Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hapo namba 7 naye akiamuwa kufata huu ustaarabu itakuwaje?Mambo 13 ya busara
1. Ufikapo mahali ambako umealikwa usiketi kwenye kiti kabla ya kukaribishwa na mwenyeji wako.
2. Kama unakula mbele ya watu wengine usipende kuvutana na nyama ambayo ni ngumu. Nyama ngumu achana nayo.
3. Uendapo kwenye usaili wa ajira (kazi) usivae suruali bila mkanda huku ukiwa umechomeka shati. Pia usivae viatu ambavyo havina kamba.
4. Ukialikwa kwenye sherehe yoyote kula kwanza nyumbani kwako kabla ya kwenda kwenye sherehe.
5. Ukialikwa kwenye sherehe yoyote usinywe kilevi ambacho hujawahi kunywa (Usijifunze kunywa pombe eneo hilo).
6. Kama umeongozana na mtu ambaye mnaheshimiana (mama, baba, mke, mume, mkwe, kaka, dada, kiongozi, n.k) halafu umekutana na mtu ambaye mnafahamiana kidogo na mbaya zaidi umemsahau; usimuulize mliwahi kuonana wapi au kukutana wapi. Tafuta wakati mwingine ukiwa pekee yako umuulize.
7. Mtu unayemuheshimu usimpe salamu ya mkono kabla hajaanza kukupa yeye.
8. Kama mkuu (kiongozi) wako wa kazi atahitaji muende kwenye mualiko alioalikwa, usivae nguo (suits) ya kiwango cha juu kuliko ya mwenyeji (kiongozi) wako.
9. Usiongeze maneno mengine tofauti na maneno yaliyosemwa na kiongozi (mkuu) wako wa kazi, au msemaji wa eneo lako la kazi bila ruhusa yake.
10. Usimkosoe mkubwa wako mbele ya wageni wake. Tafuta wakati mwingine wa kumkumbusha kile alichokosea.
11. Ufikapo kwenye sherehe chukua chakula kinachokutosha. Usibebe chakula ambacho huna uhakika wa kukimaliza.
12. Kama unakunywa chai na mkate mbele ya watu wengine usiloweke mkate kwenye chai - hata kama hiyo ndo staili yako ya unywaji wa chai na mkate ukiwa kwako.
13. Usipende kusifia mambo ya mwanamke mwingine (kama vile urembo, n.k) mbele ya mkeo, sifa ambazo mkeo hana.....Usipende kusifu mambo ya mwanaume mwingine mbele ya mumeo (mambo ambayo mumeo hana).
~ Ongeza jambo lingine la Busara...
Right Marker
Dar es salaam
Oktoba 1, 2024
Uzima upo sana jombaaVishu uzima upo mkuu
20014. Mheshimu anayekupa utelezi
Namba 2 niligundua watu wananishangaa nikajishtukia😅2. Kama unakula mbele ya watu wengine usipende kuvutana na nyama ambayo ni ngumu. Nyama ngumu achana nayo.
ji
4. Ukialikwa kwenye sherehe yoyote kula kwanza nyumbani kwako kabla ya kwenda kwenye sherehe.
5. Ukialikwa kwenye sherehe yoyote usinywe kilevi ambacho hujawahi kunywa (Usijifunze kunywa pombe eneo hilo).
Yani hiyo ndio michezo tunaifanya kwenye shughuli zinazohusu vyakula Mkuu.utakuwa wale wakialikwa sherehe hubeba kamfuko umeme ukichezatu ukumbini wanatia minyama mifukoni
Nikajua tabia hii ni mimi peke yangu uroho wa nyama utakuja kunipeleka pabayaMkuu hiyo namba 2 ya kuvutana na nyama wenyeji watanisamehe ase.. siwezi kuacha nyama hata iwe ngumu vipi, ikinishinda kabisa nitameza.
qumaniner 😂😂😂😂14. Mheshimu anayekupa utelezi
Hahah, nyama sio ya kuacha kizembe utajilaumu sana. Kwanza raha ya nyama ni ucheze nayo isiwe legevu ikitafunwa kidogo tu imeisha.Nikajua tabia hii ni mimi peke yangu uroho wa nyama utakuja kunipeleka pabaya
Mchezo umalizikapo sema ukiwa na confidence --- thank you darling it was a lovely utelezi today so hot14. Mheshimu anayekupa utelezi
halafu we jamaa kunanakufananisha nae kutokana na id yako. bila shaka akili yangu haijanidanganya237. Ukipewa ofa ya kamnyeso na Tajiri unatakiwa kucheka hata kama kitu hakichekeshi.
Unlike14. Mheshimu anayekupa utelezi
In the voice of P didy.15:USIPENDE UCHAWA UNA GARAMA YAKE KWAKO
Asante kwa kutuongezea maarifa.Mambo 13 ya busara
1. Ufikapo mahali ambako umealikwa usiketi kwenye kiti kabla ya kukaribishwa na mwenyeji wako.
2. Kama unakula mbele ya watu wengine usipende kuvutana na nyama ambayo ni ngumu. Nyama ngumu achana nayo.
3. Uendapo kwenye usaili wa ajira (kazi) usivae suruali bila mkanda huku ukiwa umechomeka shati. Pia usivae viatu ambavyo havina kamba.
4. Ukialikwa kwenye sherehe yoyote kula kwanza nyumbani kwako kabla ya kwenda kwenye sherehe.
5. Ukialikwa kwenye sherehe yoyote usinywe kilevi ambacho hujawahi kunywa (Usijifunze kunywa pombe eneo hilo).
6. Kama umeongozana na mtu ambaye mnaheshimiana (mama, baba, mke, mume, mkwe, kaka, dada, kiongozi, n.k) halafu umekutana na mtu ambaye mnafahamiana kidogo na mbaya zaidi umemsahau; usimuulize mliwahi kuonana wapi au kukutana wapi. Tafuta wakati mwingine ukiwa pekee yako umuulize.
7. Mtu unayemuheshimu usimpe salamu ya mkono kabla hajaanza kukupa yeye.
8. Kama mkuu (kiongozi) wako wa kazi atahitaji muende kwenye mualiko alioalikwa, usivae nguo (suits) ya kiwango cha juu kuliko ya mwenyeji (kiongozi) wako.
9. Usiongeze maneno mengine tofauti na maneno yaliyosemwa na kiongozi (mkuu) wako wa kazi, au msemaji wa eneo lako la kazi bila ruhusa yake.
10. Usimkosoe mkubwa wako mbele ya wageni wake. Tafuta wakati mwingine wa kumkumbusha kile alichokosea.
11. Ufikapo kwenye sherehe chukua chakula kinachokutosha. Usibebe chakula ambacho huna uhakika wa kukimaliza.
12. Kama unakunywa chai na mkate mbele ya watu wengine usiloweke mkate kwenye chai - hata kama hiyo ndo staili yako ya unywaji wa chai na mkate ukiwa kwako.
13. Usipende kusifia mambo ya mwanamke mwingine (kama vile urembo, n.k) mbele ya mkeo, sifa ambazo mkeo hana.....Usipende kusifu mambo ya mwanaume mwingine mbele ya mumeo (mambo ambayo mumeo hana).
~ Ongeza jambo lingine la Busara...
Right Marker
Dar es salaam
Oktoba 1, 2024
Hahah na nani tena?halafu we jamaa kunanakufananisha nae kutokana na id yako. bila shaka akili yangu haijanidanganya
Jamani. nimejaribu kukutext PM lkn nimekutana na kufuri. ukute ni kweli ndugu yangu tumepotezana muda mrefu kama miaka mitano hivi. kama ni yule naemfikiria lkn. ila kama sio samahaniHahah na nani tena?
Kama wewe sio Mafwele tuendelee na mada.