Travis Walker
JF-Expert Member
- Apr 10, 2017
- 323
- 334
Habari kwenu wana wa JF.
Leo nimechukua nafasi ya kuandika makala hii ili ikusaidie katika suala la kuondoa haraka ili uwe na uwezo mkubwa wa kuvumilia.Haraka ni kitu kibaya sana.Mtu ambaye ana haraka mara nyingi anakuwa ni mjinga mbele ya jamii anaweza kuchukua maamuzi yaliokuwa sio sahihi halafu ikapelekea kujuta.Pia haraka inasababisha kufeli kwa mambo mengi sana na hukatisha tamaa mapema.Hata hivyo haraka husababisha kuharibika kwa mahusiano na kuto-elewana.
Tafiti za wanasayansi zinaonesha kuwa subira hufanikisha mambo katika maisha.Ila kujiongoza na kuidhibiti haraka hali hiyo inakuwa ngumu kwa kila mtu.Lakini haya mambo 4 ukiyafanya utajifunza kusubiri na hatimaye utakuwa unafanya mambo yako kwa uwerevu pasi na kukurupuka.
1.KUJIFUNDISHA KUSUBIRI.
Unapotaka kufanya kitu chochote jaribu kukichelewesha halafu pambana na hisia zinazokutia haraka kwa kutolifanya jambo hilo kwa muda huo.Njia hii itakufanya ujifunze kuvumilia.Ingawa ni ngumu kwa mara ya mwanzo ila kadri unavyofanya utaweza.
2.JARIBU KUJISEMEA NAFSINI.
Unapokuwa na haraka sana jisemee moyoni kwa kujipa nasaha ya kusubiri.Inasadikika kujisemea moyoni kunashawishi ubongo kubadilisha hisia kwa haraka.
3.JARIBU KUVUTA PUMZI HALAFU USITE
Unapohisi una haraka mno.Jaribu kuvuta pumzi halafu sita kwa sekunde 10 baadae ndipo ushushe pumzi tarartibu.Zoezi hili linafaa sana.
4.JARIBU KUPATA MUDA MZURI WA KULALA.
Kulala ni kupumua kwa ubongo.Hivyo kulala masaa machache kunapelekea kudhoofika kwa ubongo.Hivyo utakuwa na uwezo mdogo wa kujiongoza.hivyo unashauriwa kuapa alau masaa manane ya kulala .

KWA USHAURI, MAONI WHATSAPP NO.
0778867423
0778867423