Mambo 12 Ya Msingi Kuhusu Usimamizi Bora Wa Nyumba Za Kupangisha Mwaka 2022

Mambo 12 Ya Msingi Kuhusu Usimamizi Bora Wa Nyumba Za Kupangisha Mwaka 2022

Aliko Musa

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2018
Posts
209
Reaction score
315
Maana Ya Usimamizi Bora Wa Nyumba.

Usimamizi bora ni hatua pekee za kuhakikisha kuna kipato endelevu, usalama wa uhakika, mahusiano mazuri, kutii sheria na taratibu za mtaa na nchi yako na kukufikisha kwenye uhuru wa kifedha.

Hatua hizi zinaweza kufanywa na mmiliki wa mali, au kampuni maalumu kwa ajili ya usimamizi wa mashamba, nyumba na viwanja na hata waajiriwa wa kampuni la ndani ya umiliki wa nyumba.

Mambo 12 Ya Msingi Kuhusu Usimamizi Bora Wa Nyumba.

Moja.

Faida Za Kuajiri Msimamizi Wa Nyumba Yako.

✓ Kupata punguzo ya kodi ya majengo.

✓ Kuongeza muda mwingi wa kutafuta mashamba, nyumba au viwanja vyenye manufaa makubwa.

✓ Kupata wapangaji sahihi.

✓ Kuwa na uwezo wa kuwekeza mbali na unapoishi na kuwa na changamoto chache za kisheria.

✓ Kuepukana na chanagamoto za wapangaji wasumbufu.

Mbili.

Mambo Muhimu Katika Ukusanyaji Wa Kodi Ya Pango.

✓ Kufahamu uuduma na sifa za jengo husika.

✓ Kufahamu tabia ya wapangaji.

✓ Kufahamu hali ya uchumi ya wapangaji.

✓ Kutambua viwanda vidogo karibu na nyumba.

✓ Kutathimini ukuaji wa idadi ya watu.

✓ Kutathimini ukuaji wa biashara na uwekezaji.

✓ Kutathimini ukuaji wa kipato kwa watu wa eneo husika.

✓ Kutathimini huduma muhimu kama vile shule, msitiki, kanisa, shopingi, karakana (gereji) na mgahawa.

Tatu.

Aina Nne Za Mapato Ambayo Unaweza Kupata Kutoka Kwa Msimamizi Wako.

✓Asilimia ya kodi ya pango,

✓ Ada ya kila mwezi kwa kila Pango,

✓ Kodi dhaminifu au kodi ya uhakika ya pango la nyumba na

✓ Mapato ya ushirika au gawio la mapato kutoka kwa msimamizi au kampuni la kusimamia.

Nne.

Kazi Za Msimamizi Wa Biashara Ya Nyumba.

✓ Usimamizi wa kutumia nguvu.

✓ Usimamizi wa rasilimali watu.

✓ Usimamizi wa mambo ya kifedha.

✓ Usimamizi wa masoko na matangazo.

✓ Usimamizi wa upangaji wa Pango.

✓ Usimamizi wa masuala ya kisheria, na

✓ Kutathmini hatari ya uwekezaji wenu.

Tano.

Mambo Yasiyopewa Kipaumbele Katika Usimamizi Bora Wa Nyumba.

✓ Kurudia mazungumzo kuhusu makubaliano ya kodi ya pango.

✓ Kusimamia majengo mapya.

✓ Kutathmini mahitaji ya wapangaji wako.

✓ Kuandaa mpango wa kupokea maoni.

✓ Kutafuta huduma za kisheria.

✓ Kuwa na ofisi au boksi au njia ya msaada kwa mpangaji.

✓ Kuongeza thamani nyumba yako.

✓ Kuandaa mpango wa kudumu wa kutafuta wapangaji wengi.

✓ Kuwa na ratiba maalumu, na daftari maalumu la mpangaji.

Sita.

Majengo Yanayoahitaji Usimamizi Mkubwa.

✓ Majengo ya migahawa.

✓ Vituo vya shopingi.

✓ Apatimenti kubwa.

✓ Majengo ya michezo.

✓ Hoteli, resoti na moteli.

Saba.

Changamoto Za Kuajiri Msimamizi Wa Nyumba.

✓ Kulipia kiasi kikubwa cha ada ya kusimamia nyumba.

✓ Kutumia gharama kubwa za ukarabati na marekebisho.

✓ Kuwepo kwa uuduma tofauti za wasimamizi.

✓ Uvivu na utepetevu wa baadhi ya wasimamizi wengi.

✓ Kushindwa kukusanya kodi kutoka kwa wapangaji kwa wakati.

✓ Huduma duni na za ovyo kwa wapangaji wasio na kosa lolote.

Nane.

Njia Za Kupunguza Chanagamoto Za Wasimamizi Wa Nyumba.

Kutofanya kazi na kampuni lenye wafanyakazi wa siku.

Kukataa kutoa malipo kabla ya kazi yoyote ile.

Kuchunguza kwa undani nyumba zinazouzwa kwa bei nafuu kuliko kawaida.

Kukataa huduma na bidhaa ambazo zipo nje ya bajeti na toa utaratibu wa kuwalipa wafanyakazi wako.

Kuwa na njia sahihi ya wapangaji wako kulipia kodi ya pango la nyumba.

Tisa.

Aina Za Ukarabati Wa Nyumba.

Ukarabati wa dharura, ukabarati wa marekebisho, ukarabati kinga, ukarabati wa kulinda au ulinzi na ukarabati wa mapambo.

Kumi.

Sifa Za Kuwa Msimamizi Wa Nyumba Kubwa.

Uwe na mbinu bora za mauzo na manunuzi ya mashamba, nyumba na viwanja.

Uwe na muda mwingi wa kusimamia mashamba, nyumba na viwanja. U

Uwe na nidhamu na ratiba yako, uwe unafuatilia mambo yahusuyo sheria bila kikomo.

Uwe unaweza kutawala hisia zako zinazoweza kuathiri usimamizi bora.

Uwe na uwezo wa kutumia kompyuta katika kufanikisha usimamizi bora wa nyumba zako.

Kumi Na Moja.

Maeneo Manne (4) Ya Kutathimini Usalama Wa Nyumba.

✓ Usalama dhidi ya ajali ya moto,

✓ Usalama dhidi ya kutokea kwa hewa chafu ikiwemo Kaboni monoksaidi.

✓ Usalama dhidi ya nguvu za umeme ikiwemo umeme wa radi.

✓ Usalama dhidi ya majanga ya asili kama vile volkano, na tetemeko la ardhi. Pia ukungu (mold au Mosses) ni fangasi hatari kwa afya ya mpangaji wako na ni hatari pia kwa uimara wa nyumba yako.

Kumi Na Mbili.

Njia Tano (5) Za Kutengeneza Kipato Cha Ziada.

✓ Kuandaa sehemu ya kufurahia nguo.

✓ Kuandaa ghala au chumba cha stoo,

✓ Kuandaa eneo la kuegesha vyombo vya usafiri.

✓ Kuandaa eneo la huduma za intaneti.

✓ Kuandaa samani kama vile meza na viti. Vitu vyote hivi utakodisha kwa wapangaji wako, majirani na kundi lingine la wateja.

Haya ni mambo ya msingi ya kuzingatia wakati wa kusimamia nyumba zako za kupangisha.

Pia, unaweza kutumia usimamizi mseto wa nyumba zako za kupangisha. Usimamizi mseto ni usimamizi ambao mwenye nyumba na msimamizi hushirikiana kwenye shughuli za usimamizi wa nyumba.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

WhatsApp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom