Mambo 12 yanayothibitisha kuwa Mungu aliumbwa na dini

Mambo 12 yanayothibitisha kuwa Mungu aliumbwa na dini

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Moja, haonekani.

Pili, anatetewa na binadamu.

Tatu, hakuna ushahidi wa kisayansi.

Nne, anaenezwa kwa imani na vitisho siyo ufahamu.

Tano, wanaomhubiri wanatofautiana na kuchukiana.

Sita, anapewa sifa nyingi kuliko zinazojulikana. Mfano, mtu anasema utoe sadaka ili Mungu akubariki.

Saba, utendaji wake una kila utata mfano, kwanini amuumbe mwanaume kwa udongo ashindwe kuutumia huo huo udongo kumtengeza mwanamke?

Nane, kwanini atoe mwanae mpendwa ili kusamehe dhambi? Anamtolea nani?

Tisa, ni mbaguzi anayependelea mashariki ya kati peke yake kama ni kweli.

Kumi, anaenezwa kwa nguvu, chuki na mapatilizi. Mfano, ukimtukana, wapo washenzi wanaotaka kukuua badala ya kumuache akuadhibu mwenyewe. Anatetewa utadhani kichanga au asiyekuwepo kama siyo kufa.

Kumi na moja, anatoa ahadi za ajabu ajabu kama wanawake makumi peponi au kuimba nyimbo milele utadhani wote wapenda kuimba.

Na kumi na mbili, anashindwa nguvu na shetani.
 
Back
Top Bottom