yatakapokaa sawa.

6.Viongozi wakubali kuwajibika ili wenye uwezo waongoze timu, kuendelea kung'ang'ania uongozi wakati matokeo sio mazuri sio sawa kabisa.

7.Brand ya timu imekufa kabisa kwa sababu sidhani kama mashabiki watakuwa na morali tena na hii timu.

8.Mnaweza kuwalaumu wachezaji lakn hata wajitume namna gani ngoma haiwezi kusimama tena kwa sababu wachezaji wameshafungwa miguu hao.

9.Wazee wa Simba wakiendelea kukaa kimya jahazi linakwenda mrama, muda bado upo.

10. Kama tumeshindwa kuwafunga Gwanengy leo basi msimu huu ni msimu wa ngedere.

11.Yanga leo atashinda dhidi ya Al Ahly na hali hiyo itazidi kuchochea mgogoro pale unyamani.
Watanzania wanaamini sana UCHAWI Sijui kwanini!!!!.
 
Hilo la kusema wachezaji wa Simba eti hawajitumi sio kweli ila hapo ndipo uwezo wao ulipofika, ule mkwaju wa Chama mbona ulizuiliwa na mwamba vinginevyo ilikuwa ni goli kabisa.
 
Back
Top Bottom