Mambo 13 ya busara

Mambo 13 ya busara

Hii imekaa kinafiki sana ila tunaishi nayo

8. Kama mkuu (kiongozi) wako wa kazi atahitaji muende kwenye mualiko alioalikwa, usivae nguo (suits) ya kiwango cha juu kuliko ya mwenyeji (kiongozi) wako.
Mimi kwa hili atajijua mwenyewe mkuu wa kazi,,,Kwenye mambo ya kupendeza sinaga simile ni minyoosho kwa kadri itakavyoniwia kwa siku hiyo.
 
Kama maisha yamekuwa magumu mueleze ukweli mwenzako.

Mueleze ukweli ili na yeye afanye maamuzi yake.
 
Hii imekaa kinafiki sana ila tunaishi nayo

8. Kama mkuu (kiongozi) wako wa kazi atahitaji muende kwenye mualiko alioalikwa, usivae nguo (suits) ya kiwango cha juu kuliko ya mwenyeji (kiongozi) wako.
Na mimi nimejiuliza.
Utajuaje kama yeye atavaa ya kiwango cha chini wakati mnakutana tayari kila mtu kavaa ya kwake? Au unarudi kubadilisha?
 
Ikitoke Mtu kakujibu vibaya jitahidi tu kumuelewa na kumsamehe, Kuna time watu wanapitia mambo yasio Elezeka
 
hapo namba 7 naye akiamuwa kufata huu ustaarabu itakuwaje?
14. ukiwa kwenye kadamnasi wakat wa kula jitahd kula kistaarabu na kunywa pia kistaarab hata kama kwako umezoea kula rafuli 😄 specifically namna ya kutafuna & kunywa hapa wengi tunafeli....15 usipende kutafuna jojo kizembe huku umeachia mdomo na mawazo yapo ulaya 😄
 
Mambo 13 ya busara
1. Ufikapo mahali ambako umealikwa usiketi kwenye kiti kabla ya kukaribishwa na mwenyeji wako.

2. Kama unakula mbele ya watu wengine usipende kuvutana na nyama ambayo ni ngumu. Nyama ngumu achana nayo.

3. Uendapo kwenye usaili wa ajira (kazi) usivae suruali bila mkanda huku ukiwa umechomeka shati. Pia usivae viatu ambavyo havina kamba.

4. Ukialikwa kwenye sherehe yoyote kula kwanza nyumbani kwako kabla ya kwenda kwenye sherehe.

5. Ukialikwa kwenye sherehe yoyote usinywe kilevi ambacho hujawahi kunywa (Usijifunze kunywa pombe eneo hilo).

6. Kama umeongozana na mtu ambaye mnaheshimiana (mama, baba, mke, mume, mkwe, kaka, dada, kiongozi, n.k) halafu umekutana na mtu ambaye mnafahamiana kidogo na mbaya zaidi umemsahau; usimuulize mliwahi kuonana wapi au kukutana wapi. Tafuta wakati mwingine ukiwa pekee yako umuulize.

7. Mtu unayemuheshimu usimpe salamu ya mkono kabla hajaanza kukupa yeye.

8. Kama mkuu (kiongozi) wako wa kazi atahitaji muende kwenye mualiko alioalikwa, usivae nguo (suits) ya kiwango cha juu kuliko ya mwenyeji (kiongozi) wako.

9. Usiongeze maneno mengine tofauti na maneno yaliyosemwa na kiongozi (mkuu) wako wa kazi, au msemaji wa eneo lako la kazi bila ruhusa yake.

10. Usimkosoe mkubwa wako mbele ya wageni wake. Tafuta wakati mwingine wa kumkumbusha kile alichokosea.

11. Ufikapo kwenye sherehe chukua chakula kinachokutosha. Usibebe chakula ambacho huna uhakika wa kukimaliza.

12. Kama unakunywa chai na mkate mbele ya watu wengine usiloweke mkate kwenye chai - hata kama hiyo ndo staili yako ya unywaji wa chai na mkate ukiwa kwako.

13. Usipende kusifia mambo ya mwanamke mwingine (kama vile urembo, n.k) mbele ya mkeo, sifa ambazo mkeo hana.....Usipende kusifu mambo ya mwanaume mwingine mbele ya mumeo (mambo ambayo mumeo hana).
~ Ongeza jambo lingine la Busara...

Right Marker
Dar es salaam
Oktoba 1, 2024
Siku ukienda marekani jichunge SANA usikwenda nyumbani kwa p.diddy atakufanya kitu kibaya
 
Back
Top Bottom